Important Announcement
PubHTML5 Scheduled Server Maintenance on (GMT) Sunday, June 26th, 2:00 am - 8:00 am.
PubHTML5 site will be inoperative during the times indicated!

Home Explore Mwongozo wa kuweka malengo

Mwongozo wa kuweka malengo

Published by mabulajilala, 2016-02-01 04:18:44

Description: Mwongozo wa kuweka malengo

Search

Read the Text Version

MWONGOZO WA KUWEKA MALENGOYAKO NA FAMILIA YAKO ILI UFIKIEMAFANIKIO MAKUBWA NA UTAJIRI Ndani Utapakua;-PROGRAMU YA PROGRAMU YA PROGRAMU YA KUPANGA VITABU VIWILI MUHIMUKUKOKOTOA MAPATO KULINGANISHA MAPATO BAJETI YAKO KWAKONA MATUMIZI YAKO NA MATUMIZI YAKOMabula Jilala Novemba 2015 WWW.MORNINGTANZANIA.COM

MAELEZO KUHUSU SEMINA HIIMtandao wa MORNING TANZANIA kupitia blog yake ya Morning Tanzania(www.morningtanzania.com) iliendesha Semina kwa njia ya mtandaomnamo tarehe 02 hadi 07 Novemba 2015 yenye kichwa cha habari,“MWONGOZO WA KUWEKA MALENGO YAKO NA FAMILIA YAKO ILIUFIKIE MAFANIKIO MAKUBWA NA UTAJIRI”Kwenye semina hiyo tulijifunza mambo mengi hasa kwa mtu yule anayetakakufikia mafanikio makubwa. Tulijifunza hatua kwa hatua namna ya kuwekamalengo yako kuanzia ukiwa kijana hadi ukiwa mzee. Hatukujifunza kwamaneno matupu tu bali kwa vitendo namna ya kuandika malengo hayo.Kutokana na umuhimu wa semina hii hasa kwa mtu anayetaka mafanikiomakubwa, nimeona ni vema kila mtu anayejiunga na mtandao huu waMORNING TANZANIA lazima aipate semina hii. Na sasa iko mikononimwako.Baadhi Ya Mambo Muhimu Utakayojifunza Ndani ya Semina Hii:A. Utajifunza namna ya kuweka malengo yako kiasi kwamba usielemewe majukumu kutoka kwa ndugu na watu wengine wa karibu yako. Hapa utajifunza namna ya kutumia ndugu zako kama kichocheo chako kwenye kufikia mafanikio makubwa.B. Utajifunza kutofautisha bajeti na malengo. Watu wengi wanaelemewa majukumu ya familia kwa sababu wanaandaa bajeti zao wakifikiri ndiyo malengo yao. Wewe utajifunza namna ya kutofautisha vitu hivi na hivyo kutoathiriwa na majukumu mengine.C. Ikiwa umeolewa au umeoa, hapa ndipo mahali pake. Utajifunza namna ya kuweka malengo ya familia yako, namna ya kulea watoto, lini uzae watoto na mzae watoto wangapi, lini muende kusoma au kuongeza elimu, utajifunza namna ya kuandaa ratiba ya kumtumikia Mungu kwenye familia yenu pia utajifunza namna ya kuweka malengo ya 2

kusaidia watu wengine na idadi ya watu mtakaowasaidia. Yote hayo utayapata ndani ya semina hii.D. Utajifunza namna ya kuweka malengo ya kuwa tajiri, kwahiyo utajifunza namna ya kuchagua miradi itakayokufikisha kwenye utajiri. Zaidi ya hayo utajifunza kukadiria mapato ya kila mradi.E. Semina imeigawanywa katika nyakati tatu, kuna WAKATI WA UJANA, WAKATI WA UTU UZIMA na WAKATI WA UZEE, kwenye kila wakati utajifunza namna ya kuweka malengo yako yanayoendana na wakati husika.F. Utajifunza namna ya kuweka malengo ya kuwaandaa watoto wako ili waje kuwa matajiri lakini pia ili waje kuwa waendelezaji wazuri wa miradi na mifumo yako ya kiuchumi, kijamii na kiroho utakayokuwa umeianzisha.G. Ndani ya semina utajifunza namna ya kuweka malengo ya ujenzi wa nyumba yako ya kuishi. Unaweza kujenga nyumba na usiishi humo, semina hii inakupa mbinu ya kuweka malengo juu ya afya yako.Hayo ni baadhi tu kati ya mambo mengi utakayojifunza ndani ya semina hii.Unachotakiwa kufanya wewe ni kutumia semina hii kuandaa malengo yakoau unaweza ku-copy na ku-paste halafu yakawa ndio malengo yakoKama Hiyo Haitoshi Kuna Zawadi Kubwa Mbili Utapataa) Utapata kupakua program tatu kwa ajili ya KUDHIBITI MZUNGUKO WAKO WA PESA. Programu hizi ni ‘automatic’ na zipo kwenye program ya excel. Unachotakiwa ni kuzipakua na kuzifungua kwenye kompyuta yako yenye excel halafu unaanza kuzitumia, ni rahisi sana na zitakupigia mahesabu yote ya pesa zako au hata za kampuni yako. Zitakupa uwiano wa mapato na matumizi yako na zitakusaidia kujua kama unapata faida au hasara ya uendeshaji wa miradi yako. 3

b) Zawadi ya pili utapakua vitabu viwili vya kujiendeleza kwenye kuweka malengo yako na kukupa elimu ya fedha. Karibu uendelee na Semina. 4

UtanguliziNachukua nafasi hii kwa heshima na taadhima kukukaribisha katikasemina hii inayoendeshwa na mtandao wa MORNING TANZANIA. Kwa kifupisana naomba nikueleze MORNING TANZANIA ni nini;- Ni mtandaounaojikita katika kutoa ushauri na maarifa kwa makundi mbalimbali yajamii kama vile wajasiriamali, wafanyabiashara, viongozi, na watu wotewenye nia na kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa katika maisha yao.Tunatoa ushauri na maarifa hayo kupitia makala, semina kama hii, vitabumbalimbali na baadaye tutaendelea kupanua wigo ili tuwafikie watu wengizaidi.Blogu ya MORNING TANZANIA imefikisha mwaka mmoja sasa tanguianzishwe, kwani ilianzisha mwezi Disemba 2014 na mmiliki wake ni mimininayekuletea semina hii kwa majina naitwa Mabula Jilala, kwa sasa nimwajiriwa katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Seksheni yaMiundombinu. Siko peke yangu tu bali nashirikiana na watu mbalimbalindani na nje ya nchi kwa pamoja tumekuwa tukishirikiana kukuandaliaushauri na mafundisho mbalimbali ili kuhakikisha kwa pamoja tunafikiamafanikio yetu makubwa. Kwa maelezo zaidi tembeleawww.morningtanzania.com. Karibu tuendelee na semina yetu;- 5

KIPENGELE CHA KWANZA MALENGO NA BAJETIMALENGO NI NINI?Malengo ni mpangilio wa kazi na majukumu ya kufanya katika maisha yamtu yenye lengo la kumfikisha mtu huyo kwenye hatua fulani nzuri iliyokombele yake.Malengo ni shabaha ya namna mtu ataitimiliza kazi yake hapa duniani. Nimapitio (njia na mbinu) anazopitia mtu hadi akipate kile kikubwaanachokitamani. Kwahiyo ndani ya malengo kuna mikakati kadhaa ambayomtu huiweka ikiwa ni pamoja na kujipa uhuru au kujinyima uhuru wakufanya baadhi ya mambo ili akipate kile kikubwa anachokitamani.Malengo yanaweza kuwa ya mtu mmoja au ya kikundi cha watu au yafamilia au ya Taifa zima. Kila mtu na kila familia inatakiwa kuweka malengoyake ili iweze kufikia kule inakotamani ifike kwenye mafanikio makubwa.Kwanini Tunatakiwa Kuweka MalengoMaisha ni safari ndefu yenye vituo vingi na changamoto nyingi. Tunahitajikuweka malengo ili tufike tunakotaka kufika vinginevyo hatutafika kwasababu mbalimbali ikiwemo kukata tamaa na mambo mengine. Tunazosababu kadhaa zinazotufanya tuweke malengo yetu. Sababu hizo ni kamaifuatavyo;-a) Tujidhibiti katika mienendo yetu, au tujizuie kufanya baadhi ya mambo yanayoweza kututoa kwenye mstari wa matamanio yetu.b) Akili hushindwa kufikiri ipasavyo ikiwa haijaelekezwa kufikiri kwenye kitu fulani, kama kuna malengo yalioandaliwa vizuri, akili hupata nguvu zaidi za kufikiri juu ya namna ya kuyatimiza malengo hayo na hivyo kila siku kupata wazo jipya la kuyafikia malengo yako.c) Malengo ni taswira ya mafanikio yako unayoiona wakati ukiwa mwanzoni mwa safari ya mafanikio yako. Kama utakuwa unajiona mwenyewe jinsi 6

utakavyokuwa miaka kadhaa inayokuja, itakutia hamasa ya kukazana zaidi ili uyafikie mafanikio hayo.d) Sisi binadamu si wa kudumu, leo upo na kesho haupo. Tunahitaji kuweka malengo ya familia zetu ili hata kama wewe hutakuwepo anayebaki asihangaike cha kufanya. Atapitia kwenye malengo uliyoyaacha na akiwa jasiri anaweza kufika kwenye mafanikio uliyoyatazamia.e) Kuweka malengo binafsi na kuweka malengo ya familia yako, unawapa somo zuri watoto wako nao watajifunza kupitia wewe na wao wataweka malengo yao yatakayo wasaidia katika maisha yao.f) Malengo ni kipimo kinachotumika kukujulisha umepiga hatua kiasi gani kwenye mafanikio yako. Kama hujaweka malengo yaliyodhahiri sio rahisi kujua kama kuna matumaini ya kufikia ndoto zako. Kwa lugha nyingine usipokuwa na malengo dhahiri (na yaliyoandikwa) unaweza ukachelewa kufikia mafanikio yako au unaweza usifike kabisa kwa sababu huna mahali pa kujiangalia. Ndio maana nasisitiza ni muhimu malengo yako uyaandike.Hasara Za Kutokuweka Malengo Kwenye FamiliaKama familia haina malengo yaliyoandikwa na yanayojulikana kwa kilammoja kuna baadhi/yote ya mambo yafuatayo yanaweza kujitokezakwenye familia hiyo;a) Mtu mmoja kuhenyeka sana na wengine wasijue cha kufanya.b) Mgawanyiko wa kimawazo unaolemaza juhudi za kufikia mafanikio makubwa ya familia.c) Watu wengine kusubiri kuletewa mahitaji yao wala wao wasijishughulishe kujitafutia wao wenyewe.d) Lawama nyingi zisizokoma kwenye familia zinazosababishwa na kushindwa kukidhi kwa mahitaji ya familia.e) Watoto kukosa maadili kwa sababu wazazi hawajui cha kufanya au hawakujiandaa nini cha kuwafundisha watoto wao ili wakue katika nidhamu na maadili mema. 7

f) Usaliti wa kimahusiano unaosababishwa na kudharauliana kwenye familia.g) Kama sio kutalakiana kwa wanandoa basi kuishi maisha ya bora liende na kupoteza radha nzuri ya ndoa.Ili kusawazisha mambo hayo ni vizuri kila familia ikajiwekea malengo yakeambapo kila mtu kwenye familia atakuwa na wajibu wake wa kufanyakatika muda uliopangwa. Malengo ya familia haitakiwi ajue mtu mmoja tuni vizuri yaandikwe na kila mmoja ajue wajibu wake wa kila siku. Malengoya familia ni kama Msahafu ambapo kila siku mtu husoma ili asisahau.Tofauti Kati Ya Malengo na Bajeti.Tumekwisha kuona maana ya neno Malengo, naomba tuangalie tofautiiliyopo kati yake na neno Bajeti.BAJETI NI NINI?Ni mchanganuo wa jinsi ya ukusanyaji wa mapato na namna ya kuyatumiamapato hayo katika muda maalumu; inaweza kuwa ni mwezi mmoja,mwaka mmoja au muda wowote utakaopangwa.Bajeti husimama baada ya Malengo. Kwa mfano, ukitaka kununua gari,unaanza kuweka malengo ya kununua gari, ukishaweka malengo ndipounaanza kupanga bajeti ya kununua gari. Na ukinunua gari bila malengolitakuwa linashinda ndani limepakiwa. Bajeti hugusa mambo ya fedha namalengo hugusa maisha ya mtu kwenye kila kipengele. Mfano, bajetihaigusi swala la mahusiano yako wewe na watu wengine, huwezi kuwekabajeti ya kumpenda mtu lakini unaweza kuweka malengo ya kumpendamtu. Bajeti haigusi huduma za utumishi wako, haigusi aina ya familiaunayoitaka lakini inagusa swala la fedha kwenye nyanja hizo.Kwahiyo familia au mtu binafsi anapokuwa na bajeti tu bila malengoakifikiri kuwa ndiyo malengo anakuwa amekupungukiwa na mambo mengiyasiyoguswa na pesa moja kwa moja. Mambo hayo ndiyo ya muhimu 8

kuwekewa malengo kwa kila mtu ili aweze kufikia mafanikio makubwa.Kama unataka kufanikiwa lazima ujiwekee malengo kwenye kila eneo lamaisha yako vinginevyo ukiishi kwa kutegemea bajeti tu ukifikiri kuwaumemaliza kupanga malengo, bado utakwama.Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu tofauti ya malengo na bajeti angaliajedwali hii hapa chini.S/ Malengo BajetiNo.1 Hujumuisha kila kitu katika Inahusika na mapato na matumizi maisha ya mtu. ya mali alizonazo mtu.2 Uongozi, mahusiano, malezi, Pesa na mali nyingine. elimu, ndoa, pesa, miradi, imani, n.k3 Ndani yake kuna sheria, taratibu Malengo hutangulia, kisha bajeti na mikakati thabiti. Huwezi hufuata. Unaanza kuweka malengo kufikia malengo bila kutii ya kununua gari ndipo bajeti mambo hayo. inafuata.4 Unatakiwa kuandaa malengo ya Kutegemea hii tu kama mwongozo maisha yako kwa kugusa kila wa maisha yako kufanikiwa kwako kipengele cha maisha yako ni vigumu sana.5 Ni “covergent” yaani huakisi Ni “covergent” yaani huakisi kuelekea sehemu moja yenye kuelekea sehemu moja yenye mafanikio makubwa kabisa mafanikio makubwa kabisa6 Bila malengo utashindwa Bila bajeti utafilisika kujizuia na kupotea njia.7. Malengo usipoyaandika Mali bila daftari huisha bila habari. utayasahauKutokana na ufafanuzi huo, tunapata kufahamu kwamba unatakiwakujiwekea malengo yako na ya familia yako. Usiishie kuweka bajeti tuukifikiri kuwa ndiyo malengo yako, bajeti hufuata baada ya malengo. Kama 9

unafamilia ni lazima kila mtu kwenye familia hasa baba na mama na wakatimwingine watoto (tena ni muhimu) myafahamu malengo ya familia yenu.Kama mtu mmoja asipoyafahamu malengo ya familia yenu mtapoteananjiani.Malengo yanataja muda wa kukamilisha kile unachokitaka lakini piamalengo yanataja kiasi ya kile unachokitaka. Malengo lazima yaandikwe.MAMBO YA KUZINGATIAUnatakiwa kujiwekea malengo yako na ya familia yako. Usiishie kuwekabajeti tu ukifikiri kuwa ndiyo malengo yako. Bajeti hufuata baada yamalengo. Kama unafamilia ni lazima kila mtu kwenye familia hasa baba namama na wakati mwingine watoto (tena ni muhimu) myafahamu malengo yafamilia yenu. Kama mtu mmoja asipoyafahamu malengo ya familia yenumtapoteana njiani.Malengo yanataja muda wa kukamilisha kile unachokitaka lakini piamalengo yanataja kiasi ya kile unachokitaka. Malengo lazima yaandikwe. 10

KIPENGELE CHA PILI MAHALI PA KUANZIA UNAPOWEKA MALENGO YAKOHapa tunaanza hatua kwa hatua kuandika malengo yenyewe.Nimekuandalia mfano wa malengo ya familia, mpangilio wake na vipengelevya kuweka ndani yake na namna unavyoweza kushirikiana na mwenziwako kuandika malengo hayo. Huo muundo niliouandaa unaweza ukau-copy na ku-paste yakawa ndio malengo yako au ya familia yako au unawezakuandaa malengo yako baada ya kupata mwanga wa jinsi ya kufanya. Sasa,tunaanza kuandika malengo ya familia. Lugha iliyotumika hapa ni yawanandoa wakishirikiana kuandika malengo ya familia yao. Kama wewehujaoa/kuolewa badala ya uwingi utatumia umoja, mfano kwenye nenolinaloanza na “tuta….” Wewe utasema “nita…”. Karibu tuandike malengoyako;-TUNAKOTOKAUkoo wangu -(Baba wa Familia)Mimi ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya mzee Pesa Nyingi,yenye watoto nane. Mchoro ufuatao unaonyesha ukoo wangu. (Utaandaamchoro wa familia-Family Tree)Ukoo wangu (Mama wa Familia)Mimi ni mtoto wa tatu kuzaliwa katika familia ya mzee Milioni Zangu, yenyewatoto nane. Mchoro ufuatao unaonyesha ukoo wangu (Utaandaa mchorowa familia-Family Tree).Tunaunganisha Koo MbiliNdoa yetu inaunganisha koo mbili na kuwa ndugu wa damu kupitia sisi.Kwahiyo hatuishii kuoana sisi wawili tu bali tunafanya koo zetu kuwandugu. Tunawajibu mkubwa wa kuwajibika kwa sababu kuanzia siku yandoa yetu tumekuwa jamaa moja kubwa. 11

Sababu Za Kuoana KwetuWana ndoa wanapoingia kwenye ndoa halafu hawajui sababu iliyowafanyawaoane au wanaoana kwa mazoea tu, huwa ni rahisi sana kuchokana kwasababu kiu iliyowafanya waoane ikiisha, wote wanabaki tupu mioyonimwao. Kwahiyo ili ndoa yetu idumu katika furaha yake ni vizuri tutambuesababu za kuingia kwenye ndoa, kiasi kwamba kila mtu kwenye ndoahatamchoka mwenzake kwa sababu atakuwa anamhitaji mwenzake ilikuedeleza malengo yetu.Mimi (Jina la Baba) na mke wangu (Jina la Mama) tunazo sababu sitazinazotufanya tuoane. Sababu hizi ni kama ifuatavyo;-a) Tumtumikie Mungu nasi atutumie kwa makusudi na mapenzi yake.b) Tuwe na familia yetu na watoto wetu.c) Tuwasaidie watu wengine wakiwemo ndugu zetu na watu wengine katika mahitaji yao ukiwepo ukombozi wao wa kiroho na kiakili na kiuchumi.d) Tuwe wawili ili tuimarishane katika utumishi wetu hapa duniani kwa njia ya Upendo.e) Ili tufurahi, tujionee utukufu wa Mungu popote duniani na hatimaye tufike huko mbinguni.f) Tufurahie utajiri wa Mungu nasi tuwe warithi wa utajiri wake.NB: Mpenzi msomaji wa MORNING TANZANIA, kwanini unatakiwa kuwekayote hayo, mambo ya ndugu, na ukoo? tena kuweka sababu za kuoana zotehizo za nini?.Jibu: Kumbuka mnaweka malengo ya familia na familia ni baba, mama, nawatoto (panapo majaliwa), kuweka ukoo wenu ni kuweka kumbukumbukwa ajili ya watoto wenu na nyinyi wenyewe. Lakini pia kwa ajili yakuwasaidia ndugu pale inapobidi. Pia kuweka sababu za kuoana ni ili kilamtu kwenye familia baba na mama amhitaji mwenzake kwa ukaribu kabisasio kwa kazi moja tu. Ni lazima muweke sababu za kuoana kwenuitawasaidia. 12

Tahadhari; Hili halitawezekana kwenye ndoa za MITEGO au ndoa zaNDOANO.VISION NA MISSION YETUIli kuzitimiza sababu hizo zote za kuoana kwetu hatuna budi kuwa namission na vision yetu kama ifuatavyo;-Vision yetu (Maono): Tuwe familia ya mfano wa kuigwa kwa vizazi vingikatika Utumishi Wa Mungu, Kusaidia Watu, Upendo Na Utajiri.Mission yetu (Dira): Tujikabidhi mikononi mwa Mungu, tutumie Hekimayake na Maarifa yake na Ufahamu wake siku zote.NB:Vision: Kwa maelezo rahisi ni sehemu ya mbali ya mafanikio unayoionaukiwa mwanzoni mwa safari yako ya mafanikio na ambayo unataka ufikehuko.Mission: Ni njia au mbinu utakazopitia ili kuifikia ile sehemu ya juu (vision) ya mafanikio.NYAKATI TUTAKAZO PITIANyakati hizi tumezigawanya katika makundi matatu na kila kundikutakuwa na majukumu ya kufanya. Nyakati hizi ni kama ifuatavyo.Wakati wa ujanaWakati wa utu uzimaWakati wa uzee.Kipengele kinachofuata tutangalia kwa undani zaidi jinsi ya kuwekamalengo kwenye nyakati hizi. 13

MAMBO YA KUZINGATIAKila familia ni muhimu kuweka malengo yake. Ni muhimu kuwekaushirikiano kati ya baba na mama wa familia ili familia hiyo iweze kufikiamafanikio makubwa. Ndoa ni furaha ndoa ni upendo, kuweka malengo yafamilia kwa kushiriana kutaongeza upendo na kuaminiana kwenye ndoayenu. Kumbukeni kuweka vision na mission yenu ambayo mtakuwamnaikumbuka siku zote na iwe ndipo mahali pa kujitazamia mnapoendeleambele. Sababu za kuona kwenu ni vizuri mziandike ili ziwakumbushemajukumu yenu na malengo ya familia yenu. Hata kama hujaoa au kuolewaunatakiwa kuweka Vision na Mission yako, usisahau kuweka hiyo. 14

KIPENGELE CHA TATU WAKATI WA UJANA (MIAKA 18-45)Tunaendelea kuchanja mbuga ambapo tunaendelea kuweka malengomengine wakati wa ujana. Tutaangalia namna ya kuweka malengo ya miradina namna ya kukadiria mapato ya kila mradi. Karibu tuendelee.NDOA NA MATOKEO YAKE.Tumefunga ndoa mwezi Novemba mwaka 2015Tutazaa watoto wanne katika familia yetu • Mtoto wa kwanza tutazaa mwaka 2016 • Mtoto wa pili tutazaa mwaka 2019 • Mtoto wa tatu tutazaa 2025 • Mtoto wanne tutazaa mwaka 2028Watoto wetu tutawalea katika misingi ya maadili mema na neno la Mungu.Tutakuwa na program fupi na ndefu za kuwafundisha watoto wetu ambazotutazipanga punde mtoto anapozaliwa. Moja ya mafundisho muhimuambayo watoto wetu tutawafundisha ni pamoja na;- Kumjua Mungu na uweza wake katika maisha yao. Kufahamu wito wao na kuzingatia ndoto zao. Njia nzuri za kupata utajiri ulio halali. Wajifahamu na wawe tayari kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya ukuaji wao, Elimu nzuri wanayotakiwa kuifuata. nkAFYA ZETUTutajitahidi kutunza afya zetu ingawaje ukweli ni kwamba afya yote dunianiyatoka kwa Mungu. Hata hivyo mimi (Jina la Baba) na mke wangu (Jina la 15

Mama) tutajitahidi kutunza afya zetu na afya ya watoto wetu. Katikakutimiza hili tutafanya yafuatayo.• Kutokula aina ya vyakula na vivywaji vyenye kuleta madhara katika afya zetu. Tutaepuka ulevi na uvutaji wa sigara katika familia yetu. Tutakula vyakula vyenye kujenga afya ya mwili.• Tutajitahidi kufanya mazoezi ya viungo ili kuboresha afya zetu. Tutajizoeza kutembea kwa miguu katika mizunguko yetu ili kuboresha afya zetu.• Tutakuwa na muda wa kupumzisha akili zetu kwa kutembelea maeneo yenye vivutio kama vile mbuga za wanyama na maeneo yenye historia nzuri hapa Tanzania na nje ya Tanzania. Tutakuwa tunatembelea maeneo hayo mara mbili kwa mwaka. Lengo lingine la kufanya matembezi haya ni ili kujionea maajabu ya Mungu kwa uumbaji wake na kumshukuru kwa ajili ya hayo.Tutakuwa na ratiba ya kujifunza habari za Mungu katika familia yetu.Ratiba hii tutaipanga na kila mtu kwenye familia ataifahamu.BAJETI YA FAMILIATutaandaa bajeti ya familia yetu mara tu baada ya kufunga ndoa na bajetihiyo inatakiwa ituwezeshe kuishi angalau miezi sita hadi mwaka mmojahata kama hatuzalishi chochote. Kwenye chakula kwa mfano; tunapigiabajeti ya ziada kwa muda wa miezi sita au mwaka mmoja, muda huutunaweza kuuongeza nasio kuupunguza. Vivyo hivyo kwenye mahitajimengine mfano mavazi, tutakuwa na muda maalumu wa kununua mavazi.Jambo la muhimu kwenye bajeti inatakiwa tupigie idadi ya watu mara mbiliya familia yetu. Mfano kama kwenye familia tuko watatu, tunapigia bajeti yawatu sita, bajeti ya aina hii itatusaidia kutobabaika mara tupatapo wageni. 16

KUMTUMIKIA MUNGUTutajitahidi kufahamu kusudi alilotuitia Mungu kwenye maisha yetu. Kwanjia ya maombi na utumishi tutafahamu wito wetu.Tutaandaa utaratibu wa namna ya kuendesha huduma ya Mungu kwenyefamilia yetu. Utaratibu huu tutaupanga mara tunapofunga ndoa na kilamtu ataufahamu kwenye familia yetu.Tutakuwa na ratiba ya kwenda kujifunza zaidi huduma hizi sehemunyingine ndani na nje ya nchi kwa njia ya semina, warsha, makongamanoau hata hija. Tutakuwa na ratiba hiyo angalau mara mbili kwa mwaka.Tutapanga ratiba hiyo kutegemea na upatikanaji wa mafundisho hayo.KUJENGA UCHUMI IMARA NA KUUPATA UTAJIRI.Maandiko yanasema kutajirika ni moja ya tuzo anazopewa mtu paleanapookoka na kujiachilia kwa Mungu. Maandiko yanasema hivi:“Petro akaanza kumwambia tazama sisi tumeacha vyote tukakufuata wewetutapata nini?. Yesu akasema, “amini nawaambieni Hakuna mtu aliyeachanyumba au ndugu wa ume au ndugu wake au mama au baba au watoto aumashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili ila atapewa mara mia sasawakati huu, nyumba na ndugu waume na ndugu wake na mama na watotona mashamba pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wamilele”. Marko 10:28-30“Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo jinsi alivyokuwamasikini kwa ajili yenu ingawa alikuwa tajiri ili kwamba mpate kuwamatajiri kwa umasikini wake”. 2Korintho 8:9“Na yeye ampaye mbegu mwenye kupanda na mkate uwe chakula atawapambegu za kupanda na kuzizidisha naye atayaongeza mazao ya haki yenu;mkitajirishwa katika vitu vyote mpate kuwa na ukarimu wote umpatiaoMungu shukrani kwa kazi yetu”. 2Korintho 9:10-11 17

Itakuwa utakapo isikia sauti ya Bwana Mungu wako kwa bidii kuyatunza na kuyafanya maagizo yote niwaagizayo leo….. na Baraka hizi zote zitakujilia …….utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani….. Kumbukumbu 28:1-14. NB; Kama wewe hutumii biblia, unatumia maandiko mengine, basi jaribu kutafuta aya za maandiko kwenye kitabu kitakatifu unachotumia zinazozungumzia utajiri. Ziainishe aya hizo kisha ziandike kwenye malengo yako ili zibaki zinakukumbusha ahadi ya Mungu kuhusu utajiri. Kutokana na ushuhuda wa maandiko matakatifu tuliyoyaona, sisi katika familia yetu tunatangaza kuwa umasikini marufuku kwenye familia yetu, tunahitaji kuwa matajiri ili tujionee utukufu wa Mungu popote duniani na ili tuwasiadie wahitaji katika dhiki zao za mahitaji ya kimwili na ili Mungu wetu atukuzwe kwa shukrani nyingi kupitia familia yetu. Kwa sababu hiyo tunajiwekea miradi tukakayofanya ili ituwezeshe kufikia malengo hayo kama ifuatavyo;- A. Miradi ya muda mfupi (miaka 1-5) kuanzia mwaka 2015-2020 Hii ni miradi yenye lengo la kutupatia mahitaji ya kila siku ya familia. Lakini pia miradi hii itatumika kutupatia mitaji kwa ajili ya uwekezaji kwenye miradi mikubwa. Tutakuwa na miradi kumi ya muda mfupi ambayo ni kama ifuatavyo;S/N Aina Ya Mradi Muda Wa Jumla ya Jumla yao Kuanza mapato/mwaka mapato/5yrs1 Mshahara kutokana na ajira Unaendelea 4,800,000/= 24,000,000/= yangu2 Mradi wa bodaboda Juni 2016 2,400,000/= 12,000,000/= 25,000,000/=3 Mradi wa ufugaji wa kuku Jan.2016 5,000,000/= 100,000,000/= 6,000,000/=4 Biashara ya mtandao Juni 2016 20,000,000/= 9,600,000/=5 Biashara ya Mazao ya kilimo Disemba 2015 1,200,000/= 12,000,000/= na ufugaji6 Biashara ya Disemba 2015 1,920,000/= Salon/Duka/Stationery7 Biashara ya viwanja na Unaendelea 2,400,000/= Nyumba 18

8 Kilimo Unaendelea 12,000,000/= 60,000,000/=9 Huduma ya hotel Machi 2016 2,400,000/= 12,000,000/= Feb. 201710 Ufugaji wa samaki 20,000,000/= 100,000,000/=JUMLA YA MAPATO YOTE 72,120,000/= 357,492,000/=Ufafanuzi Kuhusu Malengo ya MiradiKutoka kwenye jedwali hapo juu, unapata kufahamu kwamba; Unatakiwaujiwekee malengo ya kuwa na miradi mingi uwezavyo. Hiyo niliyokuwekeani mifano tu, wewe utaweka ya kwako. Hakikisha kila mradi unauandaliaANDIKO LA MRADI (Business Plan) hata kama huna pesa wewe andaaandiko la mradi kwanza ipo siku utapata pesa za kuwekeza kwenye miradihiyo.Unatakiwa kuwa na miradi mingi kadri uwezavyo ili kama utafanikiwakuianzisha yote itakusaidia kupata pesa nyingi kwa muda mfupi. Chukuliakwa mfano kwenye jedwali hapo juu tunaona kwenye miradi hiyo kumiunaweza kupata zaidi ya milioni miatatu ndani ya miaka mitano. Somo lakuwa na miradi mingi kadri uwezavyo nimejifunza kwa Robert Kiyosakikwenye kitabu chake maarufu “Rich Dad Poor Dad”. Kiyosaki kwenye kitabuhicho anatolea mfano wa baba yake tajiri jinsi alivyokuwa na miradi mingina jinsi alivyoweza kutajirika haraka kwa sababu ya kuwa na miradi mingi.Na mimi nakushauri jiwekee malengo ya kuwa na miradi mingi uwezavyoitakusaidia sana kwenye kupata mtaji na utajiri mapema.Faida nyingine ya kuwa na miradi mingi ni kwamba hata kama mradimmoja utagoma au utapata hasara, miradi mingine inafidia pengo hilo.Tofauti na mtu ambaye anamradi mmoja tu, siku mradi huo umekwamandio kila kitu kinakwama. Hiyo ni mbaya sana itakuchelewesha kupatamafanikio makubwa.B. Miradi Ya Muda Wa Kati (Miaka 1-10) Kuanzia Mwaka 2015-2025Hii ni miradi yenye lengo la kutupatia pesa nyingi ambazo zitatumika kwaajili ya uwekezaji kwenye miradi mikubwa. Pia miradi hii itatupatia pesakwa ajili ya maendeleo ya familia ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba 19

kubwa ya kifahari, ununuzi wa usafiri wa familia. Lakini pia miradi hii itatumika kutupatia mitaji kwa ajili ya uwekezaji kwenye miradi mikubwa. Tutakuwa na miradi mitano ya muda wa kati ambayo tumeichambua kutoka kwenye miradi ile kumi ya muda mfupi. NB: Unapoandaa miradi ya muda wa kati na miradi ya muda mrefu, kwa maoni yangu ni vizuri ukaichambua kutoka kwenye miradi ya muda mfupi. Sababu ya kufanya hivyo ni ili kuepuka kuwa na utitiri wa miradi ambayo inaweza kuathiri utendaji wako. Lakini sio mbaya kama unauwezo wa kuongeza miradi ya muda wa kati nje ya ile kumi haukatazwi unaweza kufanya hivo. Jedwali hapa chini linaonyesha mchanganuo wa miradi ya muda wa katiS/N Aina Ya Mradi Muda Wa Jumla ya Jumla yao Kuanza mapato/mwaka mapato/10yrs1 Mradi wa ufugaji wa kuku Jan.2016 25,000,000/= 250,000,000/=2 Biashara ya Mazao ya kilimo Disemba 2015 12,000,000/= 120,000,000/= na ufugaji3 Biashara ya viwanja na Unaendelea 36,000,000/= 360,000,000/= Nyumba4 Huduma ya hotel Machi 2016 24,000,000/= 240,000,000/=5 Ufugaji wa samaki Feb. 2017 10,000,000/= 100,000,000/=JUMLA YA MAPATO YOTE 107 milion 1.07 Bilioni Unapoanza utekelezaji wa miradi yako hiyo, utaanza na miradi ya muda mfupi huku ukiweka msingi mkubwa wa miradi ya muda wa kati na ya muda mrefu. Maana yake utakuwa unaweka bajeti kubwa kwenye miradi hiyo ili ikupatie faida kubwa. C. Miradi Ya Muda Mrefu (Miaka 1-15) Kuanzia Mwaka 2015-2030 Hii ni miradi yenye lengo la kutupatia pesa nyingi . Hapa ndipo kilele cha matamanio yetu kiuchumi. Miradi hii ya muda mrefu maana yake ni uwekezaji mkubwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda. Tutahitaji muda 20

mrefu kukusanya pesa ili tuweze kuanzisha miradi hii. Mapato yake nimakubwa lakini pia ndiyo miradi itakayotuhakikishia utajiri mkubwa.Tutakuwa na miradi mitatu ya muda mrefu ambayo tumeichambua kutokakwenye miradi ile kumi ya muda mfupiJedwali hapa chini linaonyesha mchanganuo wa miradi ya muda wa katiS/N Aina Ya Mradi Muda Wa Jumla ya Jumla yao Kuanza mapato/mwaka mapato/10yrs2 Ujenzi wa viwanda vya January 2025 120 milioni 600 Milioni kusindika mazao ya kilimo January 2025 200milioni 1000 Milioni na ufugaji3 Ujenzi wa nyumba za Machi 2015 150milioni 750 Milioni kupangisha (apartment 450 Milioni 2.35 Bilioni house)4 Hotel kubwa za kitalii na hotel za nyota tanoJUMLA YA MAPATO YOTENB: Kutoka kwenye majedwali hapo juu, usitishwe na kiasi cha pesakilichoandikwa, mimi najaribu kukuonyesha picha ya kile unachowezakukifanya. Kwahiyo wewe utakaa chini ujiwekee malengo yako mwenyewe,ni vizuri kufanya utafiti kidogo wa kile unachotaka kukiwekea malengo.RATIBA YA KWENDA KUSOMAIli kuboresha utendaji kazi wetu kwenye familia yetu, tutahitaji kwendakuongeza elimu. Mwaka 2020 hadi mwaka 2023 mimi (Jina la Baba) na mkewangu (Jina la Mama) tutaenda chuo, kila mtu na chuo chake na masomoyake.KUJENGA NYUMBA YETU.Mwaka kesho 2016 tutanunua kiwanja na kuanza kujenga nyumba yetu.Mwaka 2017 mwishoni tutakuwa tumemaliza kujenga nyumba yetu nakuhamia. Pesa za kujenga nyumba hiyo tutazipata kutoka kwenye miradi yamuda mfupi. 21

KUSAIDIA WATU WENGINE Tunawajibu wa kuwasaidia watu wengine kwenye mahitaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiuchumi, kimwili na kiroho. Tunatakiwa kuwasaidia watu wengine kwa sababu kupitia kusaidia watu wengine sisi tutaimarika kwa namna tunavyowasaidia watu. Pia itaongeza upendo kwenye familia yetu. Lakini pia watu wengi zaidi watabarikiwa kupitia sisi. Kubarikiwa kwa watu wengi ni baraka na faraja kwetu. Kikubwa zaidi kusaidia watu ni njia moja wapo ya kuyatimiza maono yetu (vision).Tutatumia njia tatu kuwasaidia watu wengine ambazo ni;- • Kufundisha habari njema ya Mungu kwa maneno na matendo. • Kufundisha, kushauri na kuelimisha kwa njia ya uandishi wa makala, vitabu, semina, warsha, redio na luninga. • Kuwapa mahitaji watu wenye kuhitaji mahitaji mbalimbali ya kimwili au hata kiroho.Idadi ya watu tutakao wasaidia. • Ndani ya miaka mitano kuanzia mwaka 2015-2020 tutasaidia watu laki moja (100,000) • Ndani ya miaka kumi kuanzia mwaka 2015-2025 tutasaidia watu milioni moja (1,000,000) • Ndani ya miaka ishirini kuanzia mwaka 2015-2035 tutasaidia watu milioni kumi (10,000,000)Ilikufanikisha zoezi hili la kuwasaidia watu wengine linafanikiwa, tutafanyakazi kwa bidii kwenye kazi zetu lakini pia tutatii ratiba zetu tulizojiwekeakwenye kila jambo tunalotaka kulifanya. Tutazingatia na kuzifuata zile njiatatu tulizojiwekea za kuwasaidia watu.NB: Ili kufanikisha hayo yote familia yetu lazima tuijenge kwenye misingi yakumtii Mungu maana yeye ndiye anayetuwezesha kuyafanya yote hayo.Tutatumia mission yetu kama dira yetu ya mafanikio. 22

MAMBO YA KUZINGATIAIkiwa unataka kufikia mafanikio makubwa, jambo la kwanza ni kuwekamalengo makubwa. Unatakiwa uweke malengo ya miradi ya muda mfupi,muda wa kati na muda mrefu. Malengo yako ni lazima yawe dhahiri nayanayotekelezeka. Pia elimu katika familia ni muhimu sana unatakiwaujiwekee malengo ni lini utaenda kuongeza elimu. Njia mojawapo nzuri naya haraka ya kupata mafanikio makubwa ni kusaidia watu. Jiwekeemalengo ya kusaidia watu wengine halafu wewe utabarikiwa sana. Katikakuweka malengo ya kuwa tajiri ainisha miradi mingi uwezavyo kisha, kilamradi andaa andiko la mradi (Business Plan) 23

KIPENGELE CHA NNE WAKATI WA UTU MZIMA (MIAKA 46-60)Tunaendelea kuweka malengo ya wakati wa utu uzima. Tunaweka malengoya kulea familia na kuandaa mafundisho kwa ajili ya watoto wako ili wasiwemaskini. Tunaweka malengo ya namna ya kufikia mafanikio makubwa kwakutumia mfumo (system). Ni somo zuri tafadhali usichoke.Lugha iliyotumika hapa ni ya uwingi (ikiwakilisha wanandoa)wakishirikiana kuandika malengo ya familia yao. Kama wewehujaoa/kuolewa badala ya uwingi utatumia umoja, mfano kwenye nenolinaloanza na “tuta….” Wewe utasema “nita…”. Karibu tuandike malengoyako;-Kipindi hiki ni kipindi ambacho tunatakiwa kuhakikisha malengotuliyojipangia kuyatekeleza kipindi cha ujana yamekamilika. Lakini hatakama kuna baadhi ya malengo hayakukamilika kwenye kipindi cha ujanakutokana na sababu mbalimbali, kipindi hiki kitatumika kuyakamilishahayo. Kwenye kipindi hiki kutakuwa na mambo manne ya kufanya.KULEA FAMILIAHapa tutakuwa makini kuhakikisha familia yetu hasa watoto wetuwanapata malezi sahihi na kwa wakati wake. Tutakazania zaidikuwafundisha watoto wetu elimu ya fedha Kwa sababu elimu hiihaifundishwi shuleni wala vyuoni hapa Tanzania.https://www.dropbox.com/s/fwkgq4uzyuhuy8u/UnfairAdvantageDownload%20Rich%20Dad.pdf?dl=0Kipakue kitabu hapo juu kwa kubofya link na ukisome kupata maelezozaidi kuhusu elimu ya fedha. 24

Tutawafundisha kwa maneno na kwa vitendo lakini pia tutawapelekakwenda kujifunza elimu ya fedha kila sehemu ndani ya nchi na nje ya nchiili waweze kuwa mabingwa katika elimu hii. Tutakuwa makini kwa hili kwasababu hatutaki watoto wetu wawe masikini na hatutaki kizazi chetu kiwemasikini.Tutafungua akaunti ya benki ya kila mtoto ili mahitaji yake yote awezekujiendesha yeye mwenyewe bila kututegemea sisi wazazi. Ili kuhakikishahili linafanikiwa, kila mtoto anapofikisha umri wa miaka sabatutamwanzishia mradi wake ausimamie yeye mwenyewe ambao utakuwaunampatia pesa. Sisi wazazi tutakuwa wasimamizi na washauri wa mradihuo. Kumpa mtoto mradi ausimamie kutamjengea ujasiri wa kutafuta pesazake mwenyewe lakini pia akili yake hatailekeza kwenye kuajiriwa kwanzabali atailekeza kwenye biashara kwanza ambako kunalipa zaidi.KUIMARISHA MIFUMO KWA AJILI YETU NA VIZAZI VIJAVYO.Bila shaka mpaka kufikia umri huu tutakuwa tumeshajenga mifumo mingiya kiuchumi, kiroho na kijamii, tutakachofanya kwenye umri huu nikuiimarisha mifumo hiyo ili iweze kufanya kazi hata bila uwepo wetu.Kwenye miradi yetu tutaimarisha mifumo ili kila mradi uweze kujiendeshahata kama sisi hatupo.KUHAKIKISHA MIRADI YOTE INAFANYA KAZI.Tutatakiwa kuhakikisha miradi yote yaani ya muda mfupi, ya muda wa katina ya muda mrefu inafanya kazi yote. Mwishoni mwa kipindi cha ujana namwanzoni mwa kipindi cha utu uzima, uzalishaji wa huduma utakuwa wajuu na kwa hiyo ni kipindi ambacho tunatakiwa kuingiza pesa nyingi zaidimifukoni mwetu. Jumla ya mapato yetu yote kwa mwaka kutoka kwenyemiradi ya muda mfupi na miradi ya muda wa kati na miradi ya muda mrefuitakuwa fedha za kitanzania bilioni 10 ifikapo mwaka 2040. 25

KUSAIDIA WATU WENGINEKwenye umri huu tutaendelea zaidi kusaidia watu wengine. Tutatumia njiazile zile tatu za awali ambazo ni;-• Kufundisha habari njema ya Mungu kwa maneno na matendo.• Kufundisha, kushauri na kuelimisha kwa njia ya uandishi wa makala, vitabu, semina, warsha, redio na luninga.• Kuwapa mahitaji watu wenye kuhitaji mahitaji mbalimbali ya kimwili au hata kiroho.Kutokana na mifumo tuliyoiandaa, tutasaidia watu wengi zaidi hadi kufikiawatu milioni thelathini (30,000,000) duniani kote ifikapo mwaka 2040.Kadri tunavyosaidia watu wengi zaidi ndivyo watu wengi watabarikiwa kwasababu yetu na sisi tutabarikiwa zaidi kwa sababu yao. Kwahiyo ilitufanikiwe zaidi ni lazima tusaidie watu wengi zaidi.MAMBO YOTE YANAYOHITAJI KUENDELEZWA TOKA KIPINDI CHA UJANATUTAYAENDELEZA.Kuna baadhi ya mambo mfano kuandaa bajeti ya familia, kuandaa ratiba zautumishi au kutoa huduma, ujenzi wa nyumba bora ya kuishi, kushirikisemina, kutembelea maeneo yenye vivutio kwa ajili ya kujifunza na menginemengi, tutayaendeleza kwenye kipindi hiki. Ratiba ya kila jambo tutaipangana kuitekeleza kadri ya makubaliano yetu.MAMBO YA KUZINGATIAWakati wa utu uzima ni wakati wa kutimiza ndoto zako kwa kuhakikishakila malengo uliyojipangia yanakamilika. Hakikisha unaweka malengo iliiwe rahisi kujipima. Hakikisha unawaimarisha watoto kwa kuweka malengoya kuwafundisha kwa vitendo mifumo ya utendaji ya maisha yako.Waandalie masomo ya fedha ili wakue wanafahamu vema namna yakukabiliana na changamoto ya umasikini. 26

KIPENGELE CHA TANO WAKATI WA UZEE (MIAKA 60….)Tufikishapo umri huu tutakuwa na kazi moja kubwa ambayo ni Kushauritu. Tutakuwa washauri kwenye mambo ya uchumi, huduma za kiroho nakijamii. Wakati huu utakuwa ni wakati wa kumshukuru Mungu nakufurahia matunda ya kazi ya mikono yetu. Tutafanya mambo madogomadogo tunapohitajika. 27

KIPENGELE CHA SITA VIKWAZO UTAKAVYOKUMBANA NAVYO WAKATI WA KUTEKELEZA KWA VITENDO MALENGO YAKO NA NAMNA YA KUKABILIANA NAVYO.Ndugu, ni dhahiri kwamba, kujiwekea malengo kwa njia tuliyojifunzakwenye semina hii sio tatizo, tatizo linakuja kwenye kuyatekeleza kwavitendo hayo malengo yako. Naomba tupitie baadhi ya vikwazo hivyo nanamna ya kukabiliana navyo.KUKOSA MTAJI WA KUANZISHIA MIRADIHii ni changamoto ya kwanza utakumbana nayo wakati unapotakakuyatekeleza malengo yako. Mimi nakwambia usihofu kutokana nachangamoto hiyo, kinachotakiwa ni wewe kuweka malengo kwanza, usiachekuweka malengo kwa kisingizio cha kukosa mtaji, kamwe usithubutukufanya hivyo kinachotakiwa weka malengo yako halafu ndipo uanzekutafuta mtaji. Usianze kutafuta mtaji kwanza ndio uweke malengohutafanya vizuri. Kwahiyo anza kuweka malengo yako ndipo uanze kutafutamtaji. Namna Ya Kukabiriana Na Changamoto Hii Changamoto ya kukosa mtaji wa kutekeleza malengo yako, unaweza kuishinda kwa kutumia pesa za watu wengine. Sio lazima uwe na pesa zako, kama unazo ni vizuri zaidi lakini kama huna tumia pesa za watu wengine kupata mtaji. Kuna njia kuu mbili za kutumia pesa za watu wengine ili kupata mtaji. Njia hizi ni kama ifuatavyo;- a) Kukopa kutoka kwa mtu au benki. Kama umeandaa malengo yako vizuri, na andiko la mradi (business plan) umeliandaa vizuri, unaweza kuchukua mkopo kutoka benki au hata kwa mtu mwenye nafasi ya kukukopesha. Kuna benki kama vile CRDB na 28

AKIBA BANK zinafanya vizuri sana kwa wajasiriamali. Hata utaratibu wa urudishaji wa mikopo uko vizuri. Tembelea matawi ya benki hizo kupata maelezo ya kina. b) Kuingia ubia na mwenye mtaji. Njia hii ni nzuri sana kwa ajili ya kukupatia mtaji mkubwa na kwa masharti nafuu. Unachotakiwa ni kutafuta mtu mwenye mawazo kama yako halafu unaingia ubia naye. Kwa mfano kama unataka kuanzisha mradi wa kilimo cha nyanya, tafuta mtu anayelima nyanya kwa sasa, fanya naye mazungumzo mwombe kujiunga naye kwenye kazi hiyo huku ukimwainishia namna mtakavyoweza kupata mapato makubwa akikuruhusu kujiunga naye, kama atakuruhusu kujiunga naye, hakikisha unaboresha kilimo hicho na kufikia kiwango cha juu kabisa. Mpe na mchanganuo wa jinsi atakavyonufaika kwa kujiunga na wewe. Nimekuwa nikiitumia mbinu hii kwa muda wa mwaka mmoja sasa, pia kuna rafiki yangu amekuwa akiitumia mbinu hii imetusaidia sana. Kupitia mbinu hii nimepata mashamba mengi bure na wafanyakazi bure. Nawewe ukiitumia itakusaidia sana. Kama hujaielewa vizuri tafadhali tuwasiliane kupata maelezo zaidi.KUKOSA UDHITIBI WA MZUNGUKO WA PESA ZAKOHii nayo ni changamoto kubwa utakumbana nayo wakati unapotekelezamalengo yako kwa vitendo. Mfano; kama umeazisha miradi usipokuwamakini miradi inaweza kukufilisi na hatimaye unabaki kuwa masikini.Usihofu; baada ya kuliona hilo, nimekuandalia program maalumu ya kupigamahesabu ya pesa inayoingia na ile inayotoka. Kwahiyo kila pesainayoingia utaiweka upande wa ASSET (MAPATO) na kila pesa inayotokautaiweka upande wa LIABILITY (MATUMIZI). Halafu program hiyo itakupigiamahesabu na kukuambia kiasi cha pesa kinachobaki baada ya kutoamatumizi. Hiyo ni programu ya kwanza. 29

Programu ya pili ni kwa ajili ya kukupa totafuti ya mapato yako kati yamwezi /mwaka uliopo na mwezi/mwaka uliopita. Kazi ya program hii nikukujulisha kama unaendelea kuongeza mapato au unapata hasara. Inatoaulinganisho huo kwa njia ya asilimia.Program ya tatu ni kwajili ya kuweka bajeti yako. Kunasehemu ya kuingizamakadirio ya bajeti na kunasehemu ya kuweka pesa halisi uliyoipata.Program hii itakusaidia kuandaa bajeti yako na ya familia nzima. Programzote ni rahisi kuzitumia kwenye kompyuta yako. Programu zote ziko kwenyeexcel.PAKUA PROGRAMU HIZO HAPA.1. Pakua program ya kwanza hapa chini- kukokotoa mapato na matumizi yakohttps://www.dropbox.com/s/dars7dlnm51rt4p/personal_balance_sheet.xls?dl=02. Pakua program ya pili hapa chini- kwa ajili ya kulinganisha mapato yakohttps://www.dropbox.com/s/ypqjxhrb3vxgtu8/balance_sheet_-_comparative.xls?dl=03. Pakua program ya tatu – kwa ajili ya kuandaa bajeti yakohttps://www.dropbox.com/s/cuk42ldojlwj451/Personal_Budget%201.xls?dl=0KITABU CHA KUJIENDELEZAIli kuhakikisha unapata maarifa kamili katika kujiwekea malengo yako,nimekundalia kitabu cha kujiendeleza kwenye kuweka malengo yako.Malengo yako ni nguvu ya kukutoa kwenye hali duni kwenda kwenye halinzuri. Kitabu hiki kinaitwa GOALS (MALENGO) kilichoadikwa na mwandishimashuhuri anaitwa Brian Tracy. Kipakue hapo chini kwa kubofya hiyolink na uanze kukisoma ni kizuri sana ukijumlisha na seminaniliyokuandalia hakika utakuwa umebobea kwenye kuweka malengo yakona utaanza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. 30

https://www.dropbox.com/s/q2t57q2varvkgqd/goals_by_brian_tracy.pdf?dl=0ANAYESHINDA SI YULE ANAYEJUA BALI NI YULE ANAYEFANYA KWAVITENDO.Ikiwa unataka kufikia mafanikio makubwa, anza leo kuweka malengo yakona uyafuate. Lakini kama unataka kubaki hapo ulipo, puuzia hayaninayokuambia utaendelea kubaki jinsi ulivyo. Utapoteza muda mwingisana ukifanya mambo yasiyo na faida kwako. Lakini kama utawekamalengo yako na kuyafuata ni njia nzuri ya kufikia mafanikio yakomakubwa. Tofauti ya mtu aliyefanikiwa na asiyefanikiwa ni moja tu;aliyefanikiwa hufanya kwa vitendo yale aliyojifunza na ambaye hayafanikiwahujifunza na kuyaacha kuyafanyia kazi yake aliyojifunza. Nataka ufanikiwechukua hatua haraka anza leo kuweka malengo yako na uyafuate.MAMBO MENGINE KUTOKA MORNING TANZANIAIkiwa bado hujajiunga na mtandao huu, nachukua fursa hii kukukaribishaujiunge sasa hivi. Kuna faida sita utakazozipata kwa kujiunga na mtandaohuu ambazo ni,-1. Mara unapojiunga na mtandao huu unatumiwa vitabu viwili vizurikimoja kinachokupa elimu ya fedha na biashara, itakayo kusaidiakwenye hatua zako za kuelekea mafanikio makubwa, na kingine kinahusuUpendo na mahusiano.2. Ukijiunga nasi unakuwa umejisajiri moja kwa moja kutumiwa makalazetu punde zinapotoka kwenye email yako.. 31

3. Utakuwa unatumiwa kitabu kimoja kila mwezi kitakachokusaidiakujiendeleza kwenye safari yako ya mafanikio. Pia tutakuwa tunakushaurikitabu kizuri cha kusoma kulingana na mahitaji yako.4. Tutakuwa tunakupa taarifa za semina mbalimbali tutakazo kuwatunaendesha sisi wenyewe hapa hapa Morning Tanzania au washirika wetupopote duniani. Lakini pia utakuwa na fursa ya kutumiwa semina hizomoja kwa moja kwa njia ya email yako.5. Utakuwa unatumiwa ushauri na majibu ya maswali yako utakayokuwaunatuuliza kwenye email yako.6. Utakuwa unajulishwa kuhusu fursa mbalimbali zilizopo Tanzania.JIUNGE SASA KWA KUJAZA JINA NA EMAIL YAKO HAPAhttp://www.morningtanzania.com/p/mcembedsignupbackgroundfff-clearleft_25.htmlMWISHO WA SEMINA HII NAOMBA MAONI YAKO.Nahitaji kusikia kutoka kwako, umeipokeaje semina hii. Tafadhali wasiliananami kupitia simu namba 0785661447 (Whatsapp) au 0753068371. Auniandikie kupitia email [email protected] Utekelezaji Mwema Wa Yale UliyojifunzaTunakuhamasisha Ili Ufikie Mafanikio YakoNi Mimi rafiki yako:-Mabula Jilalawww.facebook.com/MabulaJilalawww.facebook.com/morningtanzania 32


Like this book? You can publish your book online for free in a few minutes!
Create your own flipbook