Important Announcement
PubHTML5 Scheduled Server Maintenance on (GMT) Sunday, June 26th, 2:00 am - 8:00 am.
PubHTML5 site will be inoperative during the times indicated!

Home Explore Stori za Bongo, Toleo la 2, Afya ya Akili (1)

Stori za Bongo, Toleo la 2, Afya ya Akili (1)

Published by euniefoodie, 2020-09-30 18:12:02

Description: Stori za Bongo, Toleo la 2, Afya ya Akili (1)

Search

Read the Text Version

-Salamu za Mhariri -Je Wajua? -Vitu vinavyoweza kuathiri afya yako ya akili -Tabia 20 zinazoweza kusaidia maendeleo ya afya yako ya akili 02T OLLAE O -Vyakula vinavyosaidia afya yako ya akili -Jinsi ya kujali afya yako ya akili unapotumia mitandao ya kijamii -Link za kusoma zaidi kuhusu afya ya akili HITIMISHO

SALAMU ZA Na Eunice Tossy MHARIRI Kuna siku nilikuwa naongea na rafiki @eunietj yangu na akaniambia, 'unajua nikiangalia ni kama kila mtu anapitia jambo fulani kwenye maisha yake, kiasi kwamba najisikia vibaya kuwaambia shida zangu lakini pia naona kuwa kila mtu ana vita yake anayopigana' Na katika miaka yangu 25 chini ya jua, nimegundua kuwa hili ni kweli, kila mtu anapigana vita fulani kwenye maisha, kifamilia, mahusiano, kifedha, kielimu, changamoto ya kikazi nk. Tuna mawazo, ya mambo mbalimbali, tuna msongo wa mawazo, kikawaida hali ya kimwili ikikuzidia utaenda hospitali watu watajali haraka sana, lakini mambo yakikuzidia kiakili hakuna anayejali muda mwingine hata wewe hauoni au haujui kama unahitaji msaada wa haraka kwaajili ya afya yako ya akili. Mimi sio daktari, ila toleo hili nitashea machache kuhusu afya ya akili, tafadhali soma zaidi na ufuatilie kwa undani kuhusu afya ya akili mitandaoni na kwenye vitabu na hospitalini ili ujue jinsi ya kujali afya yako ya akili. Afya yako ya akili ina umuhimu na uzito sawa na afya yako ya mwili, hisia nk. Karibu kusoma toleo la 2.

je wajua? MAGONJWA YA AKILI SONONA / DEPRESSION WASIWASI / TASHWISHI / ANXIETY SKIZOFRENIA / SCHIZOPHRENIA BAIPOLA / BIPOLAR MSONGO BAADA YA JANGA / POST TRAUMATIC STRESS DISORDER (PTSD) MATATIZO YA KULA / EATING DISORDER ULEVI WA MADAWA / DRUG ABUSE UTEGEMEZI WA KILEVI / ALCOHOL ABUSE



Sonona Watu wengi hupitia vipindi vya kuwa na huzuni katika maisha yao, lakini unapokuwa na sonona unajisikia huzuni ya mara kwa mara, inayoambatana na mawazo au fikra hasi na tabia za kutoweza kujumuika na wengine. Hali hii inadumu kwa wiki kadhaa au miezi hata miaka, sio kwa siku chache. Wakati mwingine huambatana na mawazo ya kujiua. Kuwa na sonona sio dalili ya kwamba mtu ni dhaifu Wasiwasi /Tashwishi Wasiwasi ni neno linalotumika kuelezea hisia ya kawaida ambayo watu huipitia wanapokabiliwa na tishio, hatari au wakiwa na msongo. Kila mmoja anaweza kuwa na wasiwasi wakati wowote katika maisha. Ila hali ya wasiwasi inapozidi kupindukia au unapokuwa na hofu pasipo sababu ya msingi na kuathiri utendaji kazi wa kila siku ni dalili ya magonjwa ya wasiwasi (Anxiety Disorders). Utajikuta unakwepa vitu, watu au hali zinazokufanya uwe na wasiwasi. Hata hivyo kukwepa huzifanya dalili kuwa mbaya zaidi

Skizofrenia . ni ugonjwa unaoathiri mchakato wa mawazo ya mtu na mara nyingi uwezo wake wa kiutendaji. Wakati mwingine dalili zinapojitokeza, watu hupata ugumu katika kuelezea tofauti ya uzoefu halisi na ule usio halisi. Kwa mfano kusikia milio au sauti ambazo hazipo, kuona vitu visivyokuwepo, kuwa na imani za ajabu kama vile watu wapo nje wanasubiri kukudhuru wakati kiuhalisia hawapo, tabia zisizo za kawaida au mazungumzo yasiyoeleweka au kukosa mpangilio, na tafsiri potofu ya vitu. Watu wengi wanapozingatia tiba huweza kuudhibiti ugonjwa huu kiasi cha kuweza kuishi maisha yenye tija na utoshelezi. Baipola ni tatizo la akili ambalo linaathiri namna unavyojisikia (hisia), kwa kimombo wanasema mood, ambapo unaweza kuwa na vipindi vya furaha au / na huzuni kupindukia. Hapa mara unajisikia huzuni sana, mnyonge au mwenye uchovu na hali ya kulia; baada ya dakika chache tu unajisikia mwenye furaha iliyopindukia na mwenye nguvu nyingi.

Msongo baada ya janga Yapo matukio yanayotokea katika jamii yetu yenye kuleta majeraha au maumivu ya kisaikolojia. Matukio haya huitwa majanga. Kwa mfano ajali, kifo cha ghafla, unyanyaswaji, ubakwaji, utekwaji, ukatili, vita, ugaidi, tishio la kiusalama, majanga ya asili kama mafuriko nk. Mtu anaweza kuathiriwa na janga kwa kuhusika, kushuhudia au kusimuliwa. Wahanga wa janga mara nyingi huwa na hisia ya kwamba ulimwengu umebadilika na hautakuwa tena kama ulivyokuwa. Mwitikio wake huambatana na kumbukumbu au ndoto zinazojirudiarudia kuhusiana na janga, kujisikia au kutenda ghafla kama vile janga linatokea tena, kushtukashtuka endapo kitu au hali fulani itakukumbusha janga, kuepuka kuwaza kitu chochote kitakachokukumbusha janga pamoja na uwepo wa hisia hasi kama vile woga, hofu, hasira, hatia au aibu. Ni kawaida hali hii kutokea baada ya janga. Watu wengi hupata nafuu ndani ya wiki chache tu bila kufanya jitihada zozote. Hata hivyo, baadhi ya watu huendelea kupata dalili kwa muda mrefu; mtu anashindwa kupata usingizi, kutulia au kufanya jambo fulani kwa makini, anaweza kujitenga au kujilaumu. Hali hii hutibika na mtu kurejea kwenye hali ya kawaida. - Fema Magazine ( April - June 2020)

Matatizo ya kula Pia kuna Bulimia, pia Ni ugonjwa unaotokana Kuna Aneroxia, ambao unajaribu kutokuwa na na tabia endelevu za ni ugonjwa mmoja wapo uzito mkubwa ila ulaji ambazo zinaathiri ambapo unataka kuwa unakuwa na vipindi afya, hisia na utendaji nashepu na uzito mdogo ambavyo unakula sana kazi wako. Hii inatokana hivyo unapunguza au halafu unajilazimisha na kuwa makini kukataa vyakula fulani kutoa chakula kupindukia ikija kwenye ili uwe na uzito mdogo, ulichokula kwa namna chakula, uzito wako na lakini pia ukiwa na zisizosahihi kama shepu yako mpaka ugonjwa huu unakuwa kujilazimisha kutapika unabadilisha vyakula ili unaogopa kunenepa. nk. kutimiza malengo hayo. Kuna aina nyingi za matatizo ya kula tafadhali soma mtandaoni pia maana kutafuna udongo na mchele pia ni tatizo.



Ulevi wa madawa na kilevi Ni kushindwa kujizuia kwa matumizi ya madawa ya kulevya ama ya kupunguza maumivu ama kilevi/ pombe kwa vile unaitegemea na unaihitaji kihisia na kimwili. Mara nyingi utegemezi huu unatokana na kujaribu kutibu / kusahau matatizo mbalimbali

V I NK AU VVA IYTTOHUIWREI Z A AFYA YAKO YA AKILI

KUACHANA NA MPENZI WAKO / MATATIZO YA KIMAHUSIANO NA WATU/ KUFIWA AU KUMPOTEZA MTU MUHIMU KWAKO KUTOFIKIA MALENGO YAKO / KUTOTIMIZA MATARAJIO YAKO UGONJWA/AJALI KUKOSA PESA / KUPITIA SHIDA KUNYANYASIKA / KUBAKWA UPWEKE KUDHARAULIWA KUKOSA KAZI KUPITIA PRESHA KAZINI/ NYUMBANI / SHULENI/ CHUONI/ KWENYE BIASHARA VIPINDI VYA MABADILIKO MAKUBWA KWENYE MAISHA MFANO KUPATA MTOTO, KUINGIA KWENYE NDOA, KUMALIZA CHUO KURUDI MTAANI, KUINGIA UTU UZIMA NK MATATIZO NYUMBANI / YA KIFAMILIA KUTENGWA KUPITIA/ KUPATA MAJANGA MAISHANI MFANO VITA, JANGA LA MOTO, KUSHUHUDIA UNYANYASAJI, AJALI NK

TABIA 20 ZINAZOWEZA KUSAIDIA AFYA YAKO YA AKILI Kufanya Mazoezi / Kuchukua Mapumziko kwenye Mitandao ya Kijamii/ Kupumzika / Kula Vizuri na kwa Wakati / Kushiriki kwenye mambo ya kijamii na marafiki au kujitolea/ Kupumzika / Relax na Fanya Mazoezi ya Kupumua / Tafuta Msaada / Jipende na Ujithamini / Kunywa Maji / Kaa na Watu Wazuri Wanaokujali/ Andika hisia zako au ongea na mtu / Lia kama unajisikia kulia / Jiongelee maneno mazuri na chanya / Lala vizuri na kwa wakati / Punguza kupokea habari mbaya au kukaa na watu wanaokufanya ujisikie vibaya / Tafuta msaada kwa wataalamu (therapist) / Fanya sana vitu vinavyokuletea furaha / Usijihukumu sana, uwe mkarimu kwako mwenyewe kwanza / Usiwe na vitu vingi vya kuviwaza au kuvifanya / Jua jinsi ya kutuliza hisia zako, jua hisia gani unayo na unaitulizaje katika njia ambazo hazina madhara kwako/ Toka nje (jua na uota wa asili husaidia sana mwili na akili kupumzika) WWW.ABIBLEGIRL.COM

WWW.ABIBLEGIRL.COM

HAUKO PEKE YAKO, WEWE SIO DHAIFU, HATA HILI LITAPITA NA IPO SIKU UTAJISIKIA VIZURI TENA

Vyakula vinavyosaidia uwe na afya ya akili nzuri

--m---(-SR---BMJVMBMKSPtaraeaeaoioastbaaemjrzrpilawhonrzaitifbiniragadecub(oeiwkvsarihleoraayirira(tcwgzryeB)lyahne)kalaiuu&ctn)kdbuerry,



Hivi karibuni mitandao ya kijamii imekuwa ni JINSI YA chanzo cha kujilinganisha, na kuwafannya watu KUJALI AFYA wengi wajisikie vibaya au hawatoshi kwa YAKO YA AKILI kulinganisha maisha yao na yale ya watu UNAPOTUMIA wanaowaona kwenye mitandao ya kijamii. Wengi MITANDAO YA wamepata sonona, kujihisi wamefeli kwenye maisha na wengine kujiua. Hivyo kutumia KIJAMII mitandao ya kijamii kwa uangalifu ni jambo la muhimu maana ina athari kwenye afya yako ya akili. Hizi hapa ni njia chache zitakazokusadia; KUUNFOLLOW WATU AU TOPIC ZINAZOKUFANYA UJISIKIE VIBAYA CHUKUA MAPUMZIKO, HATA WIKI MOJA BILA MITANDAO YA KIJAMII KUMBUKA KUWA WATU HAWAPOSTI KILA KITU MTANDAONI, WANAPOSTI MAZURI YAO TU ZIMA NOTIFICATIONS, ILI KILA SAA USIPATE HABARI KUTOKA KWENYE MITANDAO HII, UPATE NOTIFICATIONS UKIINGIA TU SIO KILA SAA KUMBUKA KWANINI UMEJIUNGA MITANDAO HII, NA FANYA HILO

SOMA ZAIDI KUHUSU AFYA YA AKILI (BONYEZA HIZI LINK USOME ZAIDI) AFYA YA AKILI KAZINI VITABU VITAKAVYOKUSAIDIA KUJUA AFYA YA AKILI VIZURI UTU UZIMA NA AFYA YA AKILI JINSI YA KUJALI AFYA YAKO YA AKILI NA MAMBO YOTE YANAYOENDELEA DUNIANI

JALI AFYA YAKO YA AKILI ASANTE SANA KWA KUSOMA, MTUMIE NA RAFIKI YAKO PIA. EUNICE TOSSY INSTAGRAM & TWITTER @EUNIETJ BLOG: ABIBLEGIRL.COM


Like this book? You can publish your book online for free in a few minutes!
Create your own flipbook