Important Announcement
PubHTML5 Scheduled Server Maintenance on (GMT) Sunday, June 26th, 2:00 am - 8:00 am.
PubHTML5 site will be inoperative during the times indicated!

Home Explore MWANZO WA KUWA TAJIRI PREVIEW

MWANZO WA KUWA TAJIRI PREVIEW

Published by fikiaupeo, 2017-06-20 14:30:13

Description: MAHALI PA KUANZIA KWA MTU ALIYE NA MALENGO YA KUWA TAJIRI NA JINSI YA KUUSHINDA MFUMO UNAOKUFANYA UWE MASKINI

Keywords: Tajiri,Kutengeneza pesa,Duara la Thamani,Duara la Mwekezaji

Search

Read the Text Version

MWANZO WA KUWA MAHALI PA KUANZIA KWA MTU ALIYE NA MALENGO YA KUWA TAJIRI NA JINSI YA KUUSHINDA MFUMO UNAOKUFANYA UWE MASKINIVINCENT MABULA JILALA

Mwanzo wa Kuwa Tajiri©2017 Vincent Mabula Jilala. Haki zote zimehifadhiwaHairuhusiwi kuiga, kutafsiri, kupiga chapa au kukitoa kitabu hiki kwajinsi yoyote ile bila idhini ya mchapishaji na mwandishi.Duara la Thamani na Duara la Mwekezaji ni alama za kibiashara zaKampuni ya Fikia Upeo (Ltd). Duara la Thamani Duara la MwekezajiFikia Upeo Company LimitedS.L.P 369, BariadiSimiyu-TanzaniaBaruapepe: [email protected]: www.fikiaupeo.comToleo la kwanza- 2017ISBN: 978-9976-5118-0-2Kimepigwa chapa na: Niim Printers & Media ServicesS.L.P 10874Dar-es-salaam, TanzaniaBarua pepe: [email protected] ii

WAKFU……………………………………………………………………….Kitabu hiki nakiweka Wakfu kwa watu wote wanaotafuta nguvu zakuwafanya watumie karama, uwezo na vipaji vyao kuifanya nchi nadunia kuwa mahali pa Amani, Upendo, Furaha na Utajiri.……………………………………………......................................... iii

SHUKRANIAwali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa huduma hii ya uandishi na ufundishaji ili kujenga mahali palipobomokakatika watu wake. Utukufu na heshima na nguvu vina yeye daima namilele. Amina Pia ninawashukuru wazazi wangu Mzee Jilala Jinyeu na mamayangu Maria Shiwala kwa kunilea katika maadili mazuri hatimayenimekuwa jinsi nilivyo. Bila kuwasahau ndugu zangu kaka na dadazangu, ninawapenda sana, Mungu awabariki. Kwa nafasi ya pekee nawashukuru Mheshimiwa Anthony Mtaka(Mkuu wa Mkoa wa Simiyu), Jumanne A. Sagini (Katibu Tawala waMkoa wa Simiyu) na Jomaary M. Satura (Mkurugenzi wa Manispaa yaLindi) kwa mchango wao wa hali na mali katika kufanikishakupatikana kwa kitabu hiki. Shukrani ziwaendee, Eng. AlfredNghwani, Protas A. Ringo, Jane Lwakabamba, Rosalia Magotti,Donatus A. Weginah, Hatari Kapufi, Chele Ndaki na Deusdedit R.Mshuga kwa mchango wao muhimu katika kufanikisha kupatikanakwa kitabu hiki. Nawashukuru sana Bwana Charles Maganga, Addo A.Komba na Bi. Jusline Gilbert kwa mawazo na ushauri wao hasausanifu na mpangilio wa Lugha, nawashukuru sana kwa kazi hiyonzuri. Namshukuru rafiki yangu na mshirika wangu katika kampuni yaFikia Upeo, Bwana Sebastian M.John kwa kazi kubwa aliyoifanyahatimaye kupatikana kwa kitabu hiki. Nawashukuru wadau na rafikizangu kwa jitihada zao kubwa katika kufanikisha kitabu hiki baadhiyao ni;- Gogard Jilala, Charles M. John, Principius G. Karumuna,Erick Mwaipeta, Musa L. Mponeja, Deodatus M. Mushi, Juakali iv

Maganga, Grace Mgombera, Kilonzo Philipo, Sima Sayenda, Majid C.Ndongolo, Lazaro Magumba, Faraja J. Mmasa, Ernest S. Mbwana,George G. Mbena, Asanath M. Nimwobaruga, Stella Kalinga, HawaFilbert, Florenciana Kagya, Dr. Olais Ngilisho, Exaudi Tegemea,Mahobe Singu, Fadhili Wilhem, Ally R. Mzee, Imani Matimbwa,Erick Ndelwa, Mika M. Mollel, Mustapha Kimomwe, Edga Mdemu,Elias Carlos, Rashid Mchalaganya, Mathias P. Shineneko, OdiloKachete, Proches E. Tumaini pamoja na marafiki zangu wenginewote kwa maarifa na weledi wao katika kufanikisha kupatikana kwakitabu hiki. Kwa namna ya pekee kabisa nawashukuru walezi wangu kiroho kwakazi kubwa waliyoifanya ya kunilea. Hawa si wengine bali ni Pd.Kizito Nyanga, Pd. Vincent Masuke na Pd. Richard Makoye. Wengineni baba yangu mlezi wa kiroho Mwalimu Steven Pius asante baba kwamalezi yako mazuri. Mwisho shukrani zimwendee mke wangu Sipora kwa upendo wakemkubwa ulionifanya niwe jinsi nilivyo. Mungu azidi kumbariki. v

YALIYOMODibajiUkiwa Tajiri Itakuwaje?..................................................xiUtanguliziNguvu Iliyotoka Ndani ya Gideoni Siku Alipoambiwa Yeyeni Shujaa ........................................................................ 1 SEHEMU YA KWANZA: KWANINI KUNA UMASKINI?Sura ya KwanzaVitu Vipya na Vya Kale.................................................. 16 Mjadala Nikiwa na Rafiki Yangu Musa............................................17 Historia ya Maendeleo ya Binadamu..............................................20Sura ya PiliDuara la Thamani ......................................................... 28 Duara la Thamani Nini?...................................................................28 Teknolojia ni Nini? ..........................................................................44Sura ya TatuElimu Tunayosoma Kwenye Mfumo Wetu wa ElimuImeshindwa Kutatua Tatizo la Umaskini....................... 63 Mazungumzo na Wanafunzi ...........................................................64 Simu ya Meneja ..............................................................................67 Kijana Aliyefeli.................................................................................69 Njia Fupi. .........................................................................................74 Njia Ndefu. ......................................................................................83 vi

Safari ya Ndege ...............................................................................84 Nani Anaye Tawala?......................................................................103Sura ya NneAkili Zinapofikia Ukomo wa Kufikiri ............................ 106 Nini Hasa Madhumuni ya Sura Hii?...............................................106 Kipato Cha Lena Maria..................................................................113 Wazazi na Watoto Wao ................................................................120Sura ya TanoVitu Vilivyotengenezwa.............................................. 122 Mazungumzo na Mwenyekiti........................................................122 Pande Mbili za Shilingi ..................................................................130Sura ya SitaNguvu ya Dini Kutufanya Kuwa Matajiri au Maskini ... 132 Mitazamo Juu ya Dini....................................................................133 Kwenye Dini Kuna Siri Yoyote? .....................................................135 Maswali ya Kujiuliza......................................................................152 SEHEMU YA PILI CHAGUA KUWA TAJIRISura ya SabaKuwa Tajiri ni Maamuzi Yako Binafsi .......................... 155 Kujiuliza Swali la “Kwanini?” .........................................................155 Nilichokiona ..................................................................................157 Kazi Ngumu Kuliko Zote ................................................................161 Ubongo Tupu ................................................................................162Sura ya NaneChukua Hatua............................................................. 165 vii

Utamu wa Maisha.........................................................................165 Falsafa Yangu: “Maisha Ni Mchezo” .............................................169 Siasa ni Mchezo.............................................................................170 Nataka Kuwa Tajiri ........................................................................171 Maisha Matamu Nimepata Jibu Lake ...........................................172 Kwanini Nataka Tuwe Matajiri......................................................173 Utajiri Ni Nini au Ukiwa na Mali Kiasi Gani Ndipo Uitwe Tajiri? ...175 Bado Unataka Kuwa Tajiri? ...........................................................179 Kutafuta au Kutengeneza Pesa? ...................................................183Sura ya TisaMaarifa na Teknolojia Unayopaswa Kuwa Nayo......... 190 Kujua Kusudi la Kuumbwa Kwako.................................................190 Nimeumbwa Nifanye Nini?...........................................................192 Kufahamu Kusudi La Kuumbwa Kwako ni Jambo la Kiroho. .........194 Utajiri na Kusudi la Kuumbwa Vinapingana? ................................195 Mahali Unapoweza Kujifahamu na Kufahamu Aina za Watu. ......196Sura ya KumiWeka Malengo Makubwa Anza Kidogo Kidogo .......... 201 Mkutano Mkuu wa Makandarasi..................................................201 Kuufikia Utajiri ..............................................................................206 Unawezaje Kumla Tembo? ...........................................................207 Kijana Kando Kando ya Bahari ......................................................208 Malengo ni Nini?...........................................................................209 Mchwa Hawana Mifupa Lakini Wanafanya Maajabu ...................213 Kuwa Tajiri ni Kutatua Matatizo ya Watu .....................................213 SEHEMU YA TATU: MAHALI UTAJIRI UNAKOPATIKANA viii

Sura ya Kumi na MojaAkili ni Mahali Utajiri Mkubwa Ulipo.......................... 216 Mwanamke na Mtoto Wake Jangwani .........................................216 Jinsi ya Kutumia Akili Ili Zikuletee Utajiri. .....................................225Sura ya Kumi na MbiliNguvu ya Mtandao wa Intaneti .................................. 229 Maana ya Intaneti.........................................................................230 Nini Kinapatikana Kwenye Intaneti?.............................................231 Ubunifu na Uendeshaji na Miradi.................................................242 Utaanzaje Kufanya Biashara Kwa Njia Ya Mtandao wa Intaneti? 247 Sina Utaalamu Wowote wa Kutumia Compyuta Nitafanyaje? .....251 Njia ipi Unapitia?...........................................................................257 Je, Nitakuwa Tajiri? .......................................................................258Sura ya Kumi na TatuNguvu ya Biashara...................................................... 264 Maana ya Biashara........................................................................264 Kufanya Biashara kwa Kutumia Makampuni ................................270 Kampuni Yako Ifanye Biashara Gani? ...........................................280 Nguvu ya Sheria Katika Biashara...................................................286 Kupata Mtaji wa Kuanzisha Biashara ............................................293 Kwanini Kama Taifa Tunahitaji Wafanya Biashara Wengi Zaidi?..297Sura ya Kumi na NneNguvu ya Uwekezaji…………………………………………….......304 Siri ya Mafanikio............................................................................304 Uwekezaji ni Chanzo Cha Uvumbuzi na Ugunduzi........................309 Kwanini Uwekezaji Hufanya Wawekezaji Wazidi Kuwa Matajiri ..309 Umuhimu wa Nchi Kutengeneza Wawekezaji Wazawa................316 ix

Kweli Unataka Kuwa Tajiri?...........................................................319Sura ya Kumi na TanoJinsi Wafanya Biashara na Wawekezaji WanavyowezaKuendesha Biashara Nyingi kwa Wakati Mmoja......... 322 Maswali Magumu .........................................................................322 Kwanini Serikali ni Tajiri? ..............................................................332Sura ya Kumi na SitaKitu Gani Wazazi Wawafundishe Watoto Wao KuhusuUtajiri? ....................................................................... 336 Hadithi ya Vijana Wasio na Kazi....................................................336 Mafundisho ya Kujenga Fikira za Utajiri kwa Watoto...................345 Nguvu Tano za Kuupata Utajiri .....................................................360HitimishoNjia Tatu Maamuzi Matatu ........................................ 361 x

Dibaji UKIWA TAJIRI ITAKUWAJE?Utajiri si kitu isipokuwa ni Nguvu. Ni nguvu inayokuwezesha kufanya mambo mengi unayoyatamani katika maisha yako.Ukiwa tajiri utasaidia watu wengi katika nchi yako wanaopungukiwamahitaji yao, utajenga nyumba nzuri unayoitamani, utajenga nyumbanyingi kwa ajili ya mikutano ya kiroho, utasomesha watoto wakopopote duniani, utatembea dunia nzima na kujionea kila unachokitakakwa wakati wake, utanunua usafiri wako unaoutamani pasipomaumivu ya namna ya kuuhudumia, utajenga kila aina ya viwandaunavyovitamani, utafanya kila kitu unachokitaka hapa duniani lakinipia utajenga jamii bora yenye furaha na upendo pale utajiri wakoutakapoutumia kuwahudumia watu. Hivi ingekuwaje, kama ukitaka kununua gari ya kifahari leounainunua bila mawazo ya wapi upate pesa? Au ukitaka kusafirikwenda bara jingine huhaingaiki kuwaza kuhusu nauli, ukitakakujenga hospitali unaijenga muda wowote bila kuumiza kichwakuhusu pesa, ukitaka kula chakula kizuri unachokitaka unakula bilakujiuliza pesa zitatoka wapi, ukitaka kufanya jambo lolote unalifanyakwa wakati wake, ingekuwaje kama mambo hayo yote ungewezakuyafanya kwa wakati wake bila kujiuliza uliza kuhusu pesa? Utajiri ninguvu inayokuwezesha kufanya kila jambo unalotaka kwa wakatiwake. xi

Umaskini ni kinyume chake, unaweza kuona kila kitu lakini huwezikufanya kitu chochote. Utaona magari mazuri ya kifahari lakini huwezikununua ya kwako, utaona watoto wa wenzio wanasoma shule nzuri,utaona watu wengine wakijenga nyumba nzuri za ghorofa, utaonawakisafiri kwa ndege angani, utaona wakila chakula kizuri, utaonawakifanya kila kitu wanachokitamani ili hali wewe huwezi kufanyachochote. Umaskini ni kama vile umefungwa pingu isiyoonekana au nikama vile umefungwa kwenye chumba cha vioo pande zote ambapounaweza kuona nje kila kitu lakini huwezi kutoka. Umaskinihumfanya mtu achakae na wakati mwingine ashindwe kutumia vipajina karama zake zote alizopewa na Muumba wake kwa sababu kila kitukwake kinaukomo. Bahati nzuri ni kwamba kuwa tajiri au maskini ni jambo lakuchagua. Unaweza kuchagua kuwa tajiri au maskini, hakuna mtuanayekuchagulia ni maamuzi yako. Tofauti iliyopo kati ya kuwa tajirina kuwa maskini ni gharama. Ukitaka kuwa maskini utalipa gharamayake na ukitaka kuwa tajiri vile vile utalipa gharama. Moja ya gharamakubwa mtu huilipa ili kuwa tajiri au maskini ni MUDA. Unawezakuulipa muda wako kwenye mambo yanayokufanya uwe maskini aukwenye mambo yanayokufanya uwe tajiri. Kwa mfano, mtu mmojaanaweza kuulipa muda wake kwenye kujifunza yaani kutafuta maarifana mtu mwingine anaweza kuulipa muda wake kwenye kushindavijiweni akipiga soga. Watu hawa wawili hawatafanana kiuchumi kwasababu ya gharama ya muda wanaoulipa.Njia Mbili Mtoto anapozaliwa huwa hajui kitu chochote kilichopo duniani.Mimi huwa nasema anakuwa na Ubongo Tupu (empty brain). xii

Ubongo tupu maana yake anakuwa na ubongo usiokuwa na akilindani yake ya mambo ya duniani. Watu wote tumezaliwa tukiwa naubongo tupu hatukujua chochote kilichopo duniani, yote tunayoyajuahivi sasa tumejifunza hapa duniani. Watoto 100 wa nchi mojawakizaliwa siku moja, njoo uwatazame baada ya miaka hamsini;utakuta wengine ni matajiri na wengine ni maskini. Matabaka haya yaumaskini na utajiri yanapatikanaje ili hali wote wanaishi ndani ya nchimoja na walizaliwa siku moja? Huenda kukawa na sababu kadhaazinazowatofautisha, lakini moja ya sababu kubwa ni MAAMUZIWANAYOYACHUKUA. Kuna njia mbili mtu anazoweza kuchagua kupita, kuna njia yaUmaskini na kuna njia ya Utajiri. Kama nilivyokuelezea hapo awalitofauti ya njia hizi mbili ni gharama. Njia ya umaskini huhitajikuichagua, hata usipoichagua yenyewe iko moja kwa moja(automatic), usipochagua njia ya utajiri moja kwa moja utakuwaumechagua njia ya umaskini. Moja ya kazi ngumu nilizowahi kuzionahapa duniani ni kuchagua kuwa TAJIRI. Watu wengi wameshindwakuchagua utajiri kwa sababu ya hofu iliyomo kwenye utajiri, hofu hiiinaletwa na gharama za kuwa tajiri. Miaka michache iliyopita nilikuwa na mgogoro mkubwa nafsinimwangu kuhusu kuwa tajiri au maskini. Nilikuwa napingana ndaniyangu, upande mmoja ukiniambia nataka kuwa tajiri, upandemwingine unapinga kwa kuogopa gharama ya kuwa tajiri. Nilikuwanasikia watu wakisema, “Kuwa na pesa nyingi hakuna raha, unaishikwa wasiwasi hupati usingizi mzuri kama apatao kibarua, matajiriwengi ni wachoyo hawawajali hata ndugu zao, tena matajiri ni vigumukwenda mbinguni, usitumikie mabwana wawili, heri uwe na pesa xiii

kidogo za kutosheleza mahitaji yako kuliko kuwa na mali nyingi, malinyingi ni mzigo, matajiri wengi wanadhulumu watu, wanatumianguvu za giza kupata utajiri wao,” na maneno mengine mengi.Maneno hayo yalinikatisha tamaa kabisa ya kuwa tajiri. Kadri siku zilivyozidi kwenda, nikapata akili ya kufanya maamuzi,nikachagua moja kati ya kuwa tajiri au kuwa maskini. Nilichaguakuwa tajiri. Mara nilipochagua kuwa tajiri ndani yangu nikapataumoja, ule upinzani ukapotea nikaanza kuchukua hatua kwa vitendoza kuelekea kwenye utajiri. Kwa hiyo unaweza kuona jinsi gani ilivyovigumu kuchagua kuwa tajiri na ni rahisi kuchagua kuwa maskini kwasababu huhitaji kuchagua kuwa maskini kwani iko moja kwa mojakama hujachagua kuwa tajiri moja kwa moja umeshachagua kuwamaskini.Uko Tayari Kupigana? Siyo kupigana na mtu bali kupigana na Umaskini, kwa sababutangu nikiwa mtoto mdogo nilikuta wanasema umaskini ni ADUI,hata sasa nakiri hivyo kwamba Umaskini ni adui, adui wa nini? Niadui wa kutuzuia tusimiliki vitu vizuri tunavyovitaka katika maishayetu. Sasa nakuuliza, uko tayari kupigana ili tumshinde adui huyu?Kama jibu ni NDIYO, basi kitabu hiki kitakuwa msaada kwako kwaajili ya kufahamu siri na nguvu za adui huyu, hivyo basi baada yakumaliza kukisoma utapata mahali pa kuanzia kumpiga huyu adui. Lakini unafahamu jinsi ilivyo vigumu kupigana na aduiusiyemwona kwa macho? Inahitaji maarifa na nidhamu ya kutoshavinginevyo haiwezekani kumshinda kabisa. Nikualike basi kukisomakitabu hiki, lakini ninachopenda uwe nacho kichwani mwako wakatiunakisoma ni kwamba FIKIRA zako ziweke mkao wa kiaskari, maana xiv

yake mkao wa kupigana na adui huyu na kumshinda. Maarifa nanidhamu vitatusaidia kumshinda adui huyu. Tahadhari nyingine ni kwamba pesa na moyo zinatabia yakushikana kwa nguvu. Moyo wa mtu ukishikana na pesa kwa nguvu,mtu huyo huharibikiwa kabisa. Hatajali tena haki wala uzalendo, walakumpenda Mungu kunatoweka ndani yake, hali hiyo inaitwa,“Kupenda Pesa,” hali hiyo ikifikia ndipo pesa inakuwa mungu. Lakinipia siku pesa zikipotea ghafula kuna uwezekano mtu huyo akapatamadhara makubwa kama vile kurukwa akili au kuchanganyikiwa.Kitabu hiki kinakufundisha jinsi ya kutoiruhusu pesa ishikamane namoyo wako ili isikudhuru. Karibu sana. xv

Utangulizi NGUVU ILIYOTOKA NDANI YA GIDEONI SIKU ALIPOAMBIWA YEYE NI SHUJAAGideoni mwana wa Yoashi alikuwa mtu maskini; yeye na familia yake na ukoo wake wote. Umaskini huo ulimfanya awemnyonge, na kwa sababu ya maadui wao yaani taifa jirani, ilimlazimuawe anashinda shambani kwenye shimo mithili ya handaki akipepetangano ili kuificha wasije maadui wakamteka na kuichukua ngano hiyo,labda na kumdhuru yeye. Alikuwa ni mtu asiye na matumaini hatakidogo. Siku moja malaika akamtokea na kumwambia, “Bwana yu pamojanawe, ee shujaa.” Maneno yale ya kuambiwa yeye ni shujaahayakuingia akilini mwake kabisa. Alitazama uhalisia wa maisha yake;yupo kwenye shimo akipepeta ngano, jamaa zake wote ni maskini, nayeye mwenyewe ni mdogo kuliko wote katika nyumba ya baba yake.Sasa, ataambiwaje yeye ni shujaa?. Malaika akamwambia tena,“Enenda ukawaokoe watu wa taifa lako dhidi ya mkono wa adui kwauwezo wako huu.” Japo mwanzoni hakuelewa maneno ya malaikalakini baadaye alielewa na akakubali kwenda kuliokoa taifa lake, naalifanikiwa kuliokoa. Unaweza kufuatilia hadithi hiyo kwenye Biblia. Kama kuna mambo yanayochanganya akili ni pale unapoambiwaufanye jambo kubwa wakati unaona huna uwezo wa kulifanya.Gideoni aliambiwa akawaokoe taifa lake dhidi ya maadui kwa uwezowake. Alipata wapi uwezo wakati ni maskini yeye na ukoo wake 1

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilalawote?. Licha ya hilo, alikuwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa kwa babayake yaani mdogo kuliko wote katika familia ya mzee Yoashi, sasa huouwezo ameupata wapi wa kuokoa taifa zima?. Tangu siku alipoambiwana malaika kwamba yeye ni shujaa, maisha yake yalibadilika sana,kwani tangu siku hiyo alianza harakati za kulikomboa taifa lake dhidiya maadui na alifanikiwa kuwakomboa, na sio kuwakomboa tu balimaadui zake aliwapiga na kuwashinda kwa muda wa miaka arobaini. Umewahi kujiuliza, tunao akina Gideoni wangapi katika nchi yetuambao hivi sasa wapo shimoni wanapepeta ngano? Tena umewahikujiuliza kwamba huenda wewe ndiye Gideoni, hivi sasa unapepetangano, maisha ni magumu, huna mwelekeo, ni maskini wewe nafamilia yako na ukoo wako? Zaidi ya hayo, unafahamu kwamba nguvuza kukufanya uwe shujaa ziko ndani yako?. Kitabu hiki kinalenga kukupatia mbinu za kutumia nguvu zilizomondani yako ili uzitumie kwa ajili ya kufanikiwa kwako kiuchumi nalabda unaweza kufikia kuitwa tajiri. Haijalishi ikiwa hivi sasaunapepeta ngano, kinachojalisha ni maamuziutakayoyachukua baada ya kukisoma kitabu hiki katikakuzitumia nguvu zilizomo ndani yako, kwani si kila mtu kitabu hikikitamhusu bali yule tu ambaye ana nguvu ndani yake hajazitumia kwaajili ya kumletea utajiri na yupo tayari kuzitumia zimletee utajiri.Kwanini Nimeandika Kitabu Hiki? Nimeandika kitabu hiki kwa sababu ya Mwalimu anayenifundisha.Yupo mwalimu anayewafundisha watu wote kwa namna apendavyoyeye. Mwalimu huyu hutamkuta akiongea wala kuandika chochote 2

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilalawala hutasikia akipaaza sauti yake. Humfundisha kila mtu kwa njia yamatendo kwa jinsi apendavyo. Jina lake anaitwa MAISHA. Kipindi kile nasoma sekondari na baadaye nilipokuwa chuoninilipitia mazingira magumu sana ya kiuchumi. Nyumbani kwetu haliya uchumi ilikuwa mbaya kiasi kwamba hata ada za kulipia masomozilikosekana. Kipindi hicho nilikuwa nawaza kwamba, “Nikimalizachuo nikapata ajira, hali yangu kiuchumi itakuwa nzuri.” Mungu siAthumani akanisaidia nikamaliza chuo na bahati nzuri nikapata ajiramapema. Baada ya kuanza ajira, nikashangaa!, sikuona yale matarajio mazuriya kiuchumi niliyoyatarajia kuyapata kwenye ajira. Hali yangukiuchumi ilizidi kuwa mbaya mno. Ilifika hatua nikawa mtu wakukopa na kulipa madeni kila siku. Marafiki zangu wote nilikuwanimewakopa hata nilikosa mtu wa kumkopa tena. Mama yangu aliugua na dada yangu naye alikuwa anaumwa.Familia yangu na familia ya wazazi wangu zilinitegemea. Ilifika hatuamichango ya harusi na matukio mbalimbali ya kijamii sikuwezakuchangia kwa sababu sikuwa na pesa kabisa. Mshahara ulikuwahaumalizi wiki umeshaisha. Kwa ujumla maisha yalikuwa magumusijawahi ona tangu nizaliwe. Kwa nje nilionekana Afisa, lakinikiuchumi sina kitu. Mahangaiko hayo ya kiuchumi yaliamsha NGUVU iliyomo ndaniyangu na kunipelekea kuanza kuchunguza kwa makini jinsi watuwengine wanavyofanya hadi wanakuwa matajiri. Lakini pia yalinipakiu ya kuamua kuwa tajiri. Ingawaje utajiri hautatatua matatizo yotelakini utasaidia kupunguza baadhi ya mambo yanayowezekana 3

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilalakupunguzwa. Nakiri wazi wazi mchana kweupe kwamba, umaskini niMBAYA. Nimeonja nimeona. Mwalimu wangu Maisha amenifundishakuona jinsi umaskini unavyo kaba koo, lakini pia amenisaidia kunipaufahamu kwa ajili ya kuwafundisha watu wengine ili nao wawezekujikomboa kiuchumi. Mwalimu Maisha, amenisaidia kunipa ufahamu wa kufahamubaadhi ya siri za kupata utajiri. Hapa nakueleza baadhi ya siri hizoambazo utajifunza kwa kina katika sura za mbele za kitabu hiki;- a) Matajiri hawategemei akili zao pekee ili kupata utajiri. Bali pamoja na akili zao hutumia na akili za watu wengine. Hata Mwenyezi Mungu anasema kwenye maandiko matakatifu kwamba usizitegemee akili zako, ona anavyosema;. “Usijitaabishe ili kupata utajiri; acha kuzitegemea akili zako mwenyewe” (Mithali 23:4). Maana yake ni kwamba ili utajirike jifunze kutumia akili za watu wengine, ndio maana watu matajiri hawakomi kujifunza kwa namna mbalimbali kama vile kusoma vitabu, kushiriki semina nakadhalika. Lakini pia huajiri wahasibu, wanasheria, mameneja na watu wengine ili kupata utajiri. Watu maskini hutegemea akili zao pekee ndiyo maana ni maskini. b) Kuna tofauti ya kutafuta pesa na kutengeneza pesa. Wazo hili lilikuwa jipya kabisa kwangu. Kutengeneza pesa ni KUTEGA PESA KWA MITEGO na kutafuta pesa ni KUIFUKUZIA PESA. Pesa siku zote haitaki kuonwa, kwa hiyo mtu akiifukuza pesa ataipata kwa taabu sana, kumbe watu matajiri hawafukuzi pesa bali huitega pesa kwa mitego inayoitwa VITEGA UCHUMI. Kwa mara nyingine tena Mwenyezi Mungu naye 4

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilala anazungumza jambo hilo akisema pesa inayo mabawa; “Je, utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, kama tai arukaye mbinguni” (Mithali 23:5)c) Elimu tunayosoma haitufundishi jinsi ya kupata utajiri. Baada ya kumaliza chuo nikapata ajira, maisha yakawa magumu zaidi. Kilichonitesa zaidi ni kwamba, nilijikuta sina mbinu nyingine yoyote ya kunisaidia kuongeza kipato tofauti na ajira. Ndiyo maana baada ya kutafiti kwa kina kuhusu elimu yetu nikabaini kwamba watu wengi walio kwenye ajira kwa maana ya Watumishi hawatumii rasilimali zilizomo nchini kuongeza kipato chao. Utajifunza zaidi jambo hili katika Sura ya pili na ya tatu ya kitabu hiki.d) Kuna nguvu wanazotumia matajiri ili kuupata utajiri. Nguvu hizo zipo za namna nyingi lakini mimi nimeziainisha nguvu tano ambazo binafsi ninaziamini zitanisaidia, labda na wewe zinaweza kukusaidia. Kadri unavyozidi kukisoma kitabu hiki utaelewa namna zinavyotumika ili kuleta utajiri. Nguvu hizi ni; i. Nguvu ya Kampuni ii. Nguvu ya Intaneti iii. Nguvu ya Biashara iv. Nguvu ya Uwekezaji v. Nguvu ya Neno la Mungue) Watu wengi hawawafundishi watoto wao jinsi ya kupata utajiri. Mimi ni mfano halisi, wazazi wangu hawajanifundisha chochote kuhusu utajiri. Laiti kama ningelifundishwa nyumbani na wazazi wangu jinsi ya kupata utajiri, huenda ningelikuwa nimejiandaa mapema kiuchumi. Utafiti mdogo 5

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilala nilioufanya nikabaini kwamba ni familia nyingi haziwafundishi watoto wao jinsi ya kupata utajiri. Sehemu ya tatu ya kitabu hiki imetoa mwongozo wa jinsi ya kuwafundisha watoto ili baadaye waje kuwa matajiri. Hizo ni baadhi tu ya siri za kuupata utajiri, kwa kukisoma kitabuhiki kuna mambo mengi mapya ya kiuchumi na fedha utayapata. Niimani yangu kwamba huenda ukawa mwanzo wako wa kuwa tajiri.Mambo Yamebadilika Zama zimebadilika na nyakati zimebadilika, namna ya utendaji kazikwa ajili ya kujipatia kipato vile vile imebadilika sana. Teknolojiainabadilika kila baada ya miaka miwili kama alivyosema Mfanyabiashara wa Kimarekani na Mwanzilishi wa kampuni ya Intel,“Gordon Earle Moore” kwenye kanuni yake inayoitwa ‘Kanuni yaMoore.’ Kutokana na kasi kubwa ya mabadiliko, watu ambao wamekuwahawabadiliki kulingana na ukuaji wa teknolojia wanajikutawanashindwa kukua kiuchumi kwa sababu wanatumia njia zile zile zazamani ambazo zimepitwa wakati. Ajira zitaendelea kupungua kila sikukwa sababu teknolojia inakua kwa kasi, wakati hatujaandaliwakukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira. Kuanzia miaka ya 1980 kulipogunduliwa mtandao wa intanetiinakadiriwa kuwa ndiyo mwanzo wa zama mpya inayoitwa “Zama zaTaarifa (Information Age) au kwa jina jingine inaitwa Zama zaKidigitali (Digital Age)” kwa mujibu wa Wikipedia (Freeencyclopedia). Zama hizi ni tofauti kabisa na Zama iliyopita ambayo 6

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilalailikuwa inaitwa Zama za Viwanda (Industrial Age). Tofauti inatokanana nini? Tofauti inatokana na namna ya kupata kipato. Kwenye Zama za viwanda, kutokana na mapinduzi ya viwanda kuleUlaya karne ya 17, kulihitajika wafanyakazi wengi kwenye viwanda,kwa hiyo watu wengi walisoma na walipomaliza masomo yaowaliajiriwa kwenye taasisi ama makampuni yaliyokuwa yanashughulikana uzalishaji mali viwandani. Hapo ndipo utaratibu wa ajiraulipotiliwa mkazo sana, ingawaje hata kabla ya miaka hiyo yamapinduzi ya viwanda utaratibu wa ajira ulikuwepo lakini ulishika kasikubwa kwenye mapinduzi ya viwanda. Kwenye Zama hizo za Viwanda, watu walisoma sio kwa faida yaopekee bali kwa faida ya wenye pesa. Ninasema hivyo kwa sababuwasomi wengi walipokuwa wanamaliza masomo yao ya chuo,wasipopata ajira, elimu yao ilionekana kana kwamba haina faida kwaokiuchumi, kwani walikuwa wanakaa hata miaka mingi wakisubiri ajira. Kipindi cha Zama za Viwanda ndipo matabaka ya watu matajiri,watu wenye kipato cha kati na watu maskini yalipoanza. Matajiriwalikuwa ni wazalishaji wakubwa kama vile wafanya biashara nawawekezaji, wenye kipato cha kati walikuwa ni vibarua ambaowaliajiriwa na matajiri, huku watu wasio na ajira na ambao sio wafanyabiashara ama wawekezaji wengi wao walibaki kuwa maskini. Wale waliobahatika kuwa viongozi kwenye makampuni ya matajiriwalionekana wanapewa sifa kubwa katika jamii. Ilikuwa mtu akisemani Meneja wa benki au Mkurugenzi wa kampuni fulani au Mhasibuwa shirika fulani ilikuwa ana heshimika sana. 7

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilala Hali imebadilika katika Zama hizi za Taarifa, kwani kutokana nakukua kwa teknolojia, ajira zinaendelea kupotea na kupungua sana.Kinachotia wasiwasi ni kwamba watu wengi hatuko makini na jambohili kwani bado tunahimiza watoto wetu wasome mpaka chuo kishawatafute ajira, ndiyo maana unaweza kuona wasomi wengi wapomtaani hawana ajira wakisubiri kupewa ajira, hali hii inaendelea kuwambaya zaidi. Kwenye Zama hizi, mfumo wa kupata kipato umebadilika mno, siotena zama za kutegemea ajira pekee, bali mfumo wa kupata kipatokwenye Zama hizi ni kutumia taarifa kutengeneza pesa, kwa njia yabiashara, ujasiriamali na uwekezaji ili kutajirika. Wasiotumia taarifa,wanategemea ajira, utawaona kwenye vyombo vya habari wakifanyamigomo kadha wa kadha wakidai nyongeza ya mishahara, wakifikiriwatatatua tatizo la kipato kidogo!. Changamoto kubwa iliyopo, mfano kwenye jamii zetu, watuhatujaandaliwa kuwa wafanya biashara, wala kuwa wawekezaji, amawajasiriamali. Mfumo wetu wa elimu bado ni ule ule wa Zama zaviwanda ambapo watu wanasoma kwa ajili ya ajira. Watu wengi hivi sasa, wanapohitimu masomo wanabaini kwambakumbe ajira hazipo ndipo wanapoanza kuilalamikia Serikali naviongozi. Tatizo halipo kwenye Serikali wala kwa viongozi pekee tatizolipo kwenye nyakati, nyakati zimebadilika sio tena zile za viwanda,kwahiyo hatutakiwi tena kusoma kwa ajili ya ajira pekee, tunatakiwakusoma kwa ajili ya kuwa wafanya biashara, wajasiriamali nawawekezaji ili kuendana na mabadiliko ya nyakati na ukuaji wateknolojia duniani. 8

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilala Kwenye kitabu hiki utaweza kuona ni kwa namna gani, kama jamiina kama mtu mmoja mmoja ni vigumu sana kuuondoa umaskini, kwasababu mbinu zinazotumika kukabiliana na umaskini haziwezikuushinda umaskni tena!. Pia kwenye kitabu hiki tutaweza kuona ni kwa namna gani mfumowa kupata kipato kwenye Zama za Viwanda umeifanya jamii hii nawatu wake tuwe maskini na watawaliwa wa mataifa tajiri licha yakujaliwa rasilimali nyingi. Tutaangalia pia ni jinsi gani tunaweza kukabiliana na changamotoya umaskini katika maisha yetu tukiwa kwenye Zama hii za Taarifa.Kitabu hiki kinalenga kujenga fikira mpya ambazo nina imanizitasaidia kufikia utajiri kwa kutumia rasilimali tulizonazo.Malengo ya Milenia Umoja wa mataifa wamejiwekea malengo kumi na saba ambayoyanatakiwa yatimizwe ifikapo mwaka 2030. Lengo nambari moja ni,“Kuumaliza umaskini duniani katika mataifa wanachama.” Lengonambari mbili ni, “Kumaliza tatizo la njaa duniani ifikapo mwaka2030.” Kwa hiyo, juhudi zetu zote katika jamii yetu ni kuhakikishatunaumaliza umaskini ifikapo mwaka 2030 kwa sababu sisi niwanachama wa Umoja wa Mataifa.KUMBUKA; Vita vyetu dhidi ya umaskini haviishii mwaka2030, ni vita vya maisha yetu yote, sisi na watoto wetu navizazi vyetu vyote vijavyo. Kwa maoni yangu, jukumu la kuumaliza umaskini siyo jukumu lakuiachia Serikali, ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anafanya 9

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilalakila njia ili aweze kuumaliza umaskini na njaa yeye mwenyewe nafamilia yake. Hivyo basi;- a) Tunawezaje kuumaliza umaskini na njaa? b) Mbinu zipi tutumie ili tuweze kuwa matajiri? c) Nani mwenye jukumu la kuhakikisha tunakuwa matajiri? d) Tanzania tunazo rasilimali nyingi kuliko nchi nyingi duniani, lakini pamoja na kuwa na rasilimali zote hizo hali ya maisha ya watu wengi ni duni, kwanini? e) Kwenye vyombo vya habari utawasikia watu mbalimbali wakiitangaza Tanzania ni nchi nzuri yenye rasilimali nyingi, kwa hiyo wawekezaji waje wawekeze. Unafahamu matokeo ya kuwakaribisha wawekezaji kutoka nje ya nchi kuja kuwekeza nchini? Kwanini kama nchi tunatakiwa kutengeneza wawekezaji wazawa na wafanya biashara wakubwa wazawa na wajasiriamali wakubwa wazawa ili tuweze kuwa matajiri haraka?Hayo ni baadhi ya maswali ambayo kwenye kitabu hiki yamepewaufafanuzi na majibu yake. Umaskini wetu upo katika fikira. Fikira tulizonazo tumepewa naelimu yetu tunayosoma, ambayo inatufundisha tusome tukimalizachuo tutatufe ajira badala ya tukimaliza chuo tufungue makampuni yabiashara; tuwe wafanya biashara na wawekezaji, tuchangie kiasikikubwa kwenye pato la taifa, taifa liwe tajiri na sisi tuwe matajiri natutumie rasilimali zetu kuwa matajiri. Utaratibu tulionao hivi sasaimekuwa kinyume chake, tunasoma tukimaliza chuo tunatafuta watuwenye pesa wanatuajiri tunakuwa watumishi wao. Maandiko 10

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilalamatakatifu nayo yanagusia jambo hili yanaposema; “Na wageniwatasimama na kulisha makundi yenu, na watu wa kabilanyingine watakuwa wakulima wenu, na watunzaji wamizabibu yenu” (Isaya 61:5). Unaweza kuona ni nani anayetawala; Msomi au mwenye pesa?Ndiyo maana kitabu hiki kinakupatia mwanga mpya wa wewekujiandaa kuwa tajiri na kama umeshaanza kuwa tajiri au tayari nitajiri, basi utapata kuelewa kwa undani uhusiano wa mambo na jinsi yakujipanga na kuwafundisha watu wengine ili nao wawe matajiri.Je, Kitabu Hiki Kitakufanya Uwe Tajiri? Ni vigumu kubashiri ikiwa kitabu hiki kitakufanya uwe tajiri. Kuwatajiri ni jambo la kuchagua na kuamua. Watu wengi hujidanganyamioyoni mwao kwamba wanataka kuwa matajiri kumbe hawajachaguautajiri. Matendo yao huwashuhudia kama wamechagua utajiri au la,kwa sababu utajiri una kanuni zake na misingi yake ili uweze kuupata.Mtu yeyote anayeitii misingi na kanuni za kupata utajiri anayo nafasikubwa ya kuwa tajiri. Kitabu hiki kitakupatia baadhi ya misingi nakanuni za kupata utajiri, ni jukumu lako kuamua kuifuata, naukiifuata unayo nafasi ya kutajirika mapema lakini ukiipuziaukaendelea kuishi maisha yako ya siku zote, unayo nafasi kubwa yakutokuwa tajiri. Kitu kigumu kabisa ni kuchagua kuwa tajiri. Watu wengi mioyoyao imefifia, haina tena kiu ya kuupata utajiri kwa sababu kwenye dinizao wamefundishwa kwamba; huwezi kuwatumikia mabwana wawili,pia wamefundishwa kwamba kupenda pesa kunasababisha kuikanaImani, wakisahau jinsi Ibrahimu, Ayubu na Sulemani walivyokuwa 11

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilalamatajiri wala hawakujitenga na Mungu wao. Mtaani nako wanasikiamaneno mbalimbali kama vile, matajiri huupata utajiri wao kwa nguvuza giza, matajiri ni wachoyo, matajiri huwanyanyasa maskini, tenahawawajali hata ndugu zao na maneno mengine mengi. Kwa mantiki hiyo kitabu hiki kitakufanya uwe tajiri tu endapoutashinda maneno yoyote yanayo uchukia utajiri na kusema vyovyotewatakavyousema utajiri nimeshaamua kuwa tajiri, ukiwa na msimamowa namna hiyo kitabu hiki kitakusaidia mahali pa kuanzia ili kuupatautajiri. Ni wale tu walio na malengo na shauku ya kuwa matajiri ndiowanaoweza kuwa matajiri.Mgawanyo wa Kitabu Hiki Kitabu hiki kina sehemu tatu zenye jumla ya Sura kumi na sita.Sehemu ya kwanza ya kitabu imejikita kujibu swali la “Kwanini KunaUmaskini?” Hapa utajifunza kwa upana suala hilo, utaelewa kwaninibaadhi ya nchi tulizopata uhuru wakati mmoja zimetuacha mbali sanakiuchumi wakati rasilimali tunazizidi na sasa ndizo zinatuuzia bidhaazao. Swali la Kwanini kuna umaskini linalenga kukuonyesha mfumowa kimaskini tunaoutumia katika nchi yetu na kama hatutabadilikamimi na wewe, hatuwezi kuwa matajiri kamwe. Sehemu ya pili ya kitabu hiki inakupatia uhuru wa kuchagua kuwatajiri. Sehemu hii inaitwa “Chagua Kuwa Tajiri”. Kwenye sehemu hiitutaangalia baadhi ya mambo ya kifikira ambayo tunatakiwa tuanzekuyajenga kwenye akili zetu ili yatusaidie kuwa matajiri. Lakini piatutaweza kuona baadhi ya hatua stahiki za kuchukua mapema kwa ajiliya kuupata utajiri. 12

Mwanzo wa Kuwa Tajiri Vincent Mabula Jilala Sehemu ya tatu ya kitabu hiki inalenga kuonyesha “Mahali utajiriunakopatikana.” Kuna maeneo kadha wa kadha ambayo utajirihupatikana, lakini pia kwenye sehemu hii, utapata ushauri kwa ajili yakuwaandaa watoto wetu jinsi ya kuwa matajiri. Kama wewe ni mzazi,basi sehemu ya tatu itakufaa zaidi kwa ajili ya kuwapa ushauri watotowako. Kuna mambo mengi utajifunza kwenye kitabu hiki, hakika itakuwaMwanzo wako wa kuwa tajiri ukitekeleza kwa vitendo ushauri uliomo.Karibu tuendelee. 13

Sehemu Ya Kwanza KWANINI KUNA UMASKINI? Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, siku chache baada yaTanganyika kupata uhuru alisema,“Tunao maadui watatu tunaopaswakuwapiga na kuwashinda, maadui hao ni Ujinga, Maradhi naUmaskini.” Akiwa raisi wa Tanganyika na baadaye Tanzania alijitahidisana kupambana na maadui hao. Leo ninapoandika kitabu hiki miaka zaidi ya 50 tangu MwalimuNyerere ataje maadui hao, hali bado sio nzuri ingawaje vitatunaendelea kuvipiga kuwapiga maadui hao. Adui umaskini katikajamii yetu bado anazo nguvu nyingi, watu wengi zaidi amewadhuru.Sehemu hii ya kwanza ya kitabu hiki inalenga kuonyesha ni kwanamna gani Adui Umaskini anajiimarisha katika jamii yetu. Nimatumaini yangu kwamba baada ya kuisoma sehemu hii utapataufahamu mkubwa zaidi wa namna umaskini unatengenezwa katikajamii yetu. 14

Kupata kitabu hiki tafadhari Wasiliana nasi kwa simu namba; +255785661447 (Whatsapp) +255753068371Gharama ya kitabu ni Tsh. 10,000/= (Elfu kumi) tu,unaweza kutuma kwa M-PESA au AIRTEL MONEY kwa nambahizo. Ukituma pesa yako, tuma na email yako pamoja namajina yako ili tuweze kukutumia kwa email. Ukitaka hardcopywasiliana nasi ili tujue utaipaje. Gharama ya Hardcopy na Softcopyinafanana. Kumbuka kutuma pesa kwa namba hizi; +255753068371…………M-Pesa: MABULA JINYEU +255785661447……………Airtel Money: MABULA JILALAAuWasiliana nasi kwa;Barua pepe: [email protected]: www.fikiaupeo.comAnuani: Fikia Upeo Company Limited S.L.P 369, Bariadi-Simiyu, Tanzania.Pata Nakala yako sasa. 15

367


Like this book? You can publish your book online for free in a few minutes!
Create your own flipbook