Important Announcement
PubHTML5 Scheduled Server Maintenance on (GMT) Sunday, June 26th, 2:00 am - 8:00 am.
PubHTML5 site will be inoperative during the times indicated!

Home Explore Fema 63 HIV (Without Crop Mark)_compressed (1)

Fema 63 HIV (Without Crop Mark)_compressed (1)

Published by castory, 2023-08-21 07:10:52

Description: Fema 63 HIV (Without Crop Mark)_compressed (1)

Search

Read the Text Version

["Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 51 10\/10\/2022 11:39 UKWELI WA MAMBO Hao wageni haooo! NA FEMA TEAM Wahenga wanasema Majuto ni Mjukuu! Ushawahi kufanya kitu ika\ufb01kia wakati ukajisemea \u201cnajuta kwanini nilifanya hayo?\u201d Tulilijadili hili hivi karibuni. Tulipiga story sana na wanaFema wa Itipingi Sekondari, vijana waliochangamka kinoma noma, wakaibua mambo kibao ambayo yanawakuta vijana katika karne hii ya mambo mengi. (Au ni vijana wanayakuta?) Mwisho wa siku tukaibuka na hii simulizi ambayo imeijenga Cartoon story ya toleo hili. Itipingi hoyeee! Hebu vuta pumzi kidogo, pata \ufb02ashback ya visa na mikasa iliyomkuta Tafakari kali binti mrembo Mwaisa, mtoto wa Mzee Mtopelo. Unadhani baada ya zile taarifa kuwa\ufb01kia wazazi mambo yaliendaje? Ni ujumbe gani ulioupata kwenye Cartoon Story hii? Na je, ujumbe huo umekuletea hisia gani? Kama ungekuwa Kuna mtu hapo kasema ilaumiwe simu\u2026 Hapo kwanza n\u2019cheke! Basi sawa, Mwaisa, ungefanya nini tofauti, na kwa wakati upi? simu imekuwa simu na mambo yake, lakini je, kama Mwaisa asingekubali kufanya aliyoyafanya ili mradi tu apate simu, simu ingehusikaje? Na yeye hali Na je, ushawahi kujiuliza kuwa hawa watu wazima, wanaume yake ingekuwaje? Kuna yaliyo ndani ya uwezo wetu, na kuna yaliyo nje ya kwa wanawake wanatafuta nini kwa vijana wadogo na uwezo wetu. Kuna yanayotakiwa sasa hivi na kuna yanayoweza kusubiri. Ni wanafunzi? uamuzi, ni suala la kuweka vipaumbele sahihi katika mpangilio unaojenga. Unadhani Mwaisa alichukua muda kutafakari kama njia ya kupata simu Je, nia yao imebeba nini chenye faida kwako; simu tu? aliyoshauriwa na Nyamizi ilikuwa sahihi? Ona sasa! Chipsi kuku tu? Uko tayari kuvuruga ndoto zako kwa simu tu kisa likes na comments? Au utamu wa chipsi kuku Mimba na wageni juu! unaosherehesha mdomo na kulaghai kichwa? Wageni wasio na hodi! Kina nani hao? Si wengine ni Virusi vya Unadhani Nyamizi ni ra\ufb01ki bora? Ra\ufb01ki bora ana sifa zipi? UKIMWI (VVU). Kweli kabisa! Mwaisa alipata maambukizi ya VVU Kwanini kuna mara\ufb01ki wanakubalika nyumbani, lakini pamoja na mimba. Sote tunafahamu kwamba ugonjwa huu una wengine wanapigwa marufuku? madhara katika jamii na kwa mtu mmoja mmoja. Ingawa zipo dawa za kufubaza makali ya VVU, bado hakuna dawa ya kuviondoa Upo msemo mwingine usemao, nionyeshe mara\ufb01ki zako mwilini. Tufahamu pia kwamba maambukizi ya VVU yanaepukika. niijue tabia yako! Ra\ufb01ki mwema kamwe hatokuruhusu Kivipi? Acha ngono zembe, au acha kabisa ngono, usichangie na mtu ujiingize kwenye tabia hatarishi. Ra\ufb01ki mwema atasema no! mwingine vitu vyenye ncha kali, na kuwa makini popote utakapogusa Achana na hizo ishu! Twende tukasome! maji maji au damu ya mwenye maambukizi ya VVU. Soma zaidi kwenye makala ya Cheza Salama ukurasa wa 16. Maswali ya tafakari ni mengi na yanaweza kutengeneza mijadala mingi mizuri kwenye Club na nje ya Club. Hii mada isiishie hapa, ibebe uende nayo kwa mashosti na washkaji, muidadavue haswaaa, mpaka kieleweke. 49OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 52 10\/10\/2022 11:39 FEATURE ARTICLE Yalaaaaaa! Baba kaniambukiza Ukimwi! Ukisikia ngumu kumeza ndo hivi. Yaani, kwanza tufanye kwa mfano, halafu twende mapumziko mafupi, tukirudi tuwekane sawa. Unadhani ni nani mwingine anaweza kuwa alinaswa kwenye huu mtandao? Aliingiaje? 50 OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 53 10\/10\/2022 11:39 Kwa mfano Wewe hapo ni msichana mwenye umri wa miaka 25, au Tumerudi! umri wowote tu. Baba yako mtu mzima wa miaka 55, mtu fulani hivi mtanashati ana heshima zake miongoni mwa Hivi unafanyaje baada ya hapo? Ukiingia nyumbani umkute watu. Kifamilia mko vizuri tu yaani, migongano ni ile ya baba, unamtizamaje? Na yule msaidizi wa kazi? Mama je? kawaida tu kibinadamu. Mama yupo, baba yupo, wewe na Gha\ufb02a unasikia muziki mkubwa boda boda guy anapiga honi, wadogo zako pia mpo, na msaidizi wa nyumbani yupo, unafanyaje? Unawauliza nini? Unawaambia nini? binti wa miaka 20. Tangu mwaka jana uliambiwa na wazazi wako kwamba baba yako ana VVU, na familia inasimamia kuona anameza dawa bila kukosa. Upande wa pili, unaye mpenzi, nyumbani hawamfahamu, lakini mna mipango ya kunyoosha maelezo kila mtu amfahamu, mfunge ndoa siku si nyingi. Yeye anaendesha boda boda. Siku moja unagundua vitu! Vitu vingi kwa wakati mmoja; Kumbe, baba yako na msaidizi wa kazi wana lao jambo, ni wapenzi! Halafu unagundua kumbe jamaa yako boda boda lifti lifti za kwenda sokoni kwa msaidizi wenu wa kazi zimekuwa nyingi. Kumbe hao nao wako kimapenzi. Tobaa! Katikati ya taharuki unaamua kwenda kupima VVU. Lahaulaa! Ni positive. Twende Muhimu: mapumziko mafupi.... Unajua hii kwa mfano sio kwa mfano bali ni kweli kabisa inatokea? Tafakari. Unadhani tangazo gani linawekwa hapa kwenye hii commercial break? 51OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 54 10\/10\/2022 11:39 DONDOO ZA BIBI Amabilis: Bibi: Hodiii. Karibuni Pande Mbili za Shilingi Amabilis: Bibi: Kamwene. Kamwene. 52 OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE Sumaiya, Mary na Amabilis wanaketi chini. Bibi: Haya wanangu, mmekuja na lipi leo? Sumaiya: Ahh bibi shkamoo. Twaja na letu la kawaida bibi. Maongezi mataaamu kwa ajili ya jarida la Fema. Bibi: Ewaaa! Nalipenda sana jarida lenu. Sema bibi siku hizi macho mabovu. Namwambia huyu mjukuu anisomee! Haya, maudhi ya awamu hii ni yapi? Sumaiya: Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI bibi. Bibi: \u201cAhhh\u201d bibi anasema huku akitingisha kichwa. \u201cHilo nalo jambo! Basi sawa, wacha niketi mniulize yenu maswali. Mary anamvutia kiti na bibi anakaa. Sumaiya: Haya bibi, swali kwako ni hili: Ni lipi jukumu la jamii kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI? Bibi: Ahhhh! Mary, Amabilis, na wewe Sumaiya, hilo ni swali gani tena wanangu. Sumaiya: Ndo hilo hilo bibi! Bibi: Basi mimi pia nina swali. Kama nyoka akiingia nyumbani kwako, utamuita mtu kutoka nje aje amtoe? Kama sivyo, nani ni jamii kama siyo sisi wenyewe? Tukiongelea jamii, huwa tunakuwa kama tunajitenga na kujiweka mbali. Jamii ni sisi sote; walioambukizwa na wasioambukizwa Virusi vya UKIMWI. Jamii ni wazazi, ni serikali, watoto, vijana, yaani ni sisi sote. Na sote tunalo jukumu kubwa.","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 55 10\/10\/2022 11:39 Kwa Walioambukizwa afanye vipimo vyote kuhakikisha mtoto na wasioambukizwa anazaliwa salama. Ikiwa mama ameambukizwa VVU afuate ushauri wa wataalamu bila Hizi ni pande mbili za shilingi ile ile, na sisi kama kupindisha, na baba amsaidie kufuata jamii tunapaswa kushughulikia jambo hili bila mwongozo huo ili mtoto wao azaliwe salama. kujali hadhi. Kwa mfano, wale walioambukizwa, Ndani ya nyumba pia kuwe na amani na wadogo kwa wakubwa, wote wanapaswa usalama ili mama mjamzito awe salama. kupewa elimu sahihi. Wanapaswa kuelimishwa Tena, tukumbushane na hili; ni jukumu la kwamba wasijinyayapae kutokana na hali yao. wazazi kuwafundisha watoto wao tangu Na, muhimu zaidi, waelimishwe kwamba hali utotoni juu ya miili yao na namna ya kuitunza. yao ya maambukizi isiwe kisingizio cha wao Wanapaswa kujiheshimu na kujithamini hata kujitoa kwenye majukumu. katika umri wao mdogo. Wazazi wasisubiri Ni wajibu wa wenye maambukizi ya VVU watoto waitafute elimu hii kutoka nje. Huko kujitunza, pia kuzitafuta huduma za afya ili nje ulimwengu utamfundisha mtoto wapate ushauri na dawa. Ni wajibu wao mchanganyiko wa ukweli na uongo. Na umri kutumia dawa hizo kwa usahihi. Kwa kufanya nao unahusika. Mambo mengi huja na umri. hivyo watajiweka katika hali salama. Na Ni muhimu pia kukumbuka kwamba wazazi wanaweza kabisa kufanya shughuli zao kama wote wawili wanapaswa kulea. Njia ya malezi kawaida. Wanalo pia jukumu la kuhakikisha asilia kwamba mama atalea mabinti na baba ni wanazuia maambukizi ya VVU toka kwao kwa watoto wa kiume haina tija tena. Nini kwenda kwa wengine. kitatokea kama mzazi mmoja akifariki? Nani Kwa upande mwingine, wale ambao atamshauri mtoto? hawajaambukizwa waelewe na kukubali kwa Pia, wazazi wamejivua jukumu la kulea, VVU na UKIMWI upo. Waongeze uelewa wao wamezipatia shule. Watoto wa umri mdogo juu ya jambo hili. Wanalo jukumu la wa miaka miwili sasa wanaenda shule. Wazazi kuwapenda bila kuwanyanyapaa wale ambao wanapaswa kufuatilia hatua zao. Wakumbuke wameambukizwa VVU. Wanalo pia jukumu la kwamba ni wajibu wao kuwalea na kuwatunza kuhakikisha walioambukizwa wanatumia watoto wao ili wajenge tabia zenye tija. dawa, kuwakumbusha kutafuta huduma za Ikitokea kwa bahati mbaya kwamba wazazi afya haraka na kuwahimiza kuzuia maambukizi wamemwambukiza mtoto, ni jukumu lao yasiende kwa wengine. kama wazazi kumpeleka mtoto kwenye kituo cha afya afanye vipimo. Wamsaidie apate dawa Kwa Serikali hitajika. Inawapasa wazazi kutambua umuhimu wa mawasiliano. Waongee na Ni jukumu la Serikali kuratibu, kusimamia na watoto wao na kuhakikisha kuna uwazi katika kutoa huduma za afya, kuhakikisha wananchi mawasiliano yao. wake wanaozihitaji huduma hizo wana\ufb01kiwa. Nashukuru sana kwamba serikali imeleta Sasa, Bibi anaongea sana lakini huduma za afya karibu. Sasa hivi tuna kliniki nitamalizia kwa kujibu swali karibu kabisa, na mara nyingi zina vifaa na lako Sumaiya. Hatuwezi madawa ya kutosha. Kwa hiyo, kama uliza kazi ya jamii ni tulivyosema, jukumu sasa liko kwa jamii. nini \u2013 kwa sababu sisi Wanapaswa kufuatilia na kufanya yawapasayo. sote ni jamii na hii kazi yote ni kazi ya jamii Kwa Wazazi 53OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE Hapa wazazi msikilize vizuri. Jukumu lenu ni kwenye malezi, na malezi haya huanza tangu mtoto yuko tumboni. Pindi tu mwanamke apatapo ujauzito, wazazi hawa wanapaswa kufahamu kwamba sasa wao ni wazazi, hata kabla mtoto hajazaliwa. Sasa ni jukumu lao kumlinda mtoto wao. Hii inamaanisha mama","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 56 10\/10\/2022 11:39 MPENDWA ANTI Iwapo una tatizo lolote kuhusu Mpendwa Anti, swali langu Mpendwa Anti shikamoo. Mimi mabadiliko ya mwili wako, afya ni kwamba, mtu mwenye maambukizi naitwa Amina kutoka Tabora. Je, yako, matatizo ya kifamilia,shule ya Virusi vya UKIMWI (VVU) anao busu linaweza kuambukiza na hata mara\ufb01ki tafadhalituma uwezo wa kuwaambukiza watu wangapi? UKIMWI? kwa Mpendwa Anti: Naitwa Silanga Makoye kutoka Bariadi FEMINA HIP Simiyu. Endapo katika midomo hakuna vidonda S.L.P. 2065, Dar es Salaam Endapo mtu mwenye maambukizi ya VVU wala michubuko (kumbuka si michubuko e-mail: [email protected] atafanya ngono bila kutumia kinga, ana yote huonekana kwa macho wala kuleta SMS: 0753003001 uwezo wa kumwambukiza kila afanyaye maumivu) busu linaweza kuwa salama. naye ngono. Hivyo kama ana wapenzi Mate yanapotoka kwenye tezi zake huwa Mpendwa Anti, pole na kazi. wengi ana uwezo wa kuwaambukiza wote hayana VVU. Naomba kuuliza, je, unaweza kadri atakavyokuwa nao. kumtambuaje mtu mwenye Lakini, ni wangapi hutoa damu kila UKIMWI? Ili kupunguza kasi ya maambukizi ni wanapopiga mswaki japo hawana vema kuwa na mpenzi mmoja na maumivu yoyote? Kuna kujing\u2019ata na Habari? Hauwezi kumtambua kutumia kondomu, hata kama mtu kupata michubuko mtu mwenye maambukizi ya anatumia dawa za kupunguza makali ya kwenye \ufb01zi. Kwa VVU kwa kumtazama kwa VVU (ARV) kwa usahihi ili kupunguza kuwa hatuna macho, na pia usimwamini tu kasi ya VVU kuzaliana mwilini. uhakika wa yule asemaye \u201cmimi sina usalama wa maambukizi ya VVU\u201d, anaweza Kumbuka hata kama mtu midomo yetu kuwa anadanganya. Njia pekee ameambukizwa VVU, wenyewe na ya ya kujua endapo mtu huyo ana asipojilinda anawe- wenzi wetu, maambukizi au la ni kwenda za kupata aina tuepuke busu pamoja kituo cha upimaji na nyingi zaidi za la ndani ushauri nasaha na kupata VVU, na (denda) na majibu ya vipimo pamoja. kujiweka watu ambao kwenye hatari hatujapima zaidi. Jilinde nao na usiambukizwe. kujua hali Pima ujue hali yao yako, na endapo maambukizi umeambukizwa, ya VVU jilinde pia, na ikoje. uwalinde wengine. Shikamoo Anti. Je, vidonge vya kuzuia mimba hutumika baada au kabla ya tendo la ndoa? Habari? Mtu anayetumia vidonge vya uzazi wa mpango anatakiwa kumeza kidonge kimoja kila siku, tena ni vema kuchagua kama ni asubuhi au jioni na kuendelea kwa muda huo huo kila siku. Mtumiaji atameza kidonge kila siku hata kama hafanyi ngono siku hiyo. Vidonge huanza kumlinda mtumiaji siku ya saba tangu aanze kuvitumia, katika kipindi hicho ni vema kusubiri au kutumia njia nyingine kama kodomu ili kuzuia ujauzito. Kumbuka, vidonge havizuii maambukizi ya VVU wala magonjwa mengine ya ngono. 54 OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 57 10\/10\/2022 11:39 ANTI COS ANAJIBU MASWALI YENU Shikamo Anti. Mimi ni msichana Habari Anti, asante kwa kazi ya kuielimisha jamii. Anti, mwenye umri wa miaka kumi na naomba kuuliza, kwa kawaida mvulana anatakiwa kufanya nne, na kwetu wananilazimisha mapenzi akiwa na umri gani? kuolewa lakini mimi sitaki Kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla hujaamua kufanya kuolewa. Maisha yangu ni ya ngono. Kabla haujaamua kufanya ngono jiulize, je uko tayari? kuchapwa sana, kwa mfano kama Kuna ulazima wa kufanya ngono? Faida ni zipi na hasara ni wakinikuta nimesimama na zipi? Je, unaweza kukabiliana na changamoto zitokanazo na mvulana ninachapwa sana. ngono (mimba, magonjwa, hisia)? Je, mwenzi wako yuko Naomba ushauli wako Anti. tayari? Umri wako na mpenzi wako ni sahihi kisheria? Una Pole sana kwa yote unayoyapitia. malengo yapi kimaisha, na je, ngono au mahusiano yako? Kulingana na sheria za Tanzania, Kumbuka, kwa walio shuleni, sheria za shule haziruhusu kuwa mtoto wa umri wako hawezi na mahusiano ya kingono kipindi chote unasoma. Kusubiri ni kuolewa kwa ndoa halali. Fahamu salama zaidi ili kuzuia magonjwa na mimba. kuwa ndoa kamwe haiwezi kufung- wa bila ridhaa ya watu wawili yaani Mpendwa Anti, kuna madhara yoyote Mpendwa Anti, mimi ni kijana mwanamke na mwanaume, hivyo kwa mvulana kuwa na mwanamke mwenye umri wa miaka 22. Nina hata kama wanakulazimisha, bila mkubwa kiumri? mpenzi wangu nampenda sana na wewe kusema \u201cndio\u201d, kamwe hiyo Watu walio katika mahusiano ya sitegemei kumuacha lakini haiwezi kuwa ndoa. Una haki ya kimapenzi wanapotofautiana sana umri nisipokuwepo anakuwa na kukataa kuolewa bila kujali una umri kuna mambo ambayo yanaweza kuleta wengine. Tuna miaka minne gani. shida. Kuwa na umri uliokaribianahusaidia kwenye mahusiano lakini nikijaribu Ndoa za utotoni huleta mimba za kuwa na usawa katika kushirikiana kwao kusema tuachane anadai utotoni ambazo zinaweza kusababisha (partnership) kwenye mahusiano haya na ananipenda sana. Je, nifanyeje ili hata kifo kwa mtoto. Pia, athari kupunguza uwezekano wa mmoja abadilike tabia? by Rehema. zingine za ndoa za utotoni ni pamoja kumkandamiza mwenzie. Endapo mmoja Mpendwa Rehema, ili mtu abadilike na maumivu ya kihisia na kimwili ana umri mkubwa sana kulinganisha na tabia, ni yeye binafsi inabidi afanye kwa anayelazimishwa kuolewa, mwenzieni rahisi huyu mwenye umri maamuzi hayo. Kama mpenzi wako kumweka mtoto kwenye hatari ya mkubwa kumburuza na kumtumia asipoamua kuacha tabia hiyo, ni kupata maambukizi ya magonjwa mdogo kwa kadri yeye anavyotaka. ngumu wewe kumbadilisha. Mwenzi mbalimbali na kukatisha ndoto za wako anapokuwa na mahusiano na masomo na maisha kwa mtoto. Kuhusu maambukizi ya VVU na wapenzi wengi, anakuweka kwenye Tembelea o\ufb01si ya Ustawi wa Jamii magonjwa mengine ya ngono, mdogo hatari ya kupata maambukizi ya kwenye kata yako, au halmashauri anaweza kushindwa kuwa na Virusi vya UKIMWI na magonjwa ya wilaya, kisha onana na A\ufb01sa maamuzi ya kujilinda kwani hana sauti mengine ya ngono. Ustawi wa Jamii. Pia kwenye uhusiano huu, hasa ukizingatia Ni muhimu kujiuliza wewe unahitaji unaweza kupiga mwenye umri mkubwa zaidi anaweza uhusiano wa aina gani, uhusiano huu simu au kutuma pia kuwa ameshakuwa na mahusiano unakupa amani na unalinda afya ujumbe kwenda mengi mengine awali na kumweka huyu yako ya mwili na akili? Anayekupenda namba 116 kwa mdogo kwenye hatari kwa dhati atakuheshimu, atakusikiliza, msaada zaidi. ya kupata magonjwa. atajali hisia zako. Kumbuka kujali afya yako katika mahusiano. 55","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 58 10\/10\/2022 11:39 MUULIZE ANKO PESA! Una maswali lukuki kichwani mwako? Unataka An kuwa mjasiriamali lakini hujui pakuanzia? Unaogopa ku kujitosa katika biashara? Biashara inakwenda na mrama? Una senti mbili-tatu lakini hujui uwekeze ku wapi? Una maswali kedekede kuhusu mambo ya ku mshiko? USITAABIKE! Uliza ujibiwe na ANKO PESA, sija mtaalam wetu wa masuala ya ujasiriamali! un vin uk ful shu un wa ku Shkamoo Anko Pesa, mimi naitwa Neema Manento Habari Anko Pesa. Mimi naitwa Neema na nina umri wa miaka kumi na kutoka Kilimanjaro. Ningependa kujua ni vitu gani vya sita. Ninasoma kidato cha pili. Anko Pesa nina kipaji cha uchoraji na msingi vinavyotakiwa pindi unapotaka kuanzisha ningependa sana niwe mchoraji, ila wazazi wangu wanataka nimalize biashara ya bustani za mboga mboga? masomo yangu. Hata hivyo mimi ningependa niishie kidato cha pili ili Marahaba Neema. Vitu vya msingi unapotaka kuanzisha wanipeleke kwenye shule ya uchoraji. Unanishaurije? bustani ya mbogamboga kwa ajili ya biashara cha kwanza Salama Neema. Hongera sana kwa kutambua kipaji chako cha uchoraji na ni soko lako; unataka kuwauzia watu gani? Wako wapi? kuwa na moyo wa kutaka kukiendeleza. Kuendeleza kipaji ni jambo zuri sana Itabidi ujue uhitaji wa mboga ili uzalishe mbogamboga na ukiwa hodari katika uchoraji unaweza kukusaidia sana katika kujiajiri. ambazo soko linahitaji. Kwa kuzalisha namaanisha Hata hivyo kujiendeleza kwako siyo lazima uachane na masomo yako katika unalima mwenyewe ingawa inawezekana pia ukawa kidato cha pili. Hapo ni mbali sana na bado umri wako ni mdogo sana unazitoa mahali kwa jumla na kuzisambaza reja reja kwa kuachana na shule. Nakushauri endelea na masomo huku ukiwa unatumia wateja wako. Kama utalima mwenyewe hapo itabidi uwe muda wako wa ziada kuchora. Baadae unaweza kusoma zaidi katika chuo nauhakika wa ardhi\/shamba, cha Sanaa Bagamoyo au vyuo vingine. pembejeo, maji na upatikanaji wa mbegu Hongera sana kwa kazi nzuri Anko Pesa. Swali na mbolea. Ukiwa langu ni je, kama nataka kusomea mambo ya tayari anza kidogo lakini endelevu. utangazaji wa TV au redio, naanzaje? Ahsante kwa hongera. Kusomea mambo ya 56 OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE utangazaji wa TV au redio unapaswa kwanza kujiendeleza kielimu. Baada ya kumaliza masomo ya sekondari unapaswa kwenda kusoma katika vyuo vya Uandishi wa Habari. Unaweza kuanza kufuatilia vyuo hivi na kujua masomo na kiwango cha ufaulu kinachohitajika ili kujiunga. Hata hivyo kuwa mwenye shauku ya kujifunza kutoka kwa watangazaji nguli redioni na kwenye TV ili ujue na wewe namna ya kujiweka katika haiba na kuzungumza, huku ukizingatia umuhimu wa kutengeneza upekee.","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 59 10\/10\/2022 11:39 ! ANKO CHRIS ANAJIBU MASWALI YENU Anko Pesa shkamoo. Mimi naitwa John Mahola kutoka Mwanza. Swali langu ni je, nawezaje kuwekeza katika kipindi hichi ambapo nipo masomoni? Nina lengo la kuongeza kipato ili nijiandae na maisha yangu ya baadaye.Marahaba John. Sa\ufb01 sana kwa kuwa na mtazamo huo mzuri wa kuwekeza wakati uko masomoni. Kuna walau namna mbili za kuwekeza. Namna ya kwanza ni kuwekeza kipato au fedha, na hii inategemea na upatikanaji wa fedha wakati unasoma. Kwa sababu sijafahamu unasoma wapi au kwa kiwango gani ni ngumu kukupa njia ya moja kwa moja. Lakini kama una uwezo wa kupata kiasi fulani unaweza ukawa unawekeza kwenye vipande kama UTT ambavyo vinaongezeka thamani, au ukanunua hisa katika soko la hisa. Baada ya miaka kadhaa unaweza ukapata mtaji mkubwa kiasi kuweza kukuinua. Namna ya pili ni kuwekeza kwa kujifunza stadi au ujuzi fulani kwa muda wako wa ziada kila wakati. Hili litakupa kutangulia sana kivitendo ili wakati unamaliza shule uwe umeshapiga hatua sana na kurahisisha kujiajiri au kuajiriwa. Kwa mfano, unaweza kuwa unafanya kazi kwa kujitolea au malipo kidogo kwenye duka siku za mapumziko au likizo, kiasi kwamba wakati unamaliza masomo unakuwa na elimu ya vitendo katika biashara ya duka. Hii itakusaidia sana kuweza kujiajiri iwapo utaamua kufungua duka lako mwenyewe. Anko Pesa mimi naitwa Alod na ninasoma kidato Mpendwa Anko Pesa, shikamoo cha pili. Nilikuwa najishughulisha na kuuza pipi za na pole kwa shughuli ya BG Bom lakini wauzaji wamekuwa wengi hapa uelimishaji jamii. Anko, je, shule. Je, nifanyeje Anko? mchongo wa ufugaji wa nyoka Habari Alod! Naamini kuuza kwako BG Bom hapo unalipa zaidi au una risk zaidi?? shuleni hakuvunji sheria za shule wala kukurudisha Jac\u00f3 Nyerere kutoka Rusumo nyuma katika masuala yako ya kielimu. Kama niko Ngara Kagera. sahihi basi tuanze hivi; elewa kwamba biashara Marahaba na ahsante nashukuru. nzuri huzalisha ushindani. Hiyo ni sehemu ya Mchongo wa ufugaji wa nyoka maisha. Cha kufanya hapo ni kwamba utafute siyo rahisi kama inavyojadiliwa mahali ambapo utapata hizo BG Bom kwa bei juu juu kwenye mitandao ya rahisi kuliko washindani wako ili uweze kuweka kijamii. Ni shughuli yenye hatari promosheni ya punguzo la bei ambalo washindani ambayo ni bora waachiwe wakiiga wata\ufb01lisi mtaji wao. Kwa mfano punguzo wataalamu wenye elimu stahiki kwa kila mtu atakayenunua mbili. Hii itakufanya katika viumbe wa aina hiyo. uwe zaidi ya washindani. Pia ongeza aina nyingine ya bidhaa. Anko Pesa naitwa Baraka kutoka Mwanza. Nina mpango wa kuanzisha biashara ya dagaa kutoka Mwanza kupeleka Dar es Salaam. Je, ungenishauri nianzie wapi?Habari yako Baraka. Biashara ya dagaa kutoka Mwanza kupeleka Dar es Salaam ni nzuri. Lakini kama ilivyo kwa biashara nzuri ni wengi wanaoifanya na hivyo ushindani ni mwingi. Njia ambayo ningependekeza uanze nayo ni kutafuta mtu ambaye yupo kwenye biashara tayari ambaye anaweza kukuongoza. Unaweza kushirikiana naye kidogo ukazunguka naye na kujifunza biashara hii wakati unafanya pamoja naye. Hapo utajua changamoto zilizopo na namna ya kuzishinda. Baada ya kufanya nae kwa muda kidogo unaweza kuachana naye na kujitegemea mwenyewe kama utaona ina manufaa zaidi. 57OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 60 10\/10\/2022 11:39 SEMA NA FEMA Mambo vipiii? Ni wakati mwingine tena tunakutana kwenye ukurasa wetu pendwa na kufahamu yaliyojiri katika mitandao yetu mawasiliano\u2026. Hii ni sehemu tunapojimwayamwaya na kupaza sauti zetu. Zamu hii wadau wa mitandaoni wamewafunika wenzao wa sanduku la barua na email, ila, usikonde, unaweza kutuma huko pia; barua pepe [email protected] na S.L.P 2065 Dar. Kwenye mitandao ya kijamii; Facebook, Instagram na twitter kote huko piga hodi @feminahip. Wadau wakatuma Kwenye maswali sasa! message kibao za Big Up! Watu wakatiririka! Baraka Makwale Sanga Swali: Mwezi unapoanza huwa unajiwekea malengo ya mwezi? Big up sana Femina Hip kwa kuendelea kuelimisha violethlusapa wanafunzi na jamii kwa ujumla! Mnafanya kazi nzuri sana. Pia majarida ya Fema yaendelee Ukiwa na ndoto na nia ya kutimiza ndoto zako, kuwa\ufb01kia watu kwa sababu yanasaidia unafanya kile kinachoendana na ndoto zako bila kutuhabarisha, kutuelimisha, na kutuburudisha pia. kujali kama watu watanicheka au watanisema vibaya. Pia, haijalishi kama watanifurahia au Hekima Poul Kyando watanichukia. Ni lazima utatimiza ndoto zako na kuziishi. Mimi natoka Kyela, Mbeya. Big up sana Femina Hip kwa kazi yenu nzito ya kuelimisha jamii! Nimewapenda Asante sana Violeth Lusapa umetisha sana \u2026\u2026. bure MUNGU awape afya njema na maisha marefu! afe kipa afe beki, ndoto zetu lazima zitatimia. Nawakubali sana! Habari za Kyela Baraka? Asante sana kwa message! Ally Stambuly Sadick Naweka malengo yangu kila mwezi unapoanza na pia yale niliyojipangia mwezi uliopita ambayo sikuyakamilisha nayapa kipaumbele mwezi mpya unapoanza. Hongera sana Ally! Endelea hivo hivo! Swali: Ni kitu gani kinachowasukuma vijana kujihusisha kimapenzi na watu waliowazidi umri? Erickgeorgekalinga Uzidchi uummirin, dlaiokinchi,aynazpooknikaumbwenagkinineakcahmowaavfialenkyautvoirjaidnhaikkaunjiiangmizwaeknaztiikaanamyeaehnudsaiannaonnaayew. atu waliowa- 58 Shout out kwako Erick!","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 61 10\/10\/2022 11:39 Swali: Ni kitu gani kinachowasukuma Swali: Heri ya siku ya wakulima! vijana kujihusisha kimapenzi na Tunathamini mchango wenu katika watu waliowazidi umri? kukuza uchumi wa Taifa. Erickgeorgekalinga Amani Kataraiya Uchumi ndio chanzo kikubwa kinachowafanya Bila shaka kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi vijana kujiingiza katika mahusiano na watu wa taifa letu. Tunatakiwa kutambua, kuthamini waliowazidi umri, lakini, yapo na mengine kama na kuheshimu uwepo wa wakulima. vile kutoridhika na mwenzi anayeendana naye. Asante sana Amani, tunathamini mchango wako. Shout out kwako Erick! Swali: Ukisikia biashara ya mtandaoni Bodaboda, walezi, makondakta wa unaelewa nini? daladala, wauza chipsi. Listi ni ndefu sana, endeleza tuliowasahau. Renatus Sangi Ben Ndaki Ni kuuza na kununua bidhaa kwa njia ya mtandao, hivyo mtandao unabaki kuwa Jukumu ni lake, aendelee kubaki hapo juu platform kuu ya matangazo ya bidhaa husika na akishuka tu kahatarisha maisha yake. Tatizo pia mfumo wa malipo unabaki kuwa ni kwa njia ya lipo kwa hao watoto na si hao wawindaji, mtandao. wasichana wawezeshwe kwanza na kujengewa uwezo, hao waliopo hapo chini watawaogopa Hakika unaielewa vizuri biashara hii! wenyewe. Naamini wanaFema wamekusikia Ben. Swali: Vipi wewe mdau, ni miiko gani wazee walikwambia enzi izo? WmaiUtdnsaainaukdkokasuuoeitlyweoetkataaluatFeyuanascaikeabkicjoaahCotmeikikaikitaou,uoepamoncaoehdg!weaetlaiykelnelaoytmnkuoeeu.oxnwsTtthuaiteninyamaaamweks.aioikp,\u2026oen\u2026nnaodPs!iaitNtsauiatknbawaaicleaahnaauayaake!.!u!a Emmanuel Msemakweli 59OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE Wahenga ni watu koro\ufb01 sana nyie. Wakati tunahangaika kuwinda ndege kwa manati, tuliaminishwa kuwa wawindaji wanapaswa kula vichwa vya ndege tu ili wapate shabaha zaidi wakiwa mawindoni. Nakwambia tulikula vichwa sana. Tcha Kilwaboy Sisi kwetu tuliambiwa ukinyoa nywele unazikusanya zote kisha unaenda kuzitumbukiza chooni, hatukuwa tunajua sababu ni nini, labda nayo sababu ilikuwa ni kuweka mazingira sa\ufb01. Emmanuel na Tcha, mmetisha sana!","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 62 10\/10\/2022 11:39 WAKALI Vigelegele jamaniiiiiii\u2026\u2026\u2026. Wacha tuwapigie vigelegele huku tukilisakata rhumba na tshirts zao ishirini walizojishindia. Washindi wetu wa chalenji no 32 si wengine bali ni KILOLI SECONDARY Fema Club all the way from Mwaaaanzaaaa the Rock City! Sasa basi, tujikumbushe Chalenji No. 32 ilikuwa inawaelekeza nini. Chalenji yetu ilikwenda kwa jina la \u201cshowcase your talents\u201d. Chalenji hii iliwataka wanaFema Club kujidai na vipaji vyao walivyojaaliwa, tena vipaji ambavyo vinaweza kutumika katika kuelimisha wengine na ku\ufb01kisha ujumbe. KILOLI SEKONDARI hawakulaza damu, wakachakarika na wakaupiga mzigo. Wakatumia vipaji vya uchoraji, uandishi na utungaji hadithi kutu\ufb01kishia ujumbe aina tatu ulioshiba. Hawa wajanja wametumia uchoraji wa katuni kutuelimisha kuhusu namna ambavyo binti anaweza kuepukana na ukeketaji. Hawakuishia hapo, walitumia kipaji chao cha uandishi kutuandikia insha nzuri inayotuelimisha juu ya dalili za UVIKO 19. Baada ya hapo wakatupiga na hadithi moja matata inayoenda kwa jina la \u201cAsiyeskia la mguu huvunjika guu\u201d. Hawa majamaa ni hatareeee!!!!! Vigelele tena jamaniiii\u2026. CHALENJI NO 34Nichalenjiitakayotuelimishanakutupakamtokokidogo.Mmefurahi,ausio?Kamawanaklabumnapaswakumualikamtoa &ushauri nasaha shuleni kwenu ajekuwapa elimu juu ya masuala ya Virusi vya UKIMWI, au kama vipi mnaweza mkaenda nyinyi kwenye kituo cha ushauri nasaha mkapata elimu, yaani tumaanisha hivi, inabidi mpate elimu kutoka kwa mshauri nasaha. Mkishapata elimu, picha ndo linaanza. Mkishamaliza, kama wanaklabu mtumie njia yoyote ile, afe kipa afe beki, muu\ufb01kishe ujumbe huo kwa vijana wenzenu waliopo nje ya shule. Tunajua hii ni kazi ndogo sana kwenu, Deadline yetu ni au sio? Twende kazi. Februari 28, 2023 Hivi mnakumbuka? na washindi watatamba kwenye tolea la 65. Mshindi atapata tshirt ishiriniiiiii na washindi wengine watano watajipatiaa khanga yetu ya Femina KILA LA KHERI! Hip nzuuriiiiii iwapambie shughuli zao. Sisi tumemaliza. Kazi kwenu! Inatumwaje? Kama kawaida, tazama ukurasa wetu wa mawasiliano. Chaguo ni lenu, mnaweza kutuma kwa kupitia email yetu au mkatumia anuani ya posta, vyovyote mtakavyoamua, sisi mzigo utatu\ufb01kia. Hapo mnatuma ushahidi kutuonesha na kutuhakikishia kwamba kweli chalenji mliifanya na mliifanyaje. Full stop. KWA MAWASILIANO TAZAMA UKURASA 60 OCTOBER - DECEMBER: FEMA MAGAZINE WA SABA WA TOLEO HILI.","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 63 10\/10\/2022 11:41 COMPETE & WIN Hebu tusimame, turuke ruke, nondo tulizozipata kuanzia mwanzo wa jarida hadi hapa zijipange kwanza maana najua mmepata elimu na mmeburudika vya kutosha, au sio? Sasa basi, ule muda wetu pendwa wa shindano umewadia na kama kawaida tusivyo na baya, washindi wetu ishirini kama kawa watajibebea tshirt kali za Fema, kila mmoja na ya kwake. Basi tuwajue washindi wa toleo lililopita kabla hatujaendelea. Dee Jaaaay\u2026\u2026. niletee washindi. Washindi ni: 11. Leonard Rwetaka Kachuho - Mwabaluhi Sec School 12. Barnabas Ignas Ndunguru - Ngwilizi Sec School 1. Jackline Pius - Dr Nchimbi Sec School 13. Mabella Daniel Mabella - Iganzo Sec School 2. Mariam M. Maganga - Mtekente Sec School 14. Rahel Alphonce - Mwananchi Sec School 3. Johari Abdalah Muhidini - Kili Sec School 15. Balibanga Mzaliwa Balibanga - Kasimbu Sec School 4. Iptisam Ibrahim Rajabu - Kasimbu Sec School 16. Amadi Amudi Amri - Kazima sec School 5. Virgiana Massay Marsel - Kilimamoja Sec School 17. David G.Mashaka - Buchambi Sec School 6. Zakaria S. Bankwabu - Ngudu Sec School 18. Eligy Edward Kimario - Mramba Sec School 7. Zaituni Issa Hamisi - Isseke Sec School 19. Abbas Ally Mporogo - Chief Ntingiya Sec School 8. Abubakari O Hamis - Munzeze Sec School 20. Khadija Mwalimu Sharifu - Bungu Sec School 9. Rehema Mohamed - Chief Ntinginya Sec School 10.Kelvin Keneth - Magufuli Sec School Shindano letu ndani ya Fema 63 linahusu Magonjwa ya ngono. Je wajua? Gemu lipo hivi\u2026 Tafuta majina yote ya magonjwa ya ngono ambayo yameorodheshwa na yapo ndani ya jedwali, zungushia duara neno zima Kati ya mwaka 2000 na 2015, duniani wastani ili lionekane, fanya hivyo kwenye majina yote ya magonjwa yaliyopo, na wa umri wa kuishi uliongozeka kwa miaka mitano. utakuwa umeweza kushiriki kwenye gemu letu. Niwaibie siri\u2026 Mtu atakayeweza kuandika kwa maelezo mafupi ya Kiswahili, maana ya magonjwa matatu aliyoyaona kwenye jedwali, kisha atume pamoja na jedwali hilo, atajiongezea nafasi ya ushindiiiiiii!!!!! Zingatia * Mtu yeyote anaweza kushiriki shindano hili. * Kwenye kichwa cha habari andika Compete and Win ukiwa unatuma. * Maswali na majibu yanatakiwa kuandikwa kwenye karatasi nyingine na sio kwenye ukurasa huu. * Unaweza kutuma majibu kwa njia ya posta au barua pepe. * Hakikisha unaweka jina lako, la shule kama upo shule, anuani na namba ya simu kama unayo ili kurahisisha mawasiliano. * Ni shindano la mtu mmoja mmoja, sio la Club. Je wajua? Kucheka kuna faida kwenye moyo wa binadamu na kunaweza kuongeza mzunguko wa damu kwa asilimia 20.","Fema 63 HIV (Without Crop Mark).pdf 64 10\/10\/2022 11:41 A Light in the Dark"]


Like this book? You can publish your book online for free in a few minutes!
Create your own flipbook