V. Viongozi wanatoa kauli za uchochezi zinazosababisha maafa makubwa. Kwa mfano, uchochezi wa Mwanzi unasababisha kuchomwa kwa nyumba, maduka, magari mimea na hata kuuliwa kwa raia. VI. Viongozi wanawatumia vijana kuwafanyia kampeni ila hawawasaidii kujiinua kiuchumi wapochaguliwa. VII. Raia wanachangia uongozi mbaya kwa njia zifuatazo: a. Wanapokea hongo kutoka kwa Papa ndipo wamchague. b. Wanazua fujo zinazosababisha maafa mengi Mwanzi anaposhindwa katika uchaguzi. c. Wanaimba na kuwasifu viongozi wasiotahili Kwa mfano, wanaimba wakimsifu Mwanzi. d. Bwana Mbavu anapowapoka akina Shamsi ardhi kwa kutumia hatimiliki bandia lakini hawalalamiki. VIII. Viongozi Wanaoshindwa katika uchaguzi wanakataa kukubali ushinde. Kwa mfano, Mwanzi anakataa kukubali kushindwa na Mwekevu, hivyo kuzua vurugu. IX. Viongozi wanazorotesha elimu ya kwao kwa kuipuuza na kuwapeleka wanao ng'ambo wakidai kwamba elimu ya kwao haiwahakikishii wanao mustakabali mwema. X. Viongozi wamekosa uwajibikaji kwa sababu wanajenga nyumba kwenye ardhi iliyotengewa upanzi wa chakula na kuanza kuharibu misitu ili kupanda vyakula huko. XI. Viongozi wanakiuka haki za binadamu. Wanawauzia raia mahindi ambayo yameharibika, hivyo kuhatarisha maisha yao XII. Viongozi wanaendeleza unafiki. Vijana wanapowafanyia kampeni viongozi hutiririkwa machozi wanapoona ngozi zao zilivyopauka na kujaa makunyanzi kwa umaskini lakini wanapochaguliwa hali husalia kuwa ileile kwa maana hawawasaidii kujiinua kiuchumi pg. 51
Athari za tamaa Maudhui ya tamaa yanajitokeza ifuatavyo: I. Tamaa ya utajiri inawachochea viongozi kunyakua hata ardhi ya madhabahu kwenye Mlima wa Nasibu ili kujenga hoteli za kitalii. II. Tamaa ya pesa inawasukuma vigogo matajiri kuwauzia raia maskini mahindi yaliyoharibika ili wazidi kutajirika. III. Tamaa ya kupanda mahindi zaidi inamchochea Lunga kukata miti Zaidi katika Msitu wa Mamba mbali na ekari 35 zilizokuwa zimekatwa na babake iii kuendeleza kilimo cha mahindi. IV. Tamaa ya mahari inawasukuma wajombawe Pete na mamake Pete kumwoza kwa Fungo akiwa angali anasoma. V. Mwanzi hataki kuachilia uongozi licha ya kushindwa na mpinzani wake; Mwekevu. VI. Tamaa ya kuishi Maisha ya kifahari inamchochea Naomi kumtoroka mumewe Lunga anapofilisika. VII. Tamaa ya pesa inawafanya Waafrika wanaoenda Ughaibuni kuwa watumwa wa Wazungu. Kwa mfano, wanafanya kazi kwa muda mrefu na kazi zenyewe ni za kudhalilisha - kuwauguza maajuza VIII. Tamaa ya kumiliki rasilimali inawachocha wakimbizi katika Msitu wa Mamba kuufyeka msitu huo na kujenga majumba ya vigae, maduka ya jumla, viduka vya rejereja na kupanda mihindi na miharage. IX. Tamaa ya kuwa viongozi inawasababisha wanasiasa wawahonge raia ili wawachague. X. Wakoloni wanajitengea mashamba yenye rotuba wakiwaacha Waafrika wakitaabika. XI. Myunani anawapokonya raia wa Kisiwa Bora mashamba yao ili kujitajirisha. XII. Viongozi wanawajengea wenyeji wa mtaa wa Sombera nyumba kisha wanazinyakua tena. pg. 52
XIII. Tamaa ya kimwili inamchochea Maya kumwacha mkewe na kumbaka mwanawe wa kambo Sauna. XIV. Tamaa ya mali inawafanya wakoloni kuwanyonya wafanyikazi kwa kuwalipa mishahara duni. XV. Tamaa ya anasa na kujitakia makuu vinamfanya Sally kuvunja uchumba wake na Billy. XVI. Tamaa ya pesa inawachochea raia kuiba mafuta ya Jori lililoanguka. Uharibifu au uchafuzi wa mazingira Suala hili limejitokeza ifuatavyo: I. Wakimbizi wanavamia Msitu wa Mamba na kuufyeka ili kupata mahali pa kulima na mahali pa kujenga nyumba. II. Viongozi wanakata miti msituni iii kujenga viwanda na kuendeleza kilimo cha michai III. Raia wa Wahafidhina wanakata miti bila kupanda mingine hali inayotishia kuzuka kwa ukame. IV. Lunga Kiriri- Kangata anawasuta wanafunzi wenzake Pamoja na walimu kwa kushindwa kustawisha mabustani ya maua hali anayosema inatishia kuzuka kwa jangwa. V. Ukataji wa miti katika Msitu wa Mamba karibu usababishe mto wa Mamba kukauka. VI. Wakimbizi katika Msitu wa Mamba wanayachafua mazingira kwa kuenda haja kwenye nyasi aidha wanatupa vinyesi vyao mahali popote kwa maana hawana vyoo. VII. Vijana wafuasi wa Mwanzi wanaharibu mazingira kwa kuchoma magari yanayohanikiza wingu la moshi hewani VIII. Viongozi wanachafua mazingira kwa kutupa Sandarusi katika mtaa wa Sombera. IX. Watoto katika mtaa wa Sombera wanachafua mazingira kwa kuenda haja kubwa katikati ya reli pg. 53
X. Viongozi wanakata miti katika Msitu wa Mamba na kuchoma makaa. XI. Viongozi wanakata miti na kupasua mbao katika Msitu wa Mamba na kuzisafirisha usiku wa manane. XII. Raia wanatupa taka katika viambaza vya majengo jijini badala kuzitupa kwenye majalala XIII. Raia wanakojoa kwenye viambaza vya majengo jijini anamofanya kazi Neema badali ya kuenda msalani. XIV. Raia walichafua viambaza vya majengo jijini kwa kuchora picha za wanasiasa. XV. Watu kijijini mwa Mwagemi na Mwangeka wanachafua mazingira kwa kuenda haja kubwa vichakani. (uk. 180) Changamoto zinazoibuka kutokana na uyabisi wa wanawake. (i) Uavyaji mimba: Mamake Sauna anamsaidia Sauna kuavya mimba ya babake jambo ambalo halikumfurahisha. (ii) Ndoa kuvunjika: Badala ya Subira kutatua mgogoro wake na mavyaa wake, anaamua kuiacha familia yake hivyo basi kupelekea kuvunjika kwa ndoa yao na Kaizari. (iii)Ulanguzi wa watoto: Sauna anaudhika kwa kutotetetewa na mamake alipobakwa na babake. Anatoroka kwao na kuanza biashara ya ulanguzi wa watoto. (iv)Dhiki za kisaikolojia: Umu anapitia katika dhiki za kisaikolojia baada ya mamake Naomi kuwatoroka na nduguze. (v) Uyatima: Subira alipojitia kitanzi, anawaacha wanawe Lime na Mwanaheri kwa uyatima. (vi)Upweke: Naomi anawatoroka Umu na ndugu zake. Baada ya ndugu zake Umu kutekwa nyara, Umu anaishi maisha ya upweke. (vii)Vifo: Wanawake wengi wameavya mimba na kusababisha vifo vya watoto wachanga. Mf: Neema, Sauna na Pete. (viii)Magonjwa: Lunga anapatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu baada ya kuachwa na mkewe Naomi. pg. 54
(xi) Dhiki za malezi: Lunga aliachiwa uchungu wa kuwalea watoto peke yake na Naomi. (x) Ukosefu wa malezi bora: Chandachema anakosa malezi bora ya mamake Rehema aliyemtelekeza kwa kumwachia bibiye. (xi) Ndoa za mapema: Mamake Pete alimlazimisha kuolewa na Mzee Fungo akiwa dasara la saba. (xii)Ukosefu wa mahitaji ya kimsingi: Pete anatelekezwa na mamake hivyo basi kukosa mahitaji ya kimsingi k.v Sodo. (xiii) Utekaji nyara: Dick na Mwaliko walitekwa nyara na kijakazi Sauna baada ya kutelekezwa na mamaye Naomi. (xiv) Ajira za watoto: Sauna anaajiriwa kazi hatari ya kuwalangua watoto na Bi. Kangara baada ya kukosa malezi bora ya mamake. (xv)Ukosefu wa malazi: Licha ya Chandachema kuwa na mama, anakosa kwa kulala. Analala katikati ya michai. (xvi) Kukatizwa kwa masomo: Baada ya Dick kuachwa na mamake mzazi, masomo yake yaligonga mwamba. (xvii) Ukosefu wa karo: Chandachema anakosa karo licha ya kuwa na mamake Neema. Anafadhiliwa kimasomo na wahisani. (xix) Kazi za Sulubu: Watoto wachanga wanafanya kazi za Sulubu baada ya kutelekezwa na mama zao. mf: Chandachema anachuma majani chai akiwa darasa la tano. (xx) Dhuluma za kimapenzi: Pete anadhulumiwa kimapenzi na Nyangumi. Hii inatokana na kutelekezwa na mamake. (xxi) Mimba za mapema: Pete aliozwa na mamake kwa Mzee Fungo jambo linalopelekea kupata mimba za mapema. Nafasi ya vijana katika jamii. i)Wasomi kwa mfano Tila, umulkheri na mwaliko. ii)Walanguzi wa dawa za kulevya kwa mfano Dick alisafirisha dawa za kulevya katika mataifa mengi. iii)Wenye bidi – Umu ana bidi masomoni / Dick alikuwa na bidi katika biashara. iv)Watamaduni – Tuama aliunga mkono utamaduni wa kukeketwa kwa wasichana. pg. 55
v)Wapenda fujo. walitumiwa na wanasiasa kutekeleza maovu ya mauaji na kuharibu mali. vi)Katili.mabarobaro watano waliwabaka Lime za mwanaheri na kumkata subira kipajini. vii)Vigeugeu. Wanapotishwa na wanasiasa na kusababisha uharibifu katika jamii. viii)Watambuzi.Anatambua matatizo yanayokumba jamii yake kwa mfano ukosefu wa haki. ix)Watetezi wa haki. Ana azima ya kuwa jaji katika mahakamani kwa miongo mingi. x)Wenye utu kwa mfano Umu na Hazina. xi)Karimu.kwa mfano Umu alimsaidia Hazina kwa kumpa shilingi mia mbili. Jinsi vijana walizamisha merikebu ya wahafidhina i. Genge la wavulana watano linawabaka lime na mwanaheri kwa kukisia kwamba wazazi wao hawakumpagia kwa mwanzi. ii. Wanazorotesha usalama kwa kumvamia Subira na kumkata kwa sime kwa kumdhania kuwa hakumpigia kura Mwanzi. iii. Vijana wanawavamia abiria barabarani wakiongozwa na kijana aliyekuwa amevaa shati lenye maandishi “Hitman” na kuwachomea ndani ya magari. iv. Wanayachoma magari barabarani. v. Sauna awaiba watoto wake Lunga-Dick na Mwaliko na kuwatenga na dada yao Umu. vi. Pete anameza vidonge ili kuavya kitoto chake cha pili ila hakufanikiwa. vii. Zohali anajiingiza katika mapenzi na kupata mimba akiwa kidato cha pili. viii. Wanawe Kiriri wanakataa kurundi nyumbani. Kutoka ughaibuni walikoenda kusoma. ix. Vijana wanamdhalilisha Mwekevu baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi. Kipanga anaachia masomo kidato cha pili na kuanza kunywa kangara –ananusurika kifo. x. Wanafunzi shukeni –anakomesea Ridhaa, wanaendeleza ukabila dhidi ya wanafunzi walowezi. xi. Vijana wanapokea hongo kutoka kwa wanasiasa kama papa iti wawachague, hivyo kuimarisha uongozi mbaya. xii. Vijana wasichana wanajifungua watoto na kuwatupa kwenye majaa ya taka kama Yule aliyeokolewa na Neema. xiii. Wanavunja sheria kwa kuandamana huku wamebeba picha za Mwanzi na kumhimiza atawale ingawa alikuwa ameshindwa pg. 56
liandikwalo ndilo liwalo i. Neema na Mwangemi wanajitahidi kupata mtoto lakini hawafanikiwi na wanaishia kumpanga Mwaliko. ii. Wafuasi wa Mwanzi wanajaribu kushinda ushindi wa Mwekevu lakini wanashindwa. iii. Kaizari anajitahidi kuzuia wahuni wasiwabake binti zake lakini wanamzidi nguvu na kuwabaka. iv. Lunga anajitahidi kumrithia na kumpendeza mkewe Naomi lakini hatimaye anamtoroka na kumwachia Watoto v. Kiriri anampinga Annette asiende ughaibuni lakini anampuuza na kuhamia huko. vi. Kiriri anawasihi wanawe warudi nyumbani lakini waliendelea kuishi ughaibuni hata baada ya kukamilisha masomo yao. vii. nyanyake Pete anajizatiti kupinga ndoa ya Pete lakini hatimaye Pete anaozwa. viii. Kipanga anataka kuambiwa babake halisi baada ya aliyemdhania kuwa babake kumkana lakini mamake hakumwambia. ix. hata baada ya mabwanyenye kutoa hongo ili nyumba zao zisibomolewe katika mtaa wa Tononokeni, zianbomolewa. x. Dick anakataa kutumiwa na Buda kulangua dawa za kulevya lakini anamtishia na baadaye kuuza dawa za kulevya. xi. Naomi alimtoroka Lunga kwa sababu ya umaskini lakini anaishia kuteseka Zaidi na baadaye kufa xii. Amize Lucia wanajizatiti kupinga ndoa ya Lucia lakini baadaye Lucia anaolewa. xiii. Wanaume wanatishia kumtusi Mwekevu anapojitosa siasani ili kumvunja moyo lakini anavumilia mpaka anachaguliwa kuwa kiongozi wa Wahafidhina. xiv. Pete anakunywa dawa ya kuua panya ili afe lakini anapelekwa katika kituo cha afya cha Mwanzo Mpya na kuendelea kuishi. xv. Pete anajaribu kuavya mimba ya mtoto wake wa pili na wa tatu lakini anaishia kuwazaa Watoto hawa. pg. 57
Baba umewahi kumwona mtoto wa miaka hamsini ambaye hajasota; sikwambii kusimama dede?” Jadili ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari katika kauli hapo juu. Tumia hoja ishirini i. Ni kinyume na matarajio yetu kuwa baada ya miaka hamsini ya uhuru bado taifa la Uhafidhina kushikilia kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi bora ii. Ni kinaya pia kuwa tangu uhuru wa wahafidhina bado Tuama anashikilia mila na tamaduni hasi kuwa ni lazima apashwe tohara ndipo awe mwanamke kamili iii. Ni kinaya kuwa bado nchi ya wahafidhina inapokea mikopo kutoka mataifa ya kigeni na kuendelea kushabikia mkoloni aliyewatawala iv. Ni kinyume kuwa bado kuna wakoloni masetla ambayo bado walikuwa wakimiliki mashamba makubwa Uhafidhina huku wenyeji wakikosa ardhi v. Ni kinaya kuwa kahawa na bidhaa bora zinazokuzwa na kutengenezwa Uhafidhina zinauzwa ng’ambo huku wao wakipata visio bora vi. Aidha ni kinaya kuwa miaka hamsini baada ya Uhuru bado wahaidhina hawakuwa wameweza kukabiliana na ukabila mwao…bado kulikuwa na vita baina ya makabila yao vii. Vilevile ni kinaya kuwa miaka hamsini baadaye bado wanaume wazee hujihusisha kimapenzi na wasichana wadogo bila kujali athari zake k.v Mwalimu Fumba, Mzee Maya n.k viii. Aidha ni kinaya kuwa wazazi hawajaweza kujua jinsi ya kuwalea watoto wao hivyo basi kuwatelekeza k.v Wazazi wa Chandachema, wa Zohali n.k ix. Isitoshe, ni kinyume na matarajio yetu kuwa mika hamsini baada ya uhuru, serikali bado haikuwa imeweza kukabiliana na tatizo la umaskini jinsi ilivyoahidi baada ya uhuru x. Pia serikali hii inashindwa kuzuia magonjwa mbalimbali yanayowakumba wahafidhina licha ya kuahidi miaka hamsini iliyopita uhuru ulipopatikana. xi. Aidha uongozi mbaya bado unaendelea Uhafidhina licha ya kumwondoa mkoloni miaka hamsini iliyopita kwani wanachukua usukani bado wanaendeleza ukatili kama vile mkoloni. xii. Bado serikali haikuwa imweza kupiagana na tatizo la ufisadi linaloathiri ukuaji wa maendeleo yake maiaka hamsini baadaye xiii. Bado suala ya unyakuzi wa ardhi linaendelea licha ya kumwondoa mkoloni k.v Shamsi anatueleza jinsi ardhi yao iliyonyakuliwa na mwenye nguvu. pg. 58
xiv. Licha ya mkoloni kuondoka miaka hiyo yote, bado utabaka ulishamiri Uhafidhina na serikali haijaweza kukabiliana nao. xv. Mbali na hayo, licha ya kuwa Uhafidhina ilikuwa imepata uhuru miaka hamsini, bado demokrasia haikuwa imedumishwa hasa katika uchaguzi uk 19 xvi. Ni kinaya kuwa katikamuhafidhina mtu aliye hata na shahada tau hawezi kupata ajira na hivyo huenda mataifa ya kigeni kutafuta ajira miaka hamsini baada ya uhuru xvii. Ni kinaya kuwa viongozi wa uhafidhina wanaona elimu ya kwao kuwa duni badala ya kuikuza miaka hamsini tangu uhuru uk65 xviii. Ni kinaya kuwa maiaka hamsini ya uhuru, bado mauaji ya kiholela hasa vijana yanafanywa bila suluhisho ya janga hilo. xix. Tangu uhuru, bado Uhafidhina haijaweza kudumisha usalama wake kutokana na vita vya wenyewe xx. Bado hamna mshikamano wa kitaifa tangu uhuru ingawa ni mhafidhina mwenzao anayengoza matatizo ya mwiba wa kujindunga riwayani i) Jumba moja la Ridhaa linabomolewa kwa kuwa alilijenga katika ardhi iliyotengewa ujenzi wa barabara katika mtaa wa zari. Hakuchunguza uhalali. ii) Terry mkewe Ridhaa anapuuza maonyo na maneno ya mumewe kuhusu mkasa ambao ungetokea hivyo anateketea. iii) Ami wamwangeka anaagamia katika mkasa wa moto alipoenda kuwasaidia watu waliokuwa wanateketea. iv) Walioteketea katika moto wa lori walijiigiza matatani wenyewe kwani walikuwa wameonywa kulikuwa na hatari. v) Uhasama, migogoro na ukosefu wa mahitaji muhimu unaoikumba familia ya Mwimo Msubili hii ni kwa sababu ya yeye kuwaoa wake wengi. vi) Kufutwa kazi kwa Lunga Kangata Kiriri baada ya kukataa kukubali mahindi ya jano kuuziwa wananchi ni mwiba wa kujidunga. vii) Mauti yanayowakumba vijana waliokuwa wakiadamana baada ya sherehe za kuapishwa kwa kiongozi mpya. pg. 59
viii) Tendo la Subira kuondoka nyumbani na kumwacha mumewe na watoto ni mwiba wa kujindunga kwa mumewe. ix) Pete anapokubali kuolewa na Nyangumi bila kufanya uchunguzi wa kina. x) Tukio la Zohari kupata mimba na kutumbukia katika mateso mengi. xi) Tendi la Mwangeka na Mwangemi kufanyia babu yao mzaha, kwa kuwa usiku mmoja aliamua kuwalipua viboko. xii) Mwangeka anakubaliana na Tila kuigiza maombolezi ya Dedan Kimathi ambayo yanamfanya babake kumwadhibu kwa kutowajibika. xiii) Kukamatwa kwa Sauna na mwajiri wake Bi. Kangara kwa kujihusisha na Biashara ya ulanguzi wa watoto. xiv) Tuama anaathirika vibaya baada ya kupaswa tohara na kulazwa hospitalini ni tendo alilolitenda kinyume na mapenzi ya baba yake. xv) Walevi wenza wa Shamsi ambao wanapoteza uwezo wa kuona au uhai wao kwa kubugia vileo. xvi) Mumwewe Selume anamfukuza mkewe kwa kuwa si wa kabila lake baadaye anamlea mtoto peke yake. xvii) Mandu anapouawa katika vita akiwa ughaibuni ni mwiba kwani huenda hangepoteza maisha kama hangeenda huko mapema. xviii) Fujo zinazosababishwa na uhafidhina baada ya uchaguzi ambapo wanapoteza uhai na mali. xix) Wakimbizi waliohamia katika mimea na baadaye kufukuzwa ulikuwa mwiba kwani si halali kulima msituni. xx) Naomi kumwacha mumewe Lunga Kiriri na watoto na baadaye kuwatafuta baadhi ya kifo cha bwanake ulikuwa mwiba wa kujindunga. athari za vita i. Vifo: Vita baina ya pande za mwekevu na ule wa mpinzani wake wa kisiasa vilisababisha mauaji ii. Uharibifu wa mali: Aila ya ridhaa kuangamizwa katoka moto; nyumba na mali kuteketezwa iii. Ukosefu wa makazi bora – kaizari na wenzake wamekosa makazi bora kule msitu wa mamba walikotorokea. Vibanda vinasongamana pg. 60
iv. Huzuni – ridhaa alihuzunika sana baada ya aila yake na mali kuteketezwa kwa moto v. Hasara kwa wafanyibiashara – wahalifu waliingia katika maduka ya kibiashara za kihindi, kiarabu na kiafrika na kupora mali ya wenyewe vi. Kutiwa nguvuni: waporaji waliopora maduka/mali wakati wa vita walitiwa nguvuni na kukabiliana na mkono wa kisheria hapo baadaye vii. Watu kutoroka makwao: Wahafidhima walihama makwao wakati wa vita bila kujue walikokuwa wajuelekea / ukimbizi viii. Utegemezi: kukosekana kwa chakula katika kambi ya msitu wa Mamba kulifanya watu kutegemea msaada ya chakula toka kwa wahisani k.v shirika la msalaba mwekundu ix. Majeruhi: kuna mwanaume aliyevamiwa na kuumizwa kwenye mgogoro wa kupigania ardhi katika eneo la tamuchungwa. Alilazwa katika kituo cha Mwanzo Mpya. x. Kukatiziwa masomo ka vile Lime na Mwanaheri xi. Kusababisha uyatima - vita katika kambi ya Msitu wa Mamba vinasababisha walinda usalama kuua wazazi na kuwaacha watoto peke yao xii. Kuporwa – wafanyabiashara wanaporwa bidhaa zao fujo za baada ya uchaguzi zinapozuka. xiii. Kukatwa - subira anavamiwa na kukatwa na wahuni xiv. Kubakwa – baada ya fujo kuzuka, Lime na Mwanaheri wanabakwa na wahuni xv. Kukwama kwa usafiri – vijana wanalemaza shughuli za usafiri kwa kwenda barabarani na kuanza kuchoma magari xvi. Magonjwa – Ridhaa aliugua shinikizo la damu kutokana na mshtuko wa kupotea jamaa zake. xvii. Kusubaratishwa kwa jamaa / familia xviii. Athari za kisaikolojia pg. 61
Migogoro katika Chozi la Heri Migogoro ni hali ya kuwepo kwa mivutano/mikinzano/mfarakano baina ya wahusika katika kazi ya fasihi. K.m. 1. Mgogoro kati ya Mzee Kedi na familia ya Ridhaa wakati mzee Kedi anashiriki katika mauaji ya familia ya Ridhaa. 2. Mgogoro shuleni kati ya Ridhaa na wanafunzi wenzake wanapomwita “mfuata mvua” 3. Mgogoro wa kijnsia kati ya Mwekevu na Mgombea wa kiume. Mwekevu anarushiwa cheche za matumizi. 4. Mgogoro wa kijamii unajitokeza baada ya mkoloni kupuuza sera za mwafrika za umiliki wa ardhi. 5. Mgogoro katika familia yam zee Mwimo Msubili kwa sababu familia yake ilikuwa kubwa na hangeitosheleza kwa chakula. 6. Mgonjwa mmoja kwenye hospitali ya mwanzo mpya anapata majeraha mabaya baada ya kuvamiwa kwenye mzozo wa ardhi kule Tamuchungu. 7. Panatokea mgogoro kati ya baba na mama Pete. (uk 147) 8. Ridhaa anajipata katika hali ya mgogoro wa nafsi. (uk. 12) ……… baada ya muda wa mvutano wa hisis na mawazo. 9. Mgogoro wa kisiasa kuhusu ni nani atakayekuwa kiongozi wa jamii kati ya mwanamme na mwanamke (uk. 19) 10. Mgogoro kati ya raia na polisi wakiwa katika harakati za kudumisha Amani (uk. 19) 11. Nyamvula anajikuta katika mgogoro wa nafsi yake wakati ambapo Imani yake inakinzana na kazi ya mmewe ya kuwa mwanajeshi matatizo yanayowakumba wahafidhina a) Kupoteza jamaa – Familia ya Ridhaa inateketea ndani ya nyumba yake kutokana na ghasia za kikabila. b) Ubakaji – Lime na Mwanaheri wanabakwa na genge la vijana ambao wanawavamia nyumbani. pg. 62
c) Tamaa ya mali – Wafanyabiashara katika jumba la kupangisha la Ridhaa wanawafungia wateja wao ndani wakati wa mkasa wa moto ili wasipate mali. d) Tatizo la makazi – Watu wanatolewa katika msitu wa Mamba kwa kulazimishwa japo walipewa hatimiliki na serikali. e) Ulanguzi wa dawa za kulevya – Dick anapelekwa kwa Buda ambapo analazimishwa kufanya kazi ya ulanguzi wa dawa za kulevya. f) Ukosefu wa maadili – Fumba anamringa Rehema mwanafunzi wake wa Kidato cha Tatu. - Bwana Maya anamdhulumu kimapenzi Sauna, mwanawe wa kambo. g) Kudhulumiwa na vyomba vya Dola – Askari, wakiwemo wale wa ‘Penda Sugu Ujute’, wanatumia vitoza machozi na hatimaye kuwapiga risasi vijana na kuwaua. h) Tatizo la malezi – Naomi, Annette and Subira wanawasaliti wanao na waume zao wanapoamua kuwaacha na kwenda kwingineko. i) Ulanguzi wa watoto – Bi. Kangara anamtafutia Sauna ajira ya kuwateka nyara watoto wa watu na kuwauza. j) Tatizo la huduma za matibabu – Matajiri wanawadhulumu maskini wasiojiweza kwani wananyakua dawa zilizotengwa kwa ajili yao. k) Kujichukulia sheria mikononi – Wanajamii wanaonyesha ukatili wanapompiga Lemi kisha kumteketeza kwa kisingizio cha kuiba simu. l) Ukosefu wa ajira – Vijana wanaohitimu kutoka vyiuoni hawapati nafasi za kazi au zinatolewa kwa mapendeleo. m) Ufisadi – Watu wanaogombea nafasi za uongozi huwahonga wananchi kwa hela na vitu vinginevyo ili wapigiwe kura mfano: Papa. n) Ndoa za mapema – Pete anaozwa akiwa mchanga sana na wajomba zake. Anaozwa kwa Fungo kama mke wa nne. o) Ukeketaji wa wanawake – Tuama anaelezea jinsi yeye na wenzake walivyopashwa tohara ili wasikose waume. Hata hivyo, wasichana wengi huishia kuvuja damu nyingi na hata kufa. p) Ukosefu wa kazi – Shamsi anaeleza jinsi nafasi za kazi hutolewa kwa mapendeleo hivyo wengi huishia kuwa maskini hasa walio na shahada mbalimbali, pg. 63
q) Pombe haramu – Shamsi anasema kuwa wengi hufa na kupofuka kutokana na unywaji wa ndengelua iliyotiwa vijasumu ili iive haraka. r) Uavyaji mimba – Sauna anaavishwa mimba na mamake ili asiiletee familia yake fedheha. - Pete alijaribu kuavya mtoto wake wa pili bila kufanikiwa. s) Mimba za mapema – Zohali alipata mimba akiwa kidato cha pili. - Rehema aliringwa na mwalimu wake Fumba akiwa angali shuleni. t) Umaskini – Ni kutokana na ukata ambapo wananchi wanaenda kuchota mafuta kutoka kwa lori lililobingiria ili wayauze kwa watu wenye magari ya kibinafsi. binadamu alivyomwagikiwa na maji riwayani i) Lunga kumwagikiwa na maji pale anapoachwa na mkewe Naomi ii) Umu na nduguye wanamwagikiwa na maji kwa kuachwa mayatima wakati Lunga anapoaga iii) Ridhaa anamwagikikwa na maji wakati anapoipoteza aila yake yote isipokuwa Mwangeka iv) Mwangeka anamwagikiwa na maji kufuatia kifo cha mkewe na mtoto wake v) Zohali anamwagikiwa na maji pale anapotungwa mimba katika umri wa ujana na kupelekea afukuzwe shuleni na kuteswa na wazazi vi) Waafrika wanamwagikiwa na maji pale wanapokatazwa na wakoloni kulima mazao yaletayo fedha huku ikiwalazimu kufanya vibarua kwao vii) Baadhi ya vijana wa rika la Tuama wanakufa baada ya kupashwa tohara viii) Hospitali inamwagikiwa na maji pale Selume analalamikia ukosefu wa mwangaza, ukosefu wa glavu na deni kutokana na usimamizi duni ix) Wakaazi wa msitu wa mamba wanaharibikiwa pale wanapofurushwa huku vyakula walivyolima vikiibiwa na viongozi x) Vijana barobaro wanaotumiwa na wanasiasa kuandamana wanamwagikiwa wa maji pale wanapomiminiwa risasi vifuani wa walinzi huku wakiuawa xi) Kitoto kinachookotwa na Neema kilimwagikiwa na maji pale kilitupwa na mama mzazi badala ya kukilea xii) Ridhaa anasimulia mwanawe Mwangeka vile walivyobomolewa nyumba zao kwenye mtaa wa Zari, hawakupewa fidia yoyote nao wale waliowauzia viwanja hivi waliingia mitini xiii) Lunga kufutwa kazi na mkurugenzi kwa kupinga mradi wa ununuzi mahindi pg. 64
changamoto zinazoikabili jinsia ya kike katika riwaya ya Chozi la Heri i) Matusi na vitisho - Bwana Maya alipoulizwa maswali na mkewe alimpiga makonde, kumpa vitisho na matusi. Aidha, anaselea kumwuliza sababu za kuhusiana ngono na bintiye Sauna ii) Kubakwa - Sauna anabakwa na babake wa kambo Bwana Maya. Mamake naye anamsaidia kuavya mimba hiyo iii) Ndoa za mapema - Pete baada ya kupashwa tohara anaozwa kwa mzee Fungo kwa lazima. Nyanyake anajaribu kumtetea lakini hakufaulu iv) Kukatizwa elimu - kiu yake Pete ya kuendelea kusoma inakatizwa baada ya ndoa ya lazima kwake bwana Fungo v) Waume zao kukosa uaminifu katika ndoa - Mfano Bwana Tenge anashiriki ngono na wanawake wengi wakati Bi Kimai yuko kijijini vi) Uongozi / ushindi wake kudunishwa - ushindi wake Mwekevu unadhalilishwa na mpinzani wake kuandaa maandamano ili kupinga kuchaguliwa kwake vii) Kutelekezwa - mfano ni Chandachema anayeondoka kwa jirani yake baada ya kulalamikia vitu vidogo vidogo kuonyesha kutoridhika kuishi naye. Aidha Zohali anatelekezwa na wazazi wake na kuishia kuwa ombaomba mjini viii) Mazingira duni ya kazi - Subira anafanya kazi katika mazingira duni yasiyo na nguvu za umeme pia kukosa vifaa muhimu vya kufanyia kazi ix) Kufukuzwa shuleni - Zohali anafukuzwa shuleni baada ya kupata mimba x) Tamaa ya maisha ya juu - mfano ni Sally mpenziwe Billy anayemtaliki kwa kujengewa chumba kama tundu la ndege. Aidha Naomi mkewe Lunga anamtaliki kwa kuona uduni wa maisha yao baada ya Lunga kufutwa kazi xi) Kujitia kitanzi - Subira baada ya kumtoroka mumewe anakunywa sumu kwenye chumba huku amejifungia xii) Utasa - Neema, mkewe Mwangemi anakosa mtoto hivyo kumpanga Mwaliko xiii) Ujane - Rachael Apondi ni mjane wa Mandu. Hivyo anaposwa na Mwangeka baadaye xiv) Kifo - Lilly Nyamvula, Anatila, Becky na mkewe Ridhaa wanaangamia katika mkasa wa moto kwenye jumba kubwa lake Ridhaa baada ya ghasia za uchaguzi kuzuka pg. 65
xv) Simango la wanafamilia - jamaa zake Kaizari hawakukoma kumwita Subira mwizi wa mali yake mumewe na jamaa zake. Hivyo anamtaliki Kaizari. xvi) Umaskini - Umaskini wake Chandachema unamfanya kufanya kazi duni. Aidha, kutokana na umaskini wake Sauna, unamfanya ashiriki biashara mbovu ya utekaji nyara kwa watoto na kuwa kijakazi Mapuuza Ni hali ya kutojali, hivyo kuishia kujisababishia uchungu/shida au kuwasababishia watu wengine uchungu. i. Walinda usalama wanapuuza jukumu lao la kulinda usalama na kuwaua raia vita vinapotokea baada ya Mwekevu Tendakazi kutawazwa kuwa kiongozi wa Wahafidhina. ii. Viongozi hawashughuliki kuitunza misitu- wnauharibu Msitu wa Mamba kwa kukata miti na kuchoma makaa na kupasua mbao. iii. Mwanamke mmoja anajifungua na badala ya kujitwika jukumu la kumlea mwanawe, anamtupa kwenye taka anakookotwa na Neema. iv. Kiriri anamrai mkewe Annette asiende ughaibuni ili wasaidiane kuondoleana upweke lakini anampuuza na kwenda-hatimaye Kiriri anaishia kufa kutokana na upweke aliokuwa ameachiwa na Annette. v. Nyanyake Pete anawarai wajomba na mamake Pete kutomwoza kwa Fungo ili akamilishe masomo yake lakini wanampuuza na kumwoza kwa lazima, hivyo kumkatizia masomo yake. vi. Walowezi kama Ridhaa katika Msitu wa Heri wanapuuza tahadhari ya vikaratasi vilivyokuwa vikiwatahadharisha kuhusu gharika ambayo ingefuata baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya-hatimaye Ridhaa anachomewa familia yake vii. Baba Kairu anapuuza wajibu wake kwa Kairu kwa kumwacha kutaabika katika umaskini ilhali yeye ni tajiri kwa sababu alimzaa nje ya ndoa. Kairu anasoma kwa taabu. Mamake anamlilia mwalimu mkuu kumruhusu kulipa kidogokidogo hadi mwisho wa mwaka. viii. Fumba anapuuza wajibu wake wa kumtunza mwanawe Chandachema kwa kumwachia mamake malezi ya mtoto huyo na kuhamia Uingereza. pg. 66
ix. Kaizari anapuuza wajibu wake wa kumkinga mkewe Subira dhidi ya uhasama wa mamake kwa sababu ya tofauti za kiusuli, hivyo kumsababisha Subira kuivunja ndoa yao kwa kumtoroka. x. Viongozi wanapuuza umuhimu wa kunadhifisha mazingira kwa kumwaga taka katika mtaa wa Sombera, bila kuwazia afya ya raia wanaoishi katika mtaa huo. xi. Raia wanapuuza jukumu lao la kuuboresha uongozi kwa kupokea hongo kutoka kwa wanasiasa kama Papa na kuwapigia kura, hivyo kuendeleza uongozi mbaya. xii. Tuama anapuuza juhudi za babake Mzee Maarifa anayepiga vita tohara ya wasichana kwa kujificha na kutahiriwa. xiii. Tuama ameona jinsi ambavyo wasichana wenzake wamekufa kutokana na kupashwa tohara ila anazidi kuisifu tohara hiyo kwa kudai kuwa bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. xiv. Naomi anapuuza juhudi za mumewe Lunga za kujisabilia kwa hali na mali kumridhia na kumpendeza kwa kumtoroka na kuivunja ndoa yao. xv. Lunga anapinga raia kuuziwa mahindi yaliyokuwa yameharibika lakini viongozi wanampuuza na kuwauzia mahindi hayo. xvi. Wazazi wake Zohali wanapuuza wajibu wao wa kumwelekeza mwanao Zohali baada ya kupachikwa mimba kwa kuanza kumsimanga na kumdhalilisha, hivyo kumsababisha kutoroka nyumbani. xvii. Polisi wanapuuza jukumu lao la kuhakikisha kwamba ni magari yaliyo katika hali nzuri yanayohudumu barabarani kwa kuyaacha magari makuukuu barabarani kwa sababu yanamilikiwa na miamba isiyogusika. xviii. Wizara ya Ardhi na Makao ikishirikiana na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Halmashauri ya Kitaifa ya Barabara ilitoa notisi kwa mabwanyenye wanaomiliki majumba katika mtaa wa kifahari wa Tononekeni na kuipuuza kwa kutoa milungula ili majengo yao yasibomolewe-hatimaye wanaishia kupata hasara kwa kuwa yanabomolewa xix. Viongozi nchini Wahafidhina wanapuuza umuhimu wa kuimarisha viwango vya elimu katika taifa lao kwa kuwapeleka wanao katika mataifa ya nje kusomea huko. Wanaona kwamba elimu ya kwao haiwahakikishii wanao mustakabali mwema. pg. 67
xx. Ridhaa anamwambia mkewe Terry kwamba milio ya bundi iliashiria kutokea kwa jambo Fulani, Terry anampuuza na kushangaa jinsi daktari mzima anavyojishughulisha na mambo ya ushirikina-hatimaye Terry anaishia kuchomwa pamoja na watoto wake. Elimu i. Shule imesawiriwa kama mahali pa kuwapa wanafunzi mbinu-ishi za kukabiliana na changamoto za maisha. Mfano Mwalimu Dhahabu anapogundua masaibu ya Umu anamhimiza kuwa jasiri ili kukabiliana na changamoto hizo ii. Elimu ina jukumu la kukuza vipawa/talanta za wanafunzi. Mfano kipawa cha Lime cha kuigiza kimeimarika akiwa shuleni, aidha nduguye Mwanaheri anajizatiti kupalilia kipawa chake cha kughani mashairi iii. Elimu ni chombo cha kuleta mabadiliko katika jamii-Mwalimu Dhahabu anamshauri Mwanaheri kuandama elimu kwani ndiyo nyenzo ya kumwezesha kuleta mabadiliko katika jamii. iv. Elimu imesawiriwa kama chombo cha kukengeusha vijana. Wanawe Kiriri wanakataa kurudi nyumbani kwao hata baada ya kukamilisha masomo yao kule ughaibuni. v. Elimu ina wajibu wa kuimarisha umoja na mshikamano wa kijamii. Baada ya Ridhaa kudhulumiwa na wanafunzi wenzake kwa sababu ya tofauti za kikabila, Mwalimu anawashauri wanafunzi hao kuhusu umuhimu wa kuishi pamoja kwa mshikamano. vi. Mimba za mapema zinaathiri masomo ya wanafunzi. Mfano Zohali anafurushwa shuleni baada ya kupatikana akiwa mja mzito vii. Kazi za wazazi zinachangia wanafunzikuacha shule. Duma na Kemi wanaacha shule baada ya wazazi wao kuhamishwa kutoka kule walikokuwa wakifanya kazi. viii. Ridhaa anapodhulumiwa na wanafunzi wengine kwa kuwa mwanafunzi mlowezi, mama yake anamshauri kwamba elimu ni chombo cha kueneza amani na upendo wala si fujo na chuki. ix. Elimu ina jukumu la kuadilisha wanafunzi. Mwalimu anawashauri wanafunzi wanaomdhulumu Ridhaa kuhusu umuhimu wa kuishi pamoja kwa mshikamano hatimaye wanasitisha dhuluma zao dhidi ya Ridhaa. pg. 68
x. Elimu imesawiriwa kama chombo cha ajira. Baada ya Mwaliko kukamilisha masomo yake ya shahada ya uzamili anapata ajira katika kampuni ya Magazeti ya Tabora kama mhariri xi. Elimu ya ng’ambo imesisitizwa kuwa elimu inayowapa wanafunzi mustakabali mwema. Hii ndiyo sababu viongozi na matajiri kama Kiriri wanawapeleka wanao ughaibuni kusoma ili wawe na mustakabali mwema. xii. Elimu ya chuo kikuu inakashifiwa kwa kutowapa wanafunzi stadi za kuwawezesha kujitegemea kimaisha. Inawasababisha kutegemea ajira tu. xiii. Elimu ni ghali. Kedi anamtegemea Ridhaa kuyadhamini masomo ya wapwaze, aidha Kangata anamtegemea Kiriri kuyadhamini masomo ya wanawe. xiv. Elimu huwapa wanafunzi uwezo wa kuafikia malengo yao maishani. Mfano Tila anataka kusoma na kuwa jaji katika Mahakama kuu xv. Elimu inazindua-Mwalimu Meli anawazindua wanafunzi kuhusu umuhimu wa kutopima uwajibikaji wa mtu kwa misingi ya kijinsia, hali inayomchochea Tila kuja nyumbani na kumfahamisha babake Ridhaa. Ujenzi wa jamii mpya Kujenga jamii mpya ni kurekebisha maovu yaliyokuwa yakitendeka zamani kwa kutenda mema. i. Tila anataka jamii ambayo wananchi wanapata haki mahakamani. Anasuta mahakama za taifa la Wahafidhina kwa kuficha faili za washukiwa hivyo kuwasababisha kukaa kwenye rumande kwa miongo kadhaa. ii. Mwalimu Meko anaionya jamii dhidi ya kuupima uwajibikaji wa mtu kwa misingi ya jinsia. Anawahimiza wanajamii kuwapa waume na wake nafasi sawa. iii. Ridhaa anahimiza usawa wa kijinsia kwa kuwaelimisha wanawe wote- wa kiume na wa kike-Tila na Mwangeka. iv. Tila anawahimiza wanajamii kumchagua kiongozi wa jinsia yoyote, awe mwanamke au mwanamume almradi alete maendeleo katika taifa lao. v. Lucia –Kiriri anawatahadharisha wanajamii dhidi ya ukabila kwa kukubali kuolewa katika ukoo wa Waombwe ambao una uadui na ukoo wao wa Anyamvua. pg. 69
vi. Umu anafunza umuhimu wa kuwasaidia wasiojiweza/ maskini katika jamii. Anampa ombaomba mjini Karaha shilingi mia mbili licha ya mamake mzazi kukataa kuwasaidia. Aidha Apondi na Mwangeka pia wanahimiza jamii kuwasaidia wasiojiweza kwani wanawasaidia maskini waliomiminika kiamboni mwao kutoka sehumu mbalimbali za eneogatuzi lao vii. Umu anawafunza vijana umuhimu wa kutumia pesa vizuri/ kutofuja pesa. Anatumia pesa alizodunduiza kutokana na masrufu aliyokuwa akipewa na babake kumsaidia ombaomba mmoja mjini Karaha. viii. Rachel Apondi anaonya askari dhidi ya kutatua mizozo kwa makeke na bunduki. Anawaambia kwamba hilo ni jambo ambalo limepitwa na wakati. ix. Dick anawaonya vijana dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya kwa kuiacha biashara hiyo haramu na kufungua biashara halali ya kuuza vifaa vya simu x. Ridhaa anataka jamii inayodhamini masomo. Hii ndiyo sababu anayadhamini masomo ya wapwaze Mzee Kedi. Aidha Dick anaifunza jamii umuhimu wa kuthamini elimu kwani licha ya kukatiziwa masomo na Buda, anapojinasua kutoka mikononi mwake anarudi shuleni kukamilisha masomo yake xi. Ridhaa anataka jamii ambayo raia maskini wanapata matibabu kwa gharama wanayomudu. Hii ndiyo sababu anajenga kituo cha afya cha Mwanzo Mpya ili kiwahudumie raia maskini wasiomudu gharama ya matibabu katika hospitali za kibinafsi na za umma. xii. Kipanga anahimiza msamaha na maridhiano katika jamii. Licha ya kuwachukia na kuwatoroka wazazi wake baada ya aliyemdhania kuwa babake kumkana, anawasamehe wote hatimaye. xiii. Kipanga anionya jamii dhidi ya unywaji pombe haramu kwa kubadilika na kuacha kuinywa baada ya kuwaua watu sabini. xiv. Selume anataka jamii kupuuza mila zinazowakandamiza wanawake. Anamshauri Tuama kuwaelimisha wanafunzi wenzake dhidi ya kufuata mila zilizopitwa na wakati kama vile ukeketaji wa wanawake pg. 70
xv. Madaktari wanahimiza wanajamii kuthamini haki za watoto. Pete anapoenda kuavya mimba ya kitoto chake cha pili anakutana na daktari mwanamume anayekilaani kitendo hicho xvi. Mahakama inaonya dhidi ya ukiukaji wa haki za watoto kwani inawafunga Sauna na Bi. Kangara waliofanya biashara haramu ya kuwateka watoto nyara na kuwauza. xvii. Neema anahimiza jamii kuthamini haki za watoto kwa kumwokoa mtoto aliyetupwa kwenye biwi la taka na kumpeleka kwenye kituo cha mayatima cha Benefactor. xviii. Kangata anataka jamii inayothamini haki za mtoto wa kike. Anawaelimisha wanawe wa kike licha ya jamaa yake kumchochea kwamba kufanya hivyo ni kufisidi rasilmali. xix. Ridhaa anahimiza jamii kuyatunza na kuyahifadhi mazingira kwa kubadilisha eneo lililokuwa jangwa na kuwa na rangi ya chanikiwiti akitumia maji ya mabomba- anapanda miti ambayo imesababisha hata mvua kuanza kunyesha. xx. Dick anataka jamii ambayo vijana wanajitegemea kimaisha. Anafungua duka la kuuza vifaa vya simu na kuwaajiri vijana wengine ili wapate riziki ya kujikimu. xxi. Wazazi wa Rehema wanahimiza jamii kukataa ndoa za mapema. Fumba anampachika mimba mwanao Rehema na kukataa kumwoa lakini wanapinga kitendo hicho kwa kumletea Fumba mtoto na kumrudisha shuleni kusoma. Usaliti Ni hali ya kutenda kinyume cha matarajio ya mtu au jamii. Aidha mtu anaweza kuisaliti nafsi yake kwa kuenda kinyume na hadhi, falsafa au msimamo wake i. Mwanzi anawasaliti raia kwa kukataa kukubali matokeo ya uchaguzi hivyo kusababisha kutokea kwa vita. ii. Naomi anamsaliti mumewe Lunga kwa kumtoroka anapofilisika. Pia anawasaliti wanawe Umu, Dick na Mwaliko kwa kuwahini malezi yake anapotoroka na kuwaacha kulelewa na baba yao pekee iii. Sally anamsaliti mpenziwe Billy kwa kuuvunja uchumba wao akidai kuwa jumba alilolijenga waishi ni duni/kiota hali iliyomfanya Billy kuwachukia wanawake. pg. 71
iv. Sauna anamsaliti Umu kwa kumtenganisha na nduguze Mwaliko na Dick. Anawateka nyara na kutoroka nao, hali inayomwacha Umu katika hali ya taharuki. v. Subira anawasaliti wanawe Lime na Mwanaheri kwa kuwahini malezi yake anapomtoroka mumewe Kaizari, hivyo kuwataabisha mno. vi. Fumba anamsaliti mwanafunzi wake Rehema kwa kumpachika mimba, hivyo kumvurugia masomo yake. vii. Fumba anamsaliti mwanawe Chandachema kwa kumtelekeza kwa nyanyake na kuhamia Uingereza. Hatumi hata pesa za kumtunza licha ya kujiweza kiuchumi. viii. Bwana Tenge anamsaliti mkewe Bi. Kimai kwa kuzini na makahaba ix. Mama Kipanga anmsaliti Kipanga kwa kutomwambia babake mzazi anapomuuliza baada ya aliyemdhania kuwa babake kumkataa- kitendo hiki kinamsababisha Kipanga kutoroka nyumbani kwao na kuanza kunywa pombe. x. Baba mlezi wa Kipanga anamsaliti Kipanga kwa kumkana kuwa mwanawe halisi xi. Mama Pete anamsaliti Pete kwa kumtelekeza kwa nyanyake bila kumtumia mahitaji yake kama sodo. Inambidi kutumia blanketi na kanzu kuukuu. xii. Mama na wajomba wake Pete wanamsaliti Pete kwa kumkatizia masomo yake na kumwoza kwa mzee Fumba ambaye tayari ana wake watatu. xiii. Pete anakisaliti kitoto chake cha pili kwa kunywa vidonge ili kukiavya. xiv. Mzee Maya anamsaliti mwanawe Sauna kwa kumbaka na kumpachika mimba. xv. Baba Kairu anamsaliti Kairu kwa kumzaa nje ya ndoa na kumwacha akitaabika katika hali ya umaskini licha ya kuwa tajiri. xvi. Wazazi wake Zohali wanamsaliti Zohali kwa kumsimanga na kumdhalilisha anpopachikwa mimba badala ya kumpa ushauri nasaha ambao ungesaidia kumrekebisha. xvii. Tenge anawasaliti wanawe pamoja na Chandachema kwa kufanya ukahaba machoni pao. Uwajibikaji Ni hali ya kutenda linalotarajiwa kutendwa. i. Mama Ridhaa anaenda shuleni kuzungumza na mwalimu anaposikia masaibu Ridhaa anayopitia shuleni mikononi mwa wanafunzi wengine. pg. 72
ii. Ridhaa anayadhamini masomo ya wapwawe Mzee Kedi. iii. Ridhaa anahakikisha kwamba kijiji kizima cha Msitu wa Heri kina maji ya mabomba. iv. Mwekevu akiwa mkurugenzi wa shirika la Chemchemi anawasaidia raia kwa kuwachimbia visima vya maji. v. Kaizari anawasihi wakimbizi wenzake kujenga vyoo ili kuzuia maenezi ya kipindupindu. vi. Wataalamu wa ushauri nasaha wanawatembelea wakimbizi kwenye Msitu wa Mamba na kuwapa huduma za ushauri na uelekezaji hivyo kuwasaidia kutatua hali ngumu zilizowakabili. vii. Mwalimu Meli anawafunza wanafunzi umuhimu wa kutopima uwajibikaji wa mtu kwa misingi ya kijinsia. Wote waume na wake, wapewe nafasi sawa. viii. Jamii ya kimataifa iliingilia kati na kurejesha amani katika taifa la Wahafidhina baada ya machafuko ya kisiasa. ix. Lunga Kiriri Kangata anawaelimisha wakulima kuhusu mbinu bora za kilimo baada ya kusomea kilimo. x. Pete anapoenda kuavya mimba ya kitoto chake cha pili anakatazwa na daktari ambaye tena anakilaani kitendo hicho. xi. Polisi wanawajibika kwa kuwatia mbaroni Bi. Kangara na Sauna kwa kufanya biashara haramu ya kuwateka watoto nyara na kuwauza. xii. Ridhaa anajenga kituo cha afya cha Mwanzo Mpya katika ardhi yake ili kiwafae raia maskini wasioweza kumudu gharama ya matibabu katika hospitali za kibinafsi na hata za umma. xiii. Neema alikiokota kitoto kilichokuwa kimetupwa kwenye biwi la taka akielekea kazini na kukipeleka katika kituo cha polisi. xiv. Umu alipoamka na kuwakosa nduguze wadogo- Dick na Mwaliko aliwatafuta na kupiga ripoti katika kituo cha polisi ili asaidiwe kuwasaka. xv. Serikali inawaokoa vijana ombaomba mjini Karaha kama vile Hazina kwa kuwajengea makao, kuwapeleka shuleni na kuwashauri kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto za maisha. pg. 73
xvi. Mtawa Pacha anamrudisha Zohali shuleni baada ya kupachikwa mimba na kukatiza masomo yake. xvii. Wanawake wajane wanaanzisha makao ya watoto mayatima ya Jeshi la Wajane wa Kristu ili kuwasaidia mayatima, watoto waliotupwa na mama zao na wale wenye wazazi/walezi wahitaji. xviii. Baada ya kuacha biashara haramu ya kulangua dawa za kulevya, Dick anaanzisha biashara ya kuuza vifaa vya umeme ili kujikimu kimaisha kwa njia halali. xix. Dick anajielimisha mwenyewe kutokana na pesa alizodunduiza wakati wa ulanguzi wa dawa za kulevya na baada ya kujitegemea anasomea Teknolojia na Mawasiliano ya Simu. xx. Wasamaria wema wanampeleka Lemi hospitalini baada ya kuchomwa kwa kudhaniwa kuiba simu. xxi. Kituo cha afya cha Mwanzo Mpya kinatoa ushauri nasaha kwa walevi kama Kipanga ili kubadilisha hali yao ya ulevi. xxii. Nyanyake Pete anapinga ndoa ya lazima iliyomkatizia Pete masomo Mbinu za Kimtindo na Kimuundo Kejeli/stihizai/dhihaka Tamathali hii huhusiana mno na kinaya. Mwandishi hutumia maneno ya kinyume yanayonuiwa kumchoma, kumdharau/ kumdunisha na kumcheka mtu. Wakati mwingine dhihaka huenda isiwe na kinyume lakini mwandishi au msemaji atumie neno linalomuumiza mhusika. Kejeli huweza kutokea wakati unamsifu mtu kiongo kwa nia ya kutaka kumuumiza. I. Terry anamdhihaki mumewe Ridhaa kwa kumwambia kuwa anashangaa jinsi daktari mzima kama yeye anavyojishughulisha na mambo ya ushirikina (uk.2). Hapa mwandishi anafanyia tashtiti licha ya kuwa msomi. II. Sally analikejeli kasri alilojengewa na mchumbaye Billy kwa kulifananisha na kiota (uk 80) III. Kauli ya Zohali kwamba wazazi wake ni walezi wema ni kejeli kwa maana wazazi hao wanamsimanga na kumdhalilisha anapopachikwa mimba na kumsababisha kutoroka nyumbani. (uk. 98) Ukosefu wa uwajibikaji wa wazazi hawa unakejeliwa. pg. 74
IV. Tila analikejeli taifa lake kwa kulifananisha na mtoto wa miaka hamsini. (uk. 6) Hapa mwandishi analidhihaki taifa hilo kwa kutopata maendeleo licha ya kuwa huru kwa miaka hamsini. Wanafunzi wanamkejeli Ridhaa shuleni kwa kumwita (Mfuata Mvua' kwa sababu ya kuwa mwanafunzi mlowezi. Hapa athari za ukabila zinachimuzwa. (uk. 10) V. Kaizari anamkejeli aliyekuwa Waziri wa Fedha kwa kueleza jinsi anavyong'ang'ania uji naye kwenye kambi ya wakimbizi. (uk. 15) Dhiki za wakimbizi zinadokezwa. VI. Mavyaa wake Subira anamdhihaki Subira kwa kumwita 'Muki' kwa sababu ya kutoka jamii ya Bamwezi. Hapa suala la athari za ukabila linachimuzwa. (uk. 94) VII. Mwandishi anamkejeli Tuama kwa kumfanya kuusifu ukeketaji wa wasichana ambao umewaua wasichana wenzake. Kukengeuka kwa Tuama kunakashifivva. (uk.144) VIII. Pete anamkejeli Fungo kwa kuusuta unene na kutuzi aliyonuka. (uk. 149) Hali ya Pete kutompenda Fungo inadokezwa. IX. Pete anapotaka kuhama nyumbani kwa Fungo, Fungo anamdhihaki kwa kumwambia aondoke kwa maana kuwepo kwake hakuzidishi hakupunguzi. (uk. 149) Usaliti wa Fungo unadokezwa. X. Lunga anajikejeli kwa kuwaonya wenzake dhidi ya kuharibu mazingira ilhali babake analowea katika shamba lililokuwa msitu hapo Unafiki wa Lunga unasutwa. XI. Wafuasi wa Mwanzi wanamkejeli Mwekevu kwa kudai kwamba hawezi kushinda kura isipokuwa kwa kuiba au kuwahonga wapiga kura. Ukandamizaji wa iwanamke unabainishwa. XII. Wanaume wanamdhiaki Mwekevu kwa kumtusi na kumtisha anapojitosa siasani. Taasubi ya kiume inashtumiwa. XIII. Mwandishi anamkejeli Bwana Tenge kwa kumfanya kuzini na XIV. makahaba ilhali ana mke Bi. Kimai. XV. Polisi wanamkejeli Umu anapoenda kuripoti kuhusu kupotea kwa nduguze kwa kumuuliza mbona watoto wenyewe hawajaandikisha kupotea kwao kwenye OB. Udhalimu wa polisi unachimuzwa. (uk. 83) pg. 75
Kinaya Kinaya ni tamathali ya usemi ambayo msemaji/ mwandishi hutoa kauli ambayo ni kinyume na anachomaanisha. Pia kinaya hujitokeza mhusika anapotenda kinyume cha anachotarajiwa kufanya. Kinaya hutumiwa kukashifu matendo fulani. I. Sally analiita kasri alilojengewa na Billy kiota. II. Lunga anajisabilia kwa hali na kumpendeza mkewe Naomi lakini Naomi anaivunja ndoa yao kwa kumtoroka. Usaliti wa Naomi unajitokeza. III. Umu anapoenda katika kituo cha polisi kuripoti kuhusu kupotea kwa nduguze askari wanamuuliza kwa nini watoto wenyewe hawajaandikisha kupotea kwao kwenye OB. Hapa ukatili wa polisi unasisitizwa. IV. Ni kinaya wavuvi kukatazwa kuvua katika Ziwa Kuu kwa madai kuwa japo ardhi ambayo ziwa limesimama ni yao, maji ya ziwa si yao. V. Ni kinaya Subira kuitwa mwizi wa mayai ambayo kuku wenyewe watagao amewafuga yeye. VI. Zohali anadai kwamba wazazi wake ni walezi wema ilhali wanamsimanga na kumdhalilisha anapopachikwa mimba. Ukatili wa wazazi hawa unakejeliwa. VII. Fumba anamwachia mamake mzazi malezi ya mwanawe, Chandachema bila kumtumia hela za mahitaji yake. Ukosefu wa uwajibikaji wa Fumba unashtumiwa. VIII. Lunga anawarai wenzake shuleni kutunza mazingira ilhali babake ndiye anayeuharibu msitu kwa kuendeleza kilimo huko. Unafiki wa Lunga unakejeliwa. IX. Viongozi wanajenga nyumba katika ardhi iliyotengewa upanzi wa chakula kisha wanaanza kuharibu msitu ill kupata mahali pa kupanda chakula. Hapa ukosefu wa uwajibikaji wa viongozi unadhihakiwa. X. Mzungu amewajengea wafanyakazi kituo cha afya lakini wanao wanapougua na kuenda kutafuta matibabu huko madaktari waafrika wanakataa kuwatibu kwa madai kwamba kampuni hiyo haina mpango wa matibabu kwa wafanyakazi vibarua. Ukatili wa madaktari unachimuzwa. XI. Ni kinaya mwana wa kibarua kunyimwa matibabu katika kituo cha afya kwa madai kwamba kampuni haina mpango wa matibabu kwa wafanyikazi vibarua ilhali wafanyikazi vibarua pg. 76
XII. ndio wanaozalisha mali ya kuwezesha kuwepo kwa huo mpango wa matibabu. Hali hii inatuonyesha ukatili wa madaktari katika kituo hiki cha afya. XIII. Wataalamu wa masuala ya lishe wanaitikia shinikizo la vigogo na kutia sahihi kuidhinisha uuzaji wa mahindi yaliyokuwa hatari kwa afya ya binadamu. Ukosefu wa uwajibikaji wa XIV. wataalamu hawa unafanyiwa tashtiti. XV. Lunga anapopinga kitendo cha raia kuuziwa mahindi yaliyokuwa hatari kwa afya yao, XVI. anaambiwa kwamba kuyakataa mahindi hayo ni kama kuidhinisha kifo cha mamilioni ya raia ambao hawamudu kununua hata kibaba cha unga ilhali kuwauzia mahindi hayo ndiko XVII. kuidhinisha kifo chao. Ukiukaji wa haki za binadamu unakejeliwa. Ni kinaya mkurugenzi wa Kitengo cha Uhakikishaji wa Viwango na Ubora wa Bidhaa kuacha XVIII. raia kuuziwa mahindi ambayo yameharibika. Ukosefu wa uwajibikaji unajitokeza. XIX. Akiwa shuleni Lunga anawahimiza wanafunzi na walimu kupanda mti iwapo wamekata XX. mmoja lakini yeye anakata miti katika Msitu wa Mamba bila kupanda mingine. XXI. Lunga anapoachishwa kazi na kufukuzwa kwenye nyumba ya kampuni kwa sababu ya kupinga raia kuuziwa mahindi yaliyoharibika, wale aliowatetea hawakumsaidia- wapo wale waliosema kwamba huo ulikuwa msiba wa kujitakia. Ingawa raia walitangaziwa kwamba Msitu wa Mamba ulikuwa marufuku kwa binadamu, usiku wa manane husikika milio ya malori na matrekta yakibeba shehena za mbao, makaa na mahindi. Majumba katika mtaa wa Zari yanabomolewa kwa shughuli dharura ya kujenga bypass ili kupunguza msongamano wa magaribkwenye barabara kuu lakini ujenzi huo haufanyiki. Mwangeka anaenda kudumisha amani kwingine na mkewe kufa kutokana na ukosefu wa usalama nchini mwao. Fedha zinazotokana an uchimbaji madini katika taifa la Wahafidhina zinaishia kwenye mifuko ya wageni, hivyo kuwaacha wenyeji wakitaabika. Ukoloni mamboleo unakashifiwa. Ridhaa anamsaidia Mzee Kedi kwa kuyadhamini masomo ya wapwaze wawili lakini Mzee Kedi anamlipa ubaya kwa fadhila anaichoma familia yake Ridhaa. Ukatili wa Kedi unakashifiwa. pg. 77
XXII. Mwekevu anapojitosa siasani anatengwa hata na wanawake wenzake waliostahili kumsaidia XXIII. kukwea uongozini. XXIV. Ni kinaya wafuasi wa Mwekevu na Mwanzi kuzozana baada ya uchaguzi ilhali wanaozozania (Mwekevu na Mwanzi) wako majumbani mwao wakitazama runinga. XXV. Lunga anawakataza wanawe kushika tama akisema kwamba kushika tama ni kukaribisha umaskini na ukiwa ilhall yeye alishinda akishika tama baada ya kutorokwa na mkewe Naomi. (Uk. 168) Familia ya akina Mwangeka wana msala lakini wanaenda haja zao vichakani- kama wenzao vijijini. (Uk. 180) Hali ya uchafuzi wa mazingira inakashifiwa. Chuku Hii ni mbinu ya kuongeza yasiyo ya kweli ili kutilia mkazo jambo na kuipa mvuto kazi ya kifasihi. I. Mwandishi anatia chuku anaposema kwamba mahindi yaliyokuwa yameagizwa kutoka ughaibuni kwa matumizi ya binadamu yalikuwa hatari hata kwa usalama wa panya: ,(uk. 70- 71) Hapa anasisitiza madhara ambayo yangetokea iwapo binadamu wangeyala mahindi hayo. II. Tunaambiwa kwamba 'akina mama waliomlilia Dede baada ya kufariki dunia walivishikilia vichwa vyao kana kwamba wanahofia kuwa vitaanguka. (Uk. 59) Hapa mwandishi anasisitiza huzuni iliyowagubika kutokana na kifo cha Dede. III. Umbali uliokuwa baina ya Mwangeka na Ridhaa ulikuwa hatua tatu tu lakini mwandishi anatia chuku kwa kusema kwamba ulionekana kama bahari ya Shamu. (uk.46) IV. Babake Mwangeka anatia chuku anaposema kwamba yeye huwafufua maiti katika chumba cha wagonjwa mahututi. Anafanya hivi ili kusisitiza ubingwa wake katika udaktari. (uk 181) V. Mwandishi anatia chuku anaposema kwamba usiahi wa Mwangeka ungeporomosha paa la jiko la mamake. Hapa anaonyesha kilio cha Mwangeka baada ya kuchapwa na babu. (Uk. 188) VI. Mwandishi anatia chuku anaposema kwamba Lunga alihisi kama aliyechomwa kwa joto la tanuri baada ya kuusoma ujumbe wa mkewe kwenye rununu yake. Mwandishi anasisitiza iinsi kuondoka kwa Naomi kulivyomuathiri. (uk. 81) pg. 78
VII. Mwandishi anatia chuku anaposema kwamba moyo wa Lunga ulipiga mithili ya ngoma baada ya kugundua kwamba mkewe hayumo kitandani. (uk. 81) Hapa mwandishi anasisitiza woga wa Lunga. Sitiari Huu ni ulinganishi wa vitu viwili au zaidi bila kutumia vihusishi wala vilinganishi. (i) Mamake Ridhaa anawalinganisha wanaume na majimbi/ wanawake na makoo kuonyesha jinsi mtazamo wa jamii kuwahusu wanaume na wanawake. (uk. 2) Vikaratasi vilisambazwa kila mahali vikiwatahadharisha watu kuhusu gharika baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya. (uk. 12) Gharika ni sitiari/ jazanda ya vita/ghasia/ fujo ambazo zingetokea baada ya kiongozi mpya kutawazwa. (iii) Sauna anafananishwa moja kwa moja na chui kuonyesha ukatili wake - kuwaiba watoto. (uk. 84) (iv) Umu anapoliangalia jiji la Karaha, analiona kama bahari isiyo na kikomo. Bahari ni sitiari ya mahali ambapo Umu anataka kuishi bila kujua hatari zake. (uk. 85) (v) Urnu anapokutana na Hazina akiwa ombaomba mjini Karaha anamwona kama gae kuonyesha dharau ya Umu dhidi yake. (uk. 88) (vi) Mavyaa wake Subira anamlinganisha Subira na gugu ambalo linautia najisi utambulisho wao, kuonyesha ukabila wa mavyaa. (uk.94) (vii) Mshahara wanaolipwa wasomi nchini Wahafidhina unafananishwa na mkia wa mbuzi ili kusisitiza mshahara duni wanaolipwa wasomi. (uk. 65) (viii) Misitu inaharibiwa na viongozi wenye mate ya fisi. (uk.68) Mate ya fisi ni sitiari ya tamaa ya viongozi katika kumiliki rasilmali. (ix) Lunga anafananisha mahindi yaliyoharibika na sumu (Uk.71) kuonyesha jinsi yalivyokuwa hatari kwa afya ya raia. (x) Ridhaa anafananisha uhamisho wao kutoka Msitu wa Mamba kuenda nyumbani kwao kama kutoka Kanaani kwenda Misri kuonyesha kuwa maisha kambini yalikuwa mazuri kuliko nyumbani wanakopelekwa. (uk. 34) pg. 79
(xi) Tila anasema kwamba wapiga kura wameamua kujaribu mbinu mpya za kilimo kwa maana matumizi ya visagalima yameanza kupitwa na wakati. (Uk. 40). Kujaribu mbinu mpya za kilimo ni sitiari ya kuwajaribu viongozi wapya. Visagalima ni sitiari ya viongozi ambao wamekuwa uongozini kwa muda mrefu. (xii) Tila anasema kwamba wanataka kiongozi atakayeweza kulielekeza jahazi lao kwenye visiwa vya hazina. (uk. 40) Jahazi ni sitiari ya taifa la Wahafidhina. Visiwa vya hazina ni sitiari ya maendeleo. (xiii) Tila anamuuliza babake iwapo amewahi kumwona mtoto wa miaka hamsini ambaye hajasota wala kusimama dede. (uk. 5) Mtoto wa miaka hamsini ni sitiari ya taifa la Wahafidhina na kutosota/kutosimama dede ni sitiari kutoendelea kiuchumi. (xiv) Wakimbizi wanamrushia askari makombora ya matusi kuonyesha upyoro wa wakimbizi. (Uk.33) (xv) Mwaliko anawaambia polisi kwamba babake alienda kwa Mungu. (uk. 158) Kuenda kwa Mungu ni sitiari ya kufariki dunia. (xvi) Mama Sauna anamrai Sauna kutompaka Mzee Maya tope baada ya kumbaka. (uk. 155) Tope ni sitiari/jazanda ya kumharibia jina kwa kuufichua uovu wake. Chandachema anasema kwamba nyota yake ilizimika baada ya kifo cha nyanyake. Kuzimikika kwa nyota ni sitiari/jazanda ya kuharibika kwa maisha. (uk. 102) Majazi Mwanaheri Heri ni wema/uzuri. Mwanaheri anatendewa wema anapotibiwa katika kambi ya wakimbizi baada ya kubakwa Kangata Kangata ni kushikilia jambo hadi lifanyike. Jina hili linamwafiki kwani licha ya ukoo wake kupinga mwanawe kuolewa katika ukoo wa Waombwe, anashikilia msimamo wake hadi Lucia anaolewa huko/pia licha ya jamaa zake kupinga masomo ya wanawe wa kike, yeye anawapuuza na kuwasomesha. Kaizari pg. 80
Jina hili lina maana ya kiongozi. Jina hili linamwafiki kwani akiwa katika kambi ya wakimbizi aliwaongoza wenzake kuchimba misala ili kuepuka kuenea kwa kipindupindu. Aidha, anateuliwa kuwa miongoni mwa watu wanaoongoza ugavi wa chakula kwa wakimbizi. Lunga Kulunga ni kufuata/kuandama. Jina hili linamwafiki kwani anafuata nyendo za babake aliyelowea kwenye ardhi iliyokuwa msitu awali kwa kufyeka Msitu wa Mamba na kulowea huko akiendeleza ukulima. Hazina Hazina ni kitu cha thamani. Anakuwa wa thamani kwa Umu.Anamsaidia Umu anapojikuta mjini Karaha Maisha yakiwa yamemharibikia. Tenge Lina maana ya hali isiyopendeza/ kombo. Tabia zake ni kombo kwa maana anafanya mapenzi na makahaba licha ya kuwa na mke Bi. Kimai. Nasibu Lina maana ya jambo linalotokea bila kutarajiwa au kibahati tu. Jina hili linamwafiki kwani anazaliwa bila kutarajiwa. Anazaliwa baada ya mamake kujihusisha na mapenzi akiwa kidato cha pili. Wahafidhina Maana yake ni watu wanaopenda kushikilia mambo ya kale/watu wasiopenda mabadiliko. Jina hili linaafiki mahali hapa kwani raia wa taifa la Wahafidhina hawataki kiongozi mwanamke kushika hatamu za uongozi aidha hawataki kuachilia mila ya kuwakeketa wasichana vilevile hawataki mwanamke kuelimishwa n.k. Kimbaumbau, Ni mtu anayebadilisha kauli yake kila wakati. Jina hili linamwafiki kwani alikubaliana na Naomi kumfanyia biashara kisha baadaye akabadilika na kumtaka mapenzi. Maya ni hali ya kutopenda. Jina hill linamwafiki kwani anambaka Tendakazi Lina maana ya kufanya kazi. Jina hili linamwafiki kwani akiwa mkurugenzi wa Shirika la Chemchemi anawachimbia raia visima vya maji. pg. 81
Msitu wa Heri Hii ni ardhi iliyokuwa na rotuba. Bwana Lunga-Kiriri Kangata aliweka makazi yake hapa akajikuta heri imemwangukia kutokana na kufaidi mazao ya kilimo. Hata hivyo, kitumbua kiliingia mchanga walipofurushwa kwa madai kwamba wanaishi hapo kiharamu. Methali I. Liandikwalo ndilo liwalo (uk. 2) kumaanisha kwamba Ridhaa hana uwezo wa kubadilisha alilolipanga Mungu. II. Ng'ombe akivunjika mguu malishoni hujikokota zizini kusaidiwa (uk.100) kuonyesha jinsi Zohali alivyorudi nyumbani akitarajia kwamba wazazi wake watamsaidia baada ya kufukuzwa shuleni kwa sababu ya mimba. III. Teke la kuku halimuuzi mwanawe (uk 100) Kuonyesha jinsi Zohali alivyodhani kwamba wazazi wake hawatamdhuru baada ya kufukuzwa shuleni kwa sababu ya mimba. IV. Akufukuzaye hakwambii toka. (uk. 103) Chandachema anatoka nyumbani mwa Satua baada ya Satua kuanza kulalamikia kuisha haraka kwa sukari na matumizi mabaya ya sabuni. V. Wino wa Mungu haufutiki. (uk. 53) Hakuna lolote ambalo Mwan'geka angetenda baada ya familia yake kuchomewa ndani ya nyumba. VI. Dalili ya mvua ni mawingu. (uk. 40) Kumaanisha kulikuwa na dalili za kuchaguliwa kwa kiongozi mpya katika taifa la Wahafidhina. VII. Simba akikosa nyama hula nyasi (uk. 16) kumaanisha kwamba Ridhaa anakula mizizi mwitu baada ya kukosa chakula. VIII. Msafiri kafiri (uk. 16) kumaanisha kwamba ilimbidi Ridhaa kula mizizimwitu kwa maana yu katika kambi ya wakimbizi ambapo hakuna chakula. pg. 82
MBINU REJESHI. i) Ridhaa anakumbuka mlipuko na kilio cha mkewe. ii) Ridha anakumbuka milio ya kereng’ende na bundi. iii) Anakumbuka jinsi watoto walivyo mtenga shuleni anakumbuka majumba yake yanavyobomolea. iv) Anakumbuka mjadala aliokuwa akifanya na mwanawe Tila. v) Mwangeka anakumbuka mafunzo ya dini. vi) Kaizari anasimulia ridhaa jinsi familia yake ilivyovamiwa. vii) Mwanaheri anakumbuka kwenda kwa mamake kupitia kwa barua. viii) Mwangeka anakumbuka maisha yake na Mwangemi utotoni. ix) Kijana aliyekuwa amevaa sharti ambalo lilikuwa limeandikwa Hitman anaeleza jinsi aliwandanganya vikongwe kumchagua kiboko ambaye hawakumtaka. (zozote 5x1) Kweli kinzani -Tila kusema kuhusu mtoto wa miaka hamsini na hakuna mtoto mwenye umri wa miaka hamsini -Mwangeka alienda kulinda usalama mataifa mengine na kwao hakuna usalama -Wanakijiji walimwona Ridhaa kama mgeni na yeye ndiye alipabadilisha mahali hapo pa msitu wa heri. -Viongozi wananchi wanawapeleka watoto wao kusomea ng’ambo -Wana wa kiriri walikataa kurudi kwao -Annette alimnyima ushirika wa watoto wake -Naomi kutoroka na kuwaacha watoto ambao wanahuhitaji mkubwa wa mzazi wa kike -Mavyaa wa Subira anamwona subira kama muki -Wanakijiji walisababisha mauko ya Lemi na hakuwa na makosa -Tuama kumuasi babake kwa kujificha kwenda kupashwa tohara pg. 83
Taswira Taswira ni picha ambazo husawiriwa mawazoni mwa msomaji anaposoma kazi fulani ya kifasihi. I. Maelezo kuhusu watu wanaouliwa na walinda usalama baada ya ghasia za baada ya uchaguzi (uk. 19), inatusawiria ukatili wa walinda usalama. . ‘. r II. Tunachorewa picha ya kijana mwenye shati lililoandikwa ‘Hitman’ akiyachoma magari barabarani pamoja na walimo (uki 21) Tunapata picha ya mtu ambaye ni katili. III. Maelezo kuhusu namna wanawe Kaizari walivyobakwa (uk, 25) yanatusawiria udhalimu wa wahusika. IV. Maelezo kuhusu wakimbizi wakiwa msituni bila chakula (uk. 27) inatupa picha ya dhiki za wakimbizi. V. Maelezo kuhusu watoto wanaoenda haja kwenye reli katika mtaa wa Sombera (uk. 29), inatusawiria picha ya uchafuzi wa mazingira. VI. Maelezo kuhusu raia wanaochomeka wanapoenda kuiba mafuta ya lori lililoanguka (uk- 55) inaibua picha ya huzuni kwa hawa wanaochomeka. VII. Tunachorewa picha ya vijana ombaomba mjini Karaha (uk. 86). Picha hii inasawiri uhitaji wao. VIII. Maelezo kuhusu Tindi akisakata midundo(uk121) yanatusawiria picha ya msichana mpenda anasa IX. Maelezo kuhusu kuchomwa kwa Lemi (uk 122) yanatuonyesha ukatili wa raia dhidi ya binadamu wenzao. Mbinu za kimuundo Sadfa. Hii ni mbinu ya lugha ambapo mambo mawili hutokea wakati mmoja kana kwamba yalikuwa yamepangwa kutokea hivyo. I. Ridhaa anahofia kwamba milio ya bundi nyumbani kwake iliashiria kutokea kwa jambo fulani. Na ikatokea jinsi hofu yake ilivyomwelekeza - Mzee Kedi anaichoma familia yake pamoja na nyumba yake. pg. 84
II. Inasadifu kwamba majumba yote ya Ridhaa yaliyobomolewa katika mitaa ya Zari na Tononokeni yalikuwa yamejengwa katika ardhi iliyodaiwa kutengwa kwa ujenzi wa barabara. (uk.13) III. Umu anapoenda mjini Karaha akiwa hana mbele wala nyuma, anaanza kumtafuta kijana mmoja (Hazina) aliyemsaidia wakati fulani kwa kumpa pesa na inasadifu kwamba wanakutana Umu anapata msaada alioutaka. IV. Marehemu Mandu, mumewe Rachael Apondi alikuwa askari. Anapokufa, Apondi anaolewa tena na askari, Mwangeka. V. Mwangeka na Apondi wanakutana wote wakiwa wamefiwa wapenzi wao na kuanzisha uchumba ulioishia kufunga ndoa. VI. Inasadifu kwamba siku ambayo Dick anasafiri kuelekea ughaibuni ndiyo siku Umu anasafiri kuelekea huko na kukutana baada ya kupoteleana kwa siku nyingi. VII. Inasadifu kwamba wakati Dick alipokuwa akiwaza kuhusu dadake Umu, Umu naye alikuwa akiwaza na wote walikuwa katika uwanja wa ndege kusafiri kuelekea ughaibuni. VIII. Inasadifu kwamba wakati Selume anapowazia kustaafu ndipo Ridhaa anapofungua kituo cha afya cha Mwanzo Mpya na kumuajiri. IX. Inasadifu kwamba Pete anapotaka kuvunja uhusiano wake na Mzee Fungo, Mzee Fungo anamwambia aondoke na mwanawe kwa maana kuwepo kwake huko hakuzidishi hakupunguzi. X. lnasadifu kwamba nduguze Mwaliko ambao amekuwa akiwatafuta wamo kwenye mkahawa alimokuwa na Mwangemi wanakutana. XI. Inasadifu kwamba Mwangemi na Umu wanasherehekea siku yao ya kuzaliwa kwenye hoteli moja ya Majaliwa. XII. lnasadifu kwamba Mwangemi na Umu wamezaliwa siku moja. XIII. Ni sadfa mabinamu kuwalea watoto wamoja. Mwangemi anamlea Mwaliko huku Mwangeka akiwalea nduguze Mwaliko Umu na Dick. XIV. Ni sadfa Umu na Mwanaheri kukutana wote wakiwa wametorokwa na mama zao. XV. Ni sadfa Ridhaa kukutana na dadake kwenye kambi ya wakimbizi wote wakiwa wameathiriwa na ghasia za baada ya uchaguzi. pg. 85
XVI. lnasadifu kwamba mmoja wa wafuasi wa Mwanzi waliowachomea raia ndani ya magari alikuwa amevaa shati lenye maandishi 'Hitman' kwa maana ya muuaji. (uk.21) XVII. Inasadifu kwamba siku Ridhaa alikuwa ameenda kumtibu mgonjwa aliyejeruhiwa katika maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi ndiyo siku familia yake inachomwa. Barua Barua ya kustaafishwa kwa Lunga. (uk. 72) Barua hii inaufanyia tashtiti uozo uliopo katika Shirika la Maghala ya Fanaka. Lunga anaachishwa Kazi kwa kuitenda kazi yake inavyostahili - kupinga raia kuuziwa mahindi yaliyoharibika. Barua ya Subira kwa mwanawe Subira (uk. 95 - 96) Barua hii inadhihirisha: a. Chanzo cha Subira kuivunja ndoa yake. Subira anafitiniwa, anabaguliwa, analaumiwa na kusingiziwa wizi wa mayai kwa sababu ya kutoka katika jamii ya Bamwezi. b. Ukatili wa Mama Kaizari. Anamdhulumu Subira kwa kupigania mapenzi ya Kaizari c. Ukosefu wa uwajibikaji wa Kaizari. Anampagaza Subira machungu kwa kumsababisha kupigania penzi lake na mavyaa wake Ujumbe anaotuma Naomi kwa mumewe Lunga (uk.81) ujumbe huu: a. Unadokeza usaliti wa Naomi. Anaondoka na kuiachia familia yake majonzi. b. Unaonyesha kuvunjika kwa ndoa baina ya Naomi na Lunga. Nyimbo I. Kuna wimbo unaoimbwa na wafuasi wa Mwanzi (uk 20) Wimbo huu unadokeza taasubi ya kiume miongoni mwa wafuasi wa Mwanzi.Wanakataa kukubali ushinde na kuanza kuimba nyimbo za Mwanzi kumhimiza kutawala Wahafidhina licha ya kwamba alikuwa ameshindwa na Mwekevu. II. Wimbo wa mamake Mwangeka (uk. 49) Wimbo huu unaendeleza maudhui ya dini III. Wimbo wa akina Mwangeka wakiigiza mazishi ya Dede (uk 60) wimbo huu unachimuza majonzi ya akina Mwangeka na Tila kwa kufiwa ndugu yao mpendwa Dede. IV. Wimbo unaoimbwa na ndege. (uk 187) unaoendeleza maudhui ya dini V. Wimbo wa Shamsi (uk. 129). Wimbo huu: pg. 86
a. Unadokeza athari za ulevi kwani Shamsi anatoka ulevini usiku wa manane na kuimba wimbo huu unaowaghasi waliolala b. Unadokeza maudhui ya unyakuzi wa ardhi. Bwana Mabavu anawapoka akina Shamsi shamba. c. Unachimuza suala la ufisadi. Bwana Mabavu anawapoka akina Shamsi shamba akitumia hatimiliki bandia. Ajira zinatolewa pia kulingana na jinsi unavyojulikana. d. Unawakosoa raia kwa kutopigania haki zao wanapodhulumiwa na wenye nguvu. kina Shamsi wanapokwa ardhi bila kulalamika. e. Unadokeza kuwa Shamsi ni msomi. Amesoma hadi chuo kikuu. f. Unabainisha dhuluma dhidi ya wasomi. Shamsi amesoma ila ananyimwa ajira. Wakipata wanalipwa ujira duni. Wanafutwa kazi katika kampuni wanazofanyia kazi wanapoomba kupandishwa vyeo. g. Unadokeza athari za ukosefu wa chakula. Babake Shamsi anakufa kutokana na njaa anakula mizizi mwitu kutokana na ukosefu wa chakula. h. Unadokeza kudhoofika kwa asasi za umma. Hospitali katika vijiji vya walalahoi hazina dawa n.k. VI. Wimbo wa Ridhaa (uk 136-137) wimbo huu unaonyesha ukatili wa wanaopika pombe. Wanatia vijasumu ili iive haraka hivyo kuishia kuua na kupofusha walevi. Hotuba Hotuba ya Lunga kwa wanafunzi na walimu akiwa shuleni. (uk. 68-69) Hotuba hii: I. Inadokeza maudhui ya ukiukaji wa haki za wanyama. Misitu imeharibiwa hivyo kuwaacha wanyama bila makao ya kuishi. II. Inadokeza suala la uharibifu wa misitu. Viongozi wanakata miti iii kujenga viwanda na kuendeleza kilimo cha michai. III. Inawakejeli viongozi wasiowajibika. Viongozi wanajenga kwenye ardhi iliyotengewa upanzi wa chakula, hivyo kulihini taifa chakula. IV. lnachimuza tamaa ya viongozi. Viongozi wamenyakua hata madhabahu kwenye Mlima wa Nasibu ili kujenga hoteli kubwa za kitalii. pg. 87
Hotuba ya Apondi kwa askari. (uk112 - 114) Hotuba hii ina umuhimu ufuatao: I. lnahimiza askari kuwajibika katika kudumisha usalama. Anawaambia askari kwamba kila mmoja ana jukumu la kudumisha usalama. II. Inasuta askari wanaotatua mizozo midogo kwa makeke na bunduki. Anawaambia kwamba hilo ni jambo ambalo limepitwa na wakati. III. Inawatahadharisha askari dhidi ya mauaji ya raia wasio na hatia. IV. lnawaonya walinda usalama dhidi ya kuchelewa kufika pahali panapotokea mkasa/inakashifu ukosefu wa uwajibikaji wa walinda usalama - kuchelewa kufika mahali ambapo pametokea maafa. V. Inachimuza uozo uliopo miongoni mwa walinda usalama. Wanashirikiana na wahalifu kisha wanagawana mali ambazo zimeibwa. VI. Inadokeza suala la ufisadi. lnawakashifu walinda usalama kwa kuyaacha magari mabovu barabarani kwa sababu wenye magari ni miamba isiyogusika. . . VII. Inawahimiza walinda usalama kuwajibikia kazi zao. Inawahimiza kuwapeleka wahalifu mahakamani na kushtakiwa kabla hawajapewa adhabu yoyote VIII. Inamsawiri Apondi kama mtetezi wa haki za binadamu. Anavikashifu vitendo vya walinda usalama vinavyokiuka haki za binadamu. IX. Ni kichocheo cha uhusiano baina ya Apondi na Mwangeka. Dayolojia Dayolojia za wahusika ni mazunguzo kati ya wahusika wa kazi ya kifasihi. Mazunguzo haya hutumiwa kuendeleza maudhui mbalimbali, kubainisha migogoro kati ya wahusika, kudhihirisha tabia za wahusika na kubadilisha mtindo wa masimulizi na kuikinga kazi dhidi ya kuwachosha wasomaji. Kuna dayolojia baina ya Ridhaa na Tila (uk 38-44). Dayolojia hii: pg. 88
I. Inaendeleza maudhui ya mabadiliko katika jamii. Meko anaifunza jamii kuacha kupima uwajibikaji wa mtu kwa misingi ya kijinsia na badala yake wake kwa waume wapewe nafasi sawa. II. Inachimuza suala la siasa nchini Wahafidhina.Kura ya maoni inaonyesha kwamba Mwekevu anaongoza kwa asilimia 65 dhidi ya mpinzani wake mwenye asilimia 35. III. Inadokeza maudhui ya ubaguzi. Jamii inaamini kwamba mtoto wa kiume ndiye anayestahili kurithi mali ya wazazi wake. (uk. 39) IV. Inaendeleza maudhui ya ujenzi wa jamii mpya. Tila anataka raia kimchagua kiongozi atakayewaletea maendeleo bila kuzingatia jinsia yake. · V. Inachimuza maudhui ya umaskini. Ipo asilimia kubwa ambayo haimudu gharama ya matibabu ya kimsingi aidha watoto wengi wanakufa kutokana na ukosefu wa lishe bora. VI. lnadokeza dhiki za raia wanaoishi kwenye maeneo kame mashambani. Hawamudu kula mara mbili kwa siku aidha wanafanya kazi ya mshahara duni pia bwawa la Fanisi wanalotegemea kwa maji limekauka baada ya kiwango cha maji kushuka. VII. lnawakejeli viongozi wanaowasambazia wakaazi wa mashambani umeme badala ya maji ambayo hawana. VIII. Inachimuza suala la ukoloni mamboleo kwani wazungu ndio wanaochimba madini nchini Wahafidhina hivyo kuishia kuwafaidi wazungu badala ya wenyeji. Kiangaza mbele au kiona mbele I. Ridhaa anamwambia mkewe Terry kuna jambo fulani litakalotokea kutokana na milio ya kereng'ende na bundi. Hatimaye familia yake inachomewa ndani ya nyumba. (uk. 2/3) II. Vikaratasi vilisambazwa vikiwatahadharisha watu kuhusu gharika (vita) ambayo vingetokea baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya. (Uk.12) Vita hivyo vinatokea na kusababisha maafa makubwa. III. Neema anashinda akimkumbusha Mwaliko kuwa siku moja atawaona nduguze. (uk. 169) Hatimaye anakuja kukutana nao kwenye hoteli ya Majaliwa. (Uk. 189) pg. 89
IV. Dhahabu anamwambia Umu kwamba Mwangeka na Apondi ni watu karimu na wenye Imani na kwamba hatajuta kulelewa nao. Anaendelea kumwambia kwamba watamkidhia mahitaji yake yote·Haya yote yanakuja kutokea Umu alipoanza kuishi nao. (170-171) V. Mwangemi anamwambia Mwaliko kwamba nduguze walikuwa hai na kwamba wangekutana. (uk170) hatimaye Mwaliko anakutana na ndugu zake Um una Dick wakiwa hai kwenye hoteli ya Majaliwa (uk189). VI. Subira anamfahamisha mwanawe Mwanaheri kwenye barua kwamba anapoisoma barua hiyo huenda asiwe ulimwenguni. (uk. 95) Mwishowe anapatikana akiwa amekufa baada ya kunywa kinywaji kikali (uk 97) WAHUSIKA NA UMUHIMU WAO Chandachema Mwanafunzi katika shule ya Tangamano. Ni mwanawe Rehema na Fumba ila amelelewa na nyanyake. I. Mdadisi - anawadadisi majirani zake akitaka kujua kitovu cha mamake mzazi baada ya mambo kumwendea tenge kwa jiraniye Satua. II. Mwenye bidi- alirauka alfajiri kufanya kazi ya kuchuma majani chai kabla kuelekea shuleni saa kumi na mbili asubuhi. III. Mwenye hekima- anapohisi kuwa ana uwezo wa kufanya kazi anaanza kuchuma majani chai ili kuwaondolea walezi wake Bi. Kimai na Bwana Tenge mzigo wa kumnunulia sare na madaftari. IV. Mwenye matumaini- anaamini kwamba siku moja atahitimu masomo yake na kurudi nyumbani kwao na kupajenga upya aidha anataka kusoma na kuwa mwanasheria au afisa mkuu wa maslahi ya kijamii. V. Mwenye mawazo mapevu- baada ya jiraniye Satua kuanza kulalamikia vitu vidogovidogo kama vile kuisha kwa sukari haraka, anang'amua moja kwa, moja kwamba hahitajiki hapo na kuondoka. pg. 90
VI. Mstahimilivu- anavumilia shida akiwa katika shule ya Msingi ya Kilimo hadi anapofanya mtihani wa darasa la nane - kwa mfano, kuna wakati alilala katikati ya michai au kwenye uchaga wa saruji uliotumiwa kama karo na wauza chakula sokoni. VII. Mwenye shukrani -analishukuru shirika la Kidini la Hakikisho la Haki na Utulivu kwa kumpeleka kwenye makao ya watoto mayatima ya Jeshi la Wajane wa Kristu alikosaidiwa baada ya kufanya mtihani wa darasa la nane na kukosa mfadhili. VIII. Mzalendo- anataka ahitimishe masomo yake kisha arudi kwao kupajenga upya. IX. Msiri - wafadhili wake, Tenge na Bi. Kimai wanahamishwa kuenda kufanya kazi katika shamba jingine lakini hamwambii mwalimu mkuu, Bi. Tamasha. Umuhimu wa Chandachema I. Ametumiwa kudokezea dhiki za Watoto wanaotelekezwa na wazazi wao. Baada ya kutelekezwa na wazazi wake anapitia dhiki zifuatazo mikononi mwa nyanyake: a) Kuishi kimaskini kwa maana nyanyake hakumudu mahitaji yake b) Upweke – baada ya kifo cha nyanyakealiyekuwa mlezi wake II. Ni mfano wa wanafunzi wanaothamini masomo. Licha ya masaibu yaliyomkumba, alikuwa na azma ya kujiendeleza masomoni III. Anaendeleza maudhui ya uzalendo kwani ana matumaini kwamba atahitimu masomo yake na kurudi nyumbani kwao kupajenga upya. IV. Ametumiwa kuonyesha ajira ya Watoto katika jamii. Licha ya kuwa mtoto anaajiriwa katika Shirika la Chai la Tengenea kuchuma majanichai ili kujikimu kimaisha. V. Usimulizi wake unachimuza dhiki za wafanyikazi wa kima cha chini Kwa mfano, anaeleza jinsi Bwana Tenge na Bi. Kimai wanavyoishi katika chumba kimoja ambacho ndicho malazi, mapokezi na Jikoni. VI. Ameturniwa kubainisha sifa za wahusika wengine kama uzinifu wa Tenge. Tenge alikuwa na mazoea ya kuzini na makahaba mkewe, Bi. Kimai anapoenda mashambani. VII. Ametumiwa Kuendeleza maudhui ya uwajibikaji. Anaanza kufanya kazi ili awaondolee wahisani wake, Bwana Tenge na Bi. Kimai mzigo wa kununua sare za shule na madaftari. VIII. Anaendeleza maudhui ya elimu - ana azma ya kusoma na kuwa mwanasheria au afisa mkuu wa masilahi ya kijamii. pg. 91
Katini Alikuwa jirani wa Chandachema. I. Mwenye utu. Anamsaidia Chandachema kubainisha kitovu cha mamake mzazi kwa kumweleza kwamba alikuwa mzaliwa wa Pwani II. Mtambuzi. Anafahamu kwamba Fumba alihusubiana kimapenzi na mwanafunzi wake Rehema na kuachishwa kazi kwa muda kisha akahamishiwa kwingine. Umuhimu wa Katini I. Ni kielelezo cha uwajibikaji. Chandachema anapoulizia kitovu cha mamake kutoka kwa majirani, anampa maelezo yanayompa mwanga kuwahusu mamake na babake. II. Ametumiwa kubainisha tabia za wahuskia wengine kama uzinifu wa Fumba. III. Anadhihirisha jinsi wanawake walivyo vyombo vikuu vya ukiukaji wa haki za binadamu kwa kueleza jinsi mke aliyeolewa na babake hangemlea kwa sababu aliamini kwamba kumlea mtoto wa mwanamke mwingine ni kuhatarisha maslahi yake katika ndoa. Mwimo Msubili Huyu ni babake Ridhaa. Babuye Mwangeka na Mwangemi. I. Mwenye ubaguzi. Hali inapokuwa ngumu kwa sababu ya kuwa na watoto wengi, anawahamisha wakewe wawili wa mwisho katika eneo la Msitu wa Heri/Ughaishu na kuwaacha wengine wakitaabika na wanao katika ardhi iliyokuwa ndogo mno. II. Mwenye tamaa- Tamaa ya kutaka kutambulika kama mkwasi kwa kuwa na watoto wengi inamchochea kuoa wanawake kumi wawili. III. Mwenye hekima. Aliamua kesi zote zilizowashinda wazee na mabaraza ya kijadi. (UK. 183) IV. Mshirikina-Hakupenda kukutana na wanawake asubuhi kwa kuamini kwamba kukutana nao itamsababishia nuksi kutofanikiwa kwa lolote alitakalo. (Uk. 184) V. Mwongo/mnafiki-Anamdanganya Mwangeka kwamba anataka kumtuma kwa Mutangili ilhali anataka kumchapa. pg. 92
VI. Mwenye bidii. Angekosekana nyumbani kwake kwa mwezi mzima akiwa katika shughuli za kutatua kesi katika taarafa ya Heri. Umuhimu wa Mwimo Msubili I. Ametumiwa kuonyesha athari za ndoa ya wanawake wengi: a. Ardhi aliyowagawia wanawe wa kiume ishirini ilikuwa ndogo sana/aliigawanya hadi ikawa vikataa. b. Hali ya kuwa na watoto wengi ilisababisha uhasama, migogoro na uhitaji mkubwa katika familia yake. I. Ni kielelezo cha Waafrika waliotaabishwa na wakoloni. Yeye pamoja na Waafrika wengine waliishia kuwa maskwota baada ya wakoloni kuwapoka ardhi yao/vibarua kwenye mashamba waliyokuwa wamepokwa na wakoloni. II. Anaendeleza maudhui ya ubaguzi. Ardhi yake inapokuwa ndogo anawahamisha wakewe wawili wa mwisho katika ardhi iliyo Msitu wa Heri na kuwaacha wengine kumi wakitaabika katika umaskini. III. Anaonyesha maudhui ya ushirlkina - hakupenda kukutana na wanawake asubuhi. Kwake kukutana na mwanamke asubuhi ilikuwa nuksi kwani mtu hangefanikiwa kwa lolote. IV. Anaendeleza maudhui ya bidii - angekosekana nyumbani kwake mwezi mzima akiwa katika ziara za kutatua kesi zilizoshinda wa mabaraza ya kijadi. Mama Ridhaa I. Mshauri mwema. Wanafunzi wengine wanapomdhulumu Ridhaa kwa sababu ya ukabila na Ridhaa kukataa kurudi shuleni anamshauri kuwa ni vyema kujifunza kuishi na wenzake bila kujali tofauti za ukoo na nasaba. II. Amewajibika. Anaposikia masaibu ya mwanawe Ridhaa, anaamua kuenda shuleni na kuzungumza na mwalimu ambaye anawahimiza wanafunzi kuishi pamoja kwa mshikamano hivyo kusitisha dhuluma na masimango dhidi yake. III. Mwenye mawazo mapevu. Anaelewa jukumu la elimu katika jamii -anamwambia mwanawe Ridhaa kwamba elimu inafaa kueneza amani na upendo wala si fujo na chuki. pg. 93
Umuhimu wa Mama Ridhaa I. Ametumiwa kukuza maudhui ya taasubi ya kiume. Anamshauri mwanawe Ridhaa kwamba unyonge haukuumbiwa wanaume bali wanawake, hivyo kumwonya dhidi ya tabia ya kike ya kulia pindi mtu akabiliwapo na vizingiti vya maisha. II. Anaendeleza maudhui ya uwajibikaji. Anaenda shuleni kuongea na mwalimu baada ya mwanawe Ridhaa kudhulumiwa na wanafunzi wenzake. III. Anaendeleza maudhui ya ndoa – anaolewa na Mzee Mwimo Msubili kuwa mkewe wa kumi na mbili. Ridhaa Ni mwanawe Mzee Mwimo Msubili aidha ni Mumewe Terry, Babake Mwangeka, Mukeli, Annatila (Tila) na Dede. I. Mshirikina- Milio ya Bundi na kereng'ende inamtia kiwewe na kuamini kwamba inaashiria kutokea kwa jambo fulani. II. Mwerevu- Alikua bingwa masomoni - alisoma hadi akawa daktari. III. Mwenye bidi-Utendakazi wake unamsababisha kuwa mkurugenzi wa mashirika mbalimbali yanayohusiana na huduma za kiafya. IV. Mwenye utu-Anayadhamini masomo ya wapwawe Mzee Kedi vilevile anamsaidia Selume kuajiriwa kama muuguzi. V. Mkarimu-amehakikisha kwamba kijiji kizima cha Msitu wa Heri kina maji ya mabomba. VI. Mshauri mwema- Anamshauri mwanawe Mwangeka kuoa tena baada ya kufiwa mkewe ili kuondoa upweke. VII. Mwenye mlahaka mwema na watu- tunaambiwa kwamba alipofika nyumbani kutoka kazini, wanawe Tila na Mwangeka walimkimbilia aidha alipenda kucheza na mjukuu wake Becky. VIII. Mwenye hekima- Alitumia hela alizozipata kuwekeza katika majengo, alikuwa na majengo matatu katika mtaa wa Tononokeni. IX. Mwenye msimamo dhabiti- licha ya kuraiwa na mwanawe mwangeka kubomoa mabaki ya jengo ambalo familia yao iliangamia anakataa katakata pg. 94
Umuhimu wa Ridhaa I. Ametumiwa kutuonyesha dhiki wanazopitia wakimbizi wakiwa kambini anasema kuwa walikula mizizi mwitu kutokana na ukosefu wa chakula. II. Anaendeleza maudhui ya utu kwa kuyadhamini masomo ya wapwawe wawili wa Mzee Kedi. III. Ametumiwa kubainisha maovu ya kijamii kama vile wizi kwa kueleza jinsi raia walivyotumia maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi kuwapora wenzao wenye maduka. IV. Usimulizi wake unadokeza athari za maandamano: a. Kujeruhiwa- mwanamume anakanyagwa na kujeruhiwa uti wa mgongo b. Uporaji- waandamanaji wanawapora raia wenzao wenye maduka. V. Ametumiwa kubainisha madhara ya tofauti za kiukoo. Familia yake inachomewa kwenye nyumba kwa sababu ya kutokuwa mwenyeji wa eneo la Msitu wa Heri VI. Anadhihirisha uwepo wa ushirikina katika jamii kwa kuamini kwamba jambo baya litatokea kutokana na milio ya kereng'ende na bundi. VII. Anafunza umuhimu wa mshikamano wa kijamii kwa kukubali mwanawe Mwangeka kumwoa Rachael Apondi licha ya koo zao kubaidika kama ardhi na mbingu. (uk116) . VIII. Ni kiwakilishi cha uwajibikaji katika jamii. Kwa mfano, anamzindua Selume kutafuta kazi iii kujigetemea kwa maana alikuwa na kisomo. Anamwambia kwamba siku za kuwa 'Mke Nyumbani' zimekwisha. IX. Anaendleza maudhui ya elimu. Alikuwa mwerevu masomoni aidha alisoma hadi chuo kikuu na kuwa daktari. X. Anaendeleza maudhui ya Utabaka.Kutokana na utajiri wake aliishi mtaa wa kifahari wa Afueni huku maskini kama Shamsi wakiishi mtaa wa Kazikeni. XI. Ridhaa ametumiwa na mwandishi kutuonyesha athari ya ukabila. XII. Ridhaa ni kielelezo cha watu wasiobagua watu wengine hakujali wanakijiji wenzake ni wa ukoo gani bali yeye alitekeleza miradi ya maendeleo ilikuwafaidi wote. XIII. Ridhaa ametumiwa kuuonyesha udhalimu wa watu kwa kuhadithia namna majumba yake yalivyobomolewa na kuchomwa pamoja na kuangamizwa kwa familia yake. pg. 95
XIV. Ridhaa ni kielelezo cha watu waliosoma na kuneemeka. XV. Ametumika kukuza wahusika kama vile Tila XVI. Kielelezo cha watu wenye bidii maishani XVII. Ametumika kukuza maudhui ya utu na udhanaishi Terry Mkewe Ridhaa, mamake Mwangeka, Mukeli, Tila na Dede. I. Mtani- alipenda kumtania mumewe kwa mfano kumwambia kuwa alivaa chepeo ili kuficha mvi II. Mpuuzaji-Mumewe Ridhaa alipomwambia kwamba milio ya bundi huenda iliashiria kutokea kwa jambo fulani anampuuza na kumwambia kwamba huo ni ushirikina. III. Mwenye mapenzi kwani tunaarifiwa kwamba alikuwa na mazoea ya kumpiga pambaja mumewe Ridhaa. (uk.37) IV. Mwenye mlahaka mwema na watu. Licha ya kuwa mlowezi katika eneo la Msitu wa Heri, yeye na mkewe Mzee Kedi walikuwa kama ndugu wa toka nitoke. V. Mcha Mungu – kwa alipenda kumwimbia mwanawe Mwangeka wimbo pendwa wa kidini iii kumwondolea udhaifu na mashaka aliyokuwa nayo baba yake aendapo katika safari zake za kikazi. VI. Katili – anamwadhibu mwanawe Mwangeka anapokosa kwa kumnyima chakula. Umuhimu wa Terry I. Anachimuza suala la athari za ukabila/tofauti za kiusuli/ kiukoo kwani anachomewa ndani ya nyumba kwa sababu ya kuwa mlowezi katika eneo la Msitu wa Heri. II. Anaendeleza maudhui ya uwajibakaji III. Anaendeleza maudhui ya mapenzi kwa kuwa na mazoea ya kumpiga mumewe pambaja. IV. Anaendeleza maudhui ya dini anapomwimbia mwanawe Mwangeka wimbo pendwa wa kidini V. Anaendeleza maudhui ya elimu kwani usomi wake unamwezesha kuchanganya ndimi katika mazungumzo yake. VI. Anaendeleza maudhui ya ukiukaji wa haki za Watoto anapomnyima Mwangeka chakula kama njia ya kumwadhibu. (uk 186) pg. 96
Mwangeka Mwangeka ni mwanawe Ridhaa na Terry, mkewe wa kwanza aliyechomeka ni Lily Nyamvula. Mwanawe aliyechomwa Pamoja na Lily anaitwa Becky.Ni nduguye Tila, Mukeli na Dede. Ni binamu wa Mwangemi Mkewe wa Pili anaitwa Rachael Apondi. Watoto wake na Apondi ni Sophie na Ridhaa. Ni mlezi wake Dick na Umu. I. Mwenye utu kwani anashirikiana na mkewe Apondi kumtunza Umu ambaye si mwanao - wanamwelisha hadi anapata Shahada katika uhandisi. II. Mshauri mwema kwani Ushauri wake na mkewe kwa Umu unamsaidia Umu kufanikiwa maishani. III. Amewajibika-Dick anapomwendea kuhusu ushauri wa kikazi, huwa anamsaidia. Pia ananunua kiwanja cha kujenga nyumba karibu na ufuo wa bahari baada ya kurudi kazini na kujenga nyumba yake. IV. Mwenye upendo- tunaambiwa kwamba alipendana na binamu yake Mwangemi kama chanda na pete V. Mwenye mawazo mapevu- akiwa katika darasa la sita alikuwa amefahamu mighani na tendi kama vile utendi wa Shaka Zulu. VI. Mwenye msimamo dhabiti-Licha ya mkewe wa kwanza Lily Nyamvula kumkataza kuwa askari, anashikilia msimamo wake hadi mkewe anakubali msimamo wake shingo upande. VII. Mbunifu- anaunda gari la kienyeji maarufu kijijini mwao kwa jina Ngookoo. VIII. MKarimu-Tunaambiwa kwamba yeye na mkewe Apondi walikuwa watu wa mkono wazi kwani waliwasaidia wahitaji kutoka kila pembe ya eneogatuzi lao. (uk. 116) IX. Mtiifu-Anatii rai ya babake aliyemtaka kuoa kwa kumwoa Rachael Apondi. X. Mwenye mzaha- akiwa mdogo alipenda kumfanyia babake mzaha kwani angeichukua stethoskopu ya babake na kuigiza kwamba anamtibu. Umuhimu wa Mwangeka I. Anaendeleza maudhui ya utu kwa kumchukua Umu kama mwanawe wa kupanga na kumlea kwa upendo. pg. 97
II. Ni kielelezo cha watu walio wakarimu kwani yeye na mkewe Apondi wanawasaidia wahitaji wanaomiminika nyumbani kwao kutoka kila pembe ya eneogatuzi lao. III. Ni kielelezo cha uwajibikaji kwani anaitikia wito wa Apondi aliyemtaka wamlee Umu kama mwanao wa kupanga. IV. Anaendeleza maudhui ya elimu - amesomea uhandisi katika chou kikuu. V. Anafunza maadili kama vile utiifu - anautii wito wa babake Ridhaa wa kuoa kwa kumwoa Rachael Apondi. VI. Ametumiwa kudokeza ukatili wa Mwimo Msublli - Mwimo Msubili anamchapa kwa mshipi anapomtania kwa kuigiza jinsi alivyokohoa. VII. Anaendeleza maudhui ya mapenzi – Tunaambiwa kuwa alipendana na binamuye Mwangemi kama chanda na pete. Rachael Apondi Mjane wa marehemu Mandu. Mamake Sophie na Ridhaa. Rafiki wa utotoni wa Mwalimu Dhahabu. Umu ni mwanawe wa kupanga. Anaolewa na Mwangeka baada ya kifo cha mumewe Mandu. I. Mshauri mwema kwani anapohutubu anawarai wananchi kuepuka vitendo vya kihalifu ili kudumisha usalama. II. Mtetezi wa haki. Anawasuta askari kwa kufyatua risasi ovyo na kuwaua raia wasiokuwa na hatia. III. Mwoga- baada ya kifo cha mumewe Mandu, anaogopa kuolewa mumewe mwingine asije akafa na kumwacha akiwa mjane tena. IV. Mkarimu- tunaambiwa kwamba yeye na mumewe Mwangeka walikuwa wakarimu kwa maana waliwasaidia wahitaji waliomiminika maskanini mwao kutoka kila pembe ya eneogatuzi lao. (uk.116) V. Mwenye utu- anakubali kumchukua Umu kama mwanawe wa kupanga baada ya kuombwa kufanya hivyo na Mwalimu Dhahabu. VI. Mwenye mapenzi- Mapenzi aliyomwonyesha Umu yaliponya banguzi alilokuwa nalo moyoni baada ya kutorokwa na mamake mzazi na kutengwa na nduguze. pg. 98
Umuhimu wa Rachael Apondi I. Hotuba yake inafichua uozo katika vikosi vya kudumisha usalama a. Askari wanashirikiana na wahalifu kutekeleza wizi ili wagane ngawira. b. Wanachelewa kufika mahali pa mkasa kuwaokoa manusura kutoka kwenye vifusi vya mabaki ya majengo, hivyo kusababisha maafa zaidi. c. Wanayaacha magari makuukuu barabarani kwa sababu ya kumilikiwa na vizito. d. Wanafyatua risasi ovyo, hivyo kusababisha vifo ambavyo vingezuilika. II. Ni kielelezo cha utetezi wa haki. Anawaonya askari dhidi ya kuwaua wahalifu kwa maana mtu ana haki ya kufikishwa mahakamani na kushtakiwa kabla ya kupewa adhabu yoyote. III. Anaendeleza maudhui ya uwajibikaji- mumewe Mandu anapofia ughaibuni kwenye shughuli za kudumisha amani, anakaa kwa miaka sita kabla ya kumpata mume wa kufu yake. IV. Ametumiwa kuhimiza jamii kuwasaidia wasiojiweza katika jamii. Yeye na mumewe waliwasaidia wahitaji kutoka kila pembeya gatuzi lao. V. Ametumiwa kuhimiza wanandoa kushauriana kwa kila uamuzi wanaoufanya katika ndoa yao. Mwalimu Dhahabu anapompigia simu akitamka kumchukua Umu kama mwanawe anamwambia kusubiri azungumze na mumewe kwanza ndipo amjibu. VI. Anaendeleza maudhui ya elimu – ana shahada katika taaluma ya masuala ya kijamii. VII. Anaendeleza maudhui ya utu - anamchukua Umu kama mwanawe wa kupanga na kumlea kwa mapenzi. lsitoshe, analipia masomo yake. VIII. Ni kielelezo cha ujenzi wa jamii mpya - licha ya kwamba suala la tofauti za kiukoo limekithiri nchini mwao, yeye anapinga suala hili kwa kukubali kuolewa na Mwangeka licha ya koo zao kuwa na uhasama. Tila/ Annatila Ni bintiye Ridha ana Terry. Ni dadake Mwangeka, Mukeli na Dede. Aliangamia katika mkasa wa moto I. Mwenye mawazo mapevu- hakuna aliyemsinda kwenye masuala ya sheria na siasa. II. Mwenye heshima kwani anamsalimu babake Ridhaa kwa heshima ‘shikamoo baba.’ pg. 99
III. Mtetezi wa haki- anataka kusoma na kuwa jaji kwenye mahakama kuu ili awasaidie wanyonge kwa kuamua kesi zao ambazo zimechukua miongo kadhaa kuamuliwa. IV. Mwadilifu- anataka kusoma na kuwa jaji mwadilifu ambaye atahakikisha kwamba kesi ambazo hazijasikizwa kwa miongo kadhaa zimesikizwa na wenyewe kupata haki. V. Mwenye utu- anasema kwamba akiwa jaji wa mahakama ya juu atahakikisha kwamba washukiwa walioselelea kwenye rumande bila kesi zao kuamuliwa watapata haki kwa kusikiliza kesi zao na kuziamua. VI. Mwenye matumaini- anaamini kwamba siku moja atakuwa jaji wa mahakama kuu. Umuhimu wa Tila I. Maelezo yake yanachimuza suala la ukoloni mamboleo. Kwa mfano wakoloni ndio wanaoamua kinachokuzwa katika ardhi ya Waafrika licha ya kwamba Wahafidhina ni taifa huru. II. Anaendeleza maudhui ya uwajibikaji kwani anataka kusoma ili awe jaji kwenye mahakama kuu ili kuwasaidia wanyonge ambao wameozea kwenye rumande bila kesi zao kusikilizwa. III. Anaendeleza maudhui ya utetezi wa haki- anataka kusoma awe jaji ili atatue kesi ambazo zimewasababisha washukiwa kuteseka kwenye rumande. IV. Anaendeleza maudhui ya elimu- yumo shuleni na anataka kusoma na kuwa jaji wa mahakama kuu. V. Ametumiwa kuonyesha ukatili wa Mzee Kedi kwani anamchoma Pamoja na baadhi ya watu wa familia yake baada ya ghasia za baada ya uchaguzi. Mzee Kedi Huyu ni jiraniye Ridhaa. Ndiye aliyemsaidia Ridhaa kununua ardhi kutoka kwa dada yake. I. Katili. Anaichoma familia, nyumba na mahindi ya Ridhaa kwa sababu ya tofauti za kikabila. II. Mnafiki kwani anajifanya mzuri kwa Ridhaa kumbe ni mtu mbaya. mfano, anamsaidia Ridhaa kupata shamba lakini hatimaye anaichoma familia yake. pg. 100
Search
Read the Text Version
- 1
- 2
- 3
- 4
- 5
- 6
- 7
- 8
- 9
- 10
- 11
- 12
- 13
- 14
- 15
- 16
- 17
- 18
- 19
- 20
- 21
- 22
- 23
- 24
- 25
- 26
- 27
- 28
- 29
- 30
- 31
- 32
- 33
- 34
- 35
- 36
- 37
- 38
- 39
- 40
- 41
- 42
- 43
- 44
- 45
- 46
- 47
- 48
- 49
- 50
- 51
- 52
- 53
- 54
- 55
- 56
- 57
- 58
- 59
- 60
- 61
- 62
- 63
- 64
- 65
- 66
- 67
- 68
- 69
- 70
- 71
- 72
- 73
- 74
- 75
- 76
- 77
- 78
- 79
- 80
- 81
- 82
- 83
- 84
- 85
- 86
- 87
- 88
- 89
- 90
- 91
- 92
- 93
- 94
- 95
- 96
- 97
- 98
- 99
- 100
- 101
- 102
- 103
- 104
- 105
- 106
- 107
- 108
- 109
- 110
- 111
- 112
- 113
- 114
- 115
- 116
- 117
- 118
- 119
- 120
- 121
- 122
- 123
- 124
- 125
- 126
- 127
- 128
- 129
- 130
- 131
- 132